TAKUKURU: Uchunguzi sakata la Kangi Lugola na wenzie umekamilika. Jalada linapelekwa kwa Mwendesha Mashtaka (DPP)

Wanatuhadaa tu hamna lolote,hakuna historia ya mawaziri kuwahi kuhudumu katika wizara hii kushitakiwa moja kwa moja japokuwa ni wizara ambazo zimeishaitia hasara Taifa kwa kiasi kikubwa tu. Angalia Kitwanga,ilitengenezwa aonekane amelewa,akatolewa. Katika hali ya kawaida eti Charles aingie amelewa bungeni,siyo kweli.
 
Wadau,

Je, kweli anko Kangi Lugola ataepuka kikombe hichi, hususani baada ya Mkurugenzi Mkuu kutoa report ya uchunguzi waliokuwa wanafanya juu ya aliyekuwa waziri wa mambo ya ndani Ndugu Kangi Lugola ambapo anakabilwa na mashtaka ya kuhujumu uchumi na kupokea hongo.

Jalada la mashtaka limeshakamilika na linapelekwa kwa mwedesha mashtaka wa serikali DPP.

Nini hatma ya bwana Kangi hapa?
 
Taasisi ya kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini TAKUKURU imesema uchunguzi wa sakata la manunuzi ya vifaa vya zimamoto na uokoaji yasiyozingatia sheria na taratibu za nchi ambao ulisimamiwa na aliyekuwa Waziri wa mambo ya ndani KANGI LUGOLA na aliyekuwa Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto THOBIASY ANDENGENYE umekamilika kwa asilimia 99.9

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Brig. Jenerali John Mbungo, ameviambia vyombo vya habari kuwa uchunguzi umebaini makosa mengi katika mkataba wa manunuzi hayo ambayo kwa pamoja yanatengeneza kosa la uhujumu uchumi.

Baada ya kukamilika kwa uchunguzi huo TAKUKURU wanapeleka taarifa ya uchunguzi huo kwa Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali tayari kwa hatua za kisheria ikiwemo kuwafikisha mahakamani watuhumiwa wote 17 wa sakata hilo.
 
Kafara ya uchaguzi, Dana Dana za umesi zitaanza kama enzi za kina Basili Mramba na Daniel Yona, itaenda dana dana hadi uchaguzi uishe, halafu hukumu itafuata wakafagie hospital ya Mwananyamala.

Kwenye kufagia wataonyeshwa siku ya kwanza then basi michezo kwisha!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…