Nyendo
JF-Expert Member
- Jun 4, 2017
- 1,336
- 4,731
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoa wa Dodoma imemrejeshea Bi. Frida Nahamani (62) mkazi wa Michese Jijini Dodoma kiasi cha shilingi milioni kumi (10,000,000) alizodhulumiwa na Bwana Maswe Wambura Mgaya ambaye ni mmiliki wa Taasisi ya SWAHILI TRUST MICROFINANCE ya Jijini Dodoma inayofanya kazi ya ukopeshaji fedha.
Uchunguzi wa TAKUKURU ulianza baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa Bi. Nahamani ambaye ni muuguzi mstaafu ambapo umeonesha kati ya Julai na Disemba 2018 alikopa fedha kiasi cha sh. 15,000,000/= na akakabidhi kadi yake ya benki kwa Taasisi hiyo ili warejeshe pesa yao mara baada ya mafao yake kutoka. Hata hivyo mnamo tarehe 31/1/2020 aliporudishiwa kadi yake alikuta hakuna kiasi chochote kwenye akaunti yake wakati alilipwa zaidi ya milioni arobaini na sita kwenye mafao yake
TAKUKURU imejirizisha kabisa kuwa Taasisi ya SWAHILI TRUST MICROFINANCE ilizidisha kiasi cha shilingi milioni kumi ambacho ilizidisha kwenye kukata marejesho na hivyo imelazimika kuzirudisha baada ya TAKUKURU kuingilia kati na kuwataka kufanya hivyo