TAKUKURU Shinyanga inamshikilia Joseph Jonas Tasia kwa kukutwa na doti mia sita (600) za vitenge vyenye nembo ya Chama Cha Mapinduzi na vya kawaida

TAKUKURU Shinyanga inamshikilia Joseph Jonas Tasia kwa kukutwa na doti mia sita (600) za vitenge vyenye nembo ya Chama Cha Mapinduzi na vya kawaida

TAKUKURU mkoa wa Shinyanga katika ufatiliaji wa vitendo vya rushwa kuelekea uchaguzi mkuu wa viongozi, manao tarehe 29/06/2020 majira ya saa tatu usiku mtaa wa Mwasele B nyumbani kwa Joseph Jonas Tasia ilikamata doti mia sita za vitenge zenye nembo ya Chama cha Mapinduzi na vya kawaida vikiwa vimehifadhiwa nyumbani kwake jambo ambalo linaashiria kuwa vilikuwa vinaandaliwa kutumika kufanya ushawishi kwa wapiga kura.

Aidha uchunguzi wa TAKUKURU umebaini kuwa Joseph Jonas Tasia ambaye ni mfanyabiashara wa magari madogo tax hana duka la vitenge wala hafanyi biashara ya vitenge.

Katika mahojiano na TAKUKURU Joseph Jonas alishindwa kutoa maelezo ya kutosha kuhusiana na mzigo huo wa vitenge na hata risiti za manunuzi ya vitenge hivyo hazikujitosheleza.
View attachment 1496341
Mwaka uchaguzi nina jamaa yangu dereva wa bodaboda ana bendera zote za CCM,CUF na CHADEMA yy hana chama anaangalia hela kote yupo hela yako tu.
 
  • Thanks
Reactions: Auz
sasa takukuru hawataki bibi zetu wale matunda ya uchumi wa kati
 
Doti 600 za Khanga na Vitenge vya CCM vyadakwa na TAKUKURU vikihisiwa kutaka kutumika kuwahonga wapiga kura kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020.

Kosa liko wapi apo,je kama anataka kuuza!?[emoji1787]au kuvaa na familia yake?au kwa sasa ni nyara za serikali hizo mbogamboga?!
 
Usanii tu uchunguzi wa takokuru wa baiskeli na pikipiki za Hamisi madigirii kule Igunga umeishia wapi!?

Doti 600 za Khanga na Vitenge vya CCM vyadakwa na TAKUKURU vikihisiwa kutaka kutumika kuwahonga wapiga kura kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020.

Takukuru wanaishi dunia gani? Kuna wanaofanya kampeni bila kujitangaza kwenye mavazi? Inategemea tu utamaduni wa eneo husika. Mfano Marekani, kama si kofia ni t-shirts, wao hawavai vitenge. Sasa Tz wajinadi vipi?
 
Sasa hapo rushwa iko wapi? Yaani hamna kesi kabisa. Sema kutishana kunamfanya asijiamini.
 
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Mkoa wa Shinyanga, imemkamata mfanyabiashara wa magari ya teksi, Joseph Tasia, akiwa na doti 600 za vitenge vyenye nembo ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) nyumbani kwake na kushindwa kutoa maelezo yanayojitosheleza.

Nipashe

TAKUKURU mkimaliza huko kote Mzukulu ninawaombeni sana ikiwezekana mkite Kambi Jimbo Tajiri la Kawe kwani kuna Makubwa yanaendelea.
 
Attachments

  • 2448897_facebook_106462946_1652883354871216_2490927066034797977_n.mp4
    1.8 MB
TAKUKURU mkoa wa Shinyanga katika ufatiliaji wa vitendo vya rushwa kuelekea uchaguzi mkuu wa viongozi, manao tarehe 29/06/2020 majira ya saa tatu usiku mtaa wa Mwasele B nyumbani kwa Joseph Jonas Tasia ilikamata doti mia sita za vitenge zenye nembo ya Chama cha Mapinduzi na vya kawaida vikiwa vimehifadhiwa nyumbani kwake jambo ambalo linaashiria kuwa vilikuwa vinaandaliwa kutumika kufanya ushawishi kwa wapiga kura.

Aidha uchunguzi wa TAKUKURU umebaini kuwa Joseph Jonas Tasia ambaye ni mfanyabiashara wa magari madogo tax hana duka la vitenge wala hafanyi biashara ya vitenge.

Katika mahojiano na TAKUKURU Joseph Jonas alishindwa kutoa maelezo ya kutosha kuhusiana na mzigo huo wa vitenge na hata risiti za manunuzi ya vitenge hivyo hazikujitosheleza.
View attachment 1496341
Mzigo wa Rushwa huo. CCM bila rushwa HAIWEZEKANI.
 
Back
Top Bottom