Tajirimsomi
JF-Expert Member
- Jan 12, 2017
- 4,824
- 5,587
Kwani unajuaje kama hakua na mishe nyingine ?Cheo Cha Mkuu wa wilaya kwa mshahara wa mil.4.1
Hawez kumudu kiwanja Cha mil.120
Sent using Jamii Forums mobile app
Bashite analiwa timing ajae.Kwa huu mgogoro inaonekana bado Makonda ana nguvu nchini kwa msuli alionao GSM hili suala lisingechukua dakika makonda angekuwa jela ila inaonyesha Bashite bado wamo
Makonda kajaaNashangaa wote wanaotoa mawazo yao kwenye hii mada wanataka Makonda achunguzwe alipata wapi fedha za kununua kiwanja sijasikia hata mmoja akisema huyo GSM achunguzwe alipata wapi hizo fedha za kununua kiwanja au nyie wote ni Yanga? Juzi hapa huyo GSM ameingiza malori mapya kama mwenda wazimu wala hakuna anayestuka au kuuliza au kwa sababu ya rangi yake? Sakala hili la Makonda mwenye akili atafahamu nani yupo nyuma ya hili sakata kuna jamaa alichukia Makonda kuhama kambi yake na kujiunga na kambi ya JPM na hii kazi aliyofanya ya kuwataja wauza unga baadhi wakiwa ni wa kambi ya huyo kigogo imesababisha. Hata huyo aliyefungua kesi ya kumshitaki Makonda inajulikana nani amefadhili fedha za kuendesha kesi. Hili la kiwanja kuna jamaa anahusika kwa njia fulani amefanyaje utakuja kusikia.Tusubiri muda utaongea lakini Tanganyika ya sasa ni ya watu kukomoana tusipoangalia watu wataanza kupoteza maisha kirahisi.
Ndo ngoja takukuru aingilie Kati akatuonyeshe Ayo mashamba na hivo visiki alivyokata izo mbao[emoji4]Kwani unajuaje kama hakua na mishe nyingine ?
Watu wanalima watu wana mashamba ya miti nk
Kwani unajuaje kama hakua na mishe nyingine ?
Watu wanalima watu wana mashamba ya miti nk
kwa. nini hakwenda kifanya transfer ili aliyepoteza akifuatilia anaambiwa hati imebadilishwa kiwanja sio chake,Yaani inawezekana walimpa hati halafu wakaripoti kupotea
Nijuavyo Mimi huu mchezo makonda aliucheza wakati wa Baba
Kwa mtu yeyote mwenye akili akiangalia issue nzima,utagundua tu kulikuwa na makubaliano kati ya hao wawili.Huyu anayejiita GSM ni marafiki wa Kikwete wanaotumia vibaya ,madaraka ya Kikwete Kama Rais msataafu kupora mali za watu.Yaan bongo ,mambo mengi yanaendeshwa kihuni tu.Unaingia mkataba ,baadae utawala umebadilika.Unadai umeibiwa hati.Watu wa aina hii ni hatari Sana.Swali .Kwann GSM aliuza hicho kiwanja?Kwanini amebadilika?Eti Sasa ameibiwa hati.Huo ni uhuni.
Angalia na wewe unapoishi, unaiba nini?Yote mijizi 2.
Mwaka mgumu kwa Makonda:Inawezekana GSM alilazimishwa kukiachia hicho kiwanja katika style ya Sabaya. Inawezekana wakati ule hakuwa na ujanja. Ikambidi akiachie.
Makonda anasema kiwanja hicho aliuziwa na GSM mwaka 2013. Hapo ndipo alipojichanganya. Mwaka 2013 Makonda alikuwa wapi? Alipata wapi zaidi ya milioni 100 za kununua hicho kiwanja?
Utata mwingine ni huu, nani alijenga jengo lililopo kwenye hicho kiwanja? Mkandarasi aliyejenga hapo alipewa kazi na nani? Ilikuwa mwaja gani? Kodi ya hayo malipo ililipwa TRA? Ililipwa na nani?
Kuna uwezekano hii kesi inakwenda kufukua mengi yaliyojificha.
Mwaka 2015 ndio aliupata UDC KinondoniSi alikua mkuu wa wilaya ya kinondoni
Dah ni umafia hatari, na liyeokota hati ni ndugu makonda.Serikali imesema inalichunguza sakata la aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda na mfanyabiashara Ghalib Said Mohamed (GSM) la kugombea kiwanja Na.60 kilichopo Regent Estate Manispaa ya Kinondoni jijini hapa.
Akizungumza mwisho wa wiki iliyopita, Wakili wa GSM, Alex Mgongolwa alisema mteja wake ana vielelezo vyote, huku Makonda akimtaka mfanyabiashara huyo kumwachia mai yake.
Akizungumza jana na Mwananchi kwa simu, Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (Takukuru), Salum Hamduni alisema suala hilo wanalifanyia kazi.
"Uchunguzi upo wa namna nyingi. Na mimi taarifa nimezisikia kupitia vyombo vya habari lakini tunaona kuna kazi ya kufanya katika hilo. Kwa hiyo tumelichukua tunalifanyia kazi," alisema Hamduni.
Akizungumza na gazeti hili kuhusu uhalali wa vielelezo vya wawili hao, Kamishna wa Ardhi wa Mkoa wa Dar es Salaam, Idrisa Kayera alisema vyombo vya Serikali vinavyochunguza suala hilo.
"Zinachunguzwa (hati) na mamlaka nyingine ili kujua uhalali wao. Sisi tukipata wakishatoa maelekezo tutaendelea na hatua nyingne.
"Kwa mujibu wa utaratibu ni kwamba mtu ukifanya uhamisho anatakiwa awasilishe ofisini, ili ijulikane, lakini hilo tumeziachia mamlaka zifanyie kazi ili kujua," alisema.
Alisisitiza kuwa hizo ni mamlaka za uchunguzi, bila kuzitaja, huku akizitaka pande mbili kwenda kushtaki kwenye vyombo vya Dola.
"Kwa sababu wao wenyewe ndio walihusika kwenye mkataba baina ya Makonda na GSM, wao wapeleke kule, majibu tutaletewa, wakisema hivi vitu havina uhalali tutachukua hatua," alisema.
Akifafanua zaidi, Kayera alisema GSM alishatoa taarifa idara ya ardhi kuhusu kupotea kwa hati ya kiwanja hicho, na alipewa nakala ya uthibitisho mwingine.
"Baada ya kutoa taarifa kuwa amepoteza na kwa mujibu wa sheria, ukipoteza hati unaleta taarifa, inatangazwa kwenye gazeti la kawaida, inatolewa certified, kwa mujibu wa kumbukumbu, hatua hizo zilifuatwa, lakini kwa sasa si rahisi kusema nani ni halali," alisema.
Chanzo: Mwananchi