Nimestushwa na Taarifa ya TAKUKURU. Wafanyakazi wa Bohari 30 wapo Mahabusu kwa kile kinachodaiwa kuwa walikuwa katika maandalizi ya kupiga mzigo wa Mil 254!
Huku aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa MSD akiendelea kutumikia mahabusu, wafanyakazi wake 30 wameingia kwenye kundi lilelile la kujaribu kuhujumu uchumi.
Taasisi ina Mkurugenzi Mkuu, ina Wakurugenzi, ina meneja, ina wasimamizi; hayo yote inawezekana vipi kutokea?
Sasa najaribu kuuliza zoezi la kuhesabu mali kwa miaka ya nyuma lilikuwa na udanganyifu kiasi gani? Bila shaka reconciliation ya miaka ya nyuma ilikuwa fake hatari.
Kuna haja ya serikali kutolea macho sana hiyo taasisi bado haijakaa sawa kabisa.
TAKUKURU wanadai kwamba hao wafanyakazi wanajitetea kuwa Dawa hizo zilikuwa zimeshamaliza muda wake wa matumizi.
Dawa zilizokufa zinahifaziwa vipi ndani ya ghala ? halafu humo humo kuna wafanyakazi, Je TMDA, OSHA mpo wapi kuhusu usalama wa maisha ya watu, hawa watu hawapo makini kabisa! Kuhifadhi Dawa zilizomaliza muda wake ni kuhifadhi sumu.
Matokeo yake ni wafanyakazi kufa na Saratani na kutojua chanzo chake ni nini.
Wizara ya Afya inapotoa takwimu za kuongezeka kwa ugonjwa wa Saratani, kuna haja pia kujumuisha sababu kama hizo za kukaa na madawa yaliyomaliza muda wa matumizi.
Ila Ukistaajabu ya Firauni, Utayaona ya MSD, Hospitali hazina Dawa, nyie dawa zinawafia humo humo. Aisee JPM kazi anayo sana.
Ushauri wa wazi kabisa kwa Mkurugenzi Mkuu Mpya, tunajua hili pia sio lake, ni lazima litakuwa ni muendelezo wa Utawala uliopita; lakini pia Brigedia Mhidze alichunguze vema hili tukio. Isijekuwa ni katika harakati za kumtia DOA huyo Mkurugenzi Mpya. Sehemu yoyote yenye Ulaji Fitna hazikosi. Kuna kitu hakipo sawa hapo Bohari Kuu!
Kubwa kuliko, Mkurugenzi Mpya akitaka kufaulu afumue hiyo taasisi kichwa chini miguu juu. Ni wazi kuwa tatizo sio watu, tatizo ni mfumo. Kama utabadili watu na mfumo ni uleule, bado ni tatizo.
Kama utabadili mfumo na ukabadili na watu hasa wale ambao ni bogasi na wapo sehemu za maamuzi, hapo utakuwa umefaulu.
Vinginevyo drama zitakuwa nyingiiiii mwishowe wote mnadondokea pua.
Ila TAKUKURU, hii ishu ya Kangi Lugola imeishia wapi? mnakomaa na vi Mil 254, mnaacha Tril za pesa na perdiem za nje ya nchi walizokuwa wakilipana, acheni drama na muwe Serious. Kama mnapambana na Rushwa pambaneni na Rushwa kwa Wote.
Au kupambana na Rushwa kuna matabaka?
I hate kuona dagaa wakisumbuliwa halafu wale masterminder wanazungushiwa mlango wa nyuma. Acheni hiyo mambo. Tatizo la Rushwa hapo Tanzania ni kubwa.
Lifanyieni kazi kumsaidia Rais majukumu yake.