Takwimu za Al Masry ni za kawaida wala hazitishi

Takwimu za Al Masry ni za kawaida wala hazitishi

Hao jamaa sio wa kuwachukulia poa. Kuna game yao na pyramids niliicheki juzi juzi tu hapa iliisha 0-0. Pyramids alipigiwa mpira mkubwa pale pale nyumbani kwake
We waache tu,timu yenyewe streka ateba,wanakula nne imara hao
 
Simba fanyeni kila liwezekanalo ili mtolewe kwenye hii hatua. Aisee kufika fainali siyo kazi nyepesi! Waulizenu kaka zenu wa Yanga wawape mbinu! Lazima uwe mkatili kwenye kupindua meza.

NB: haya siyo yale mashindano ya bonanza ya zamani. Hapa unatakiwa uvimbe kweli kweli hata kama kombe lenyewe ni looser cup!
Hebu acheni kujitoa ufahamu yani muwape simba mbinu kwa kukutana na vibonde kina rivers united na marumo gallants kwenye hatua za robo na nusu, mngekutana na wenye kombe lao kina zamalek na berkane kwenye hizo hatua nawahakikishia mngeishia robo, yani na kikosi chote kile bado mkashindwa kuchukua lile kombe mbele ya usm alger mnakuja kutupigia kelele na medali halafu eti mnataka muwape simba mbinu mtawapa mbinu gani sasa
 
Kuelekea mchezo wa Al Masry dhidi ya Simba katika Kombe la Shirikisho Afrika, hizi ni takwimu za Al Masry na Simba katika hatua ya Makundi.

Kwenye michezo sita ya makundi,
Al Masry kafanya ifuatavyo;
Kashinda - 2
Kadroo - 3
Kafungwa - 1
Kafunga goli - 7
Kafungwa goli - 4
Clean sheet - 2

Hii inatoa taswira kwamba Simba Sports akikomaa vizuri huyu mwarabu koko anafungika vizuri bila shaka.

Kila la heri kwa Simba Sports, wawakilishi sahihi wa Tanzania kimataifa
View attachment 3287651
Ni sawa lakini pia uweke akiba ya maneno kwamba ubora wa ligi ya misri na ushindani sio sawa na ligi ya Tanzania,,kibonde wa misri anaweza kutoa ushindani mkubwa kwa title contender wa ligi ya Tanzania!
 
Attachments

  • Screenshot_2025-03-31-00-12-33-037.jpg
    Screenshot_2025-03-31-00-12-33-037.jpg
    264.5 KB · Views: 28
Niliangalia mechi yao na Pyramids kwenye ligi, Al Masry wanaubonda mpira acheni kuchukuliwa vitu kiuwepesi,Simba ipambane ipate draw ije kumaliza game Tanzania ila sema ukweli majamaa si wepesi kama unavyowaza.
Wewe acha ujuaji, ni sehemu gani nimesema wepesi? Shule ulienda kusomea ujinga
 
Wewe huna akili. UCL imeanzishwa mwaka gani? Ukishajua nenda kaangalia bingwa wa kihistoria Real Madrid kombe la kwanza kachukua mwaka gani?
Kama uefa cup iliyovunjwa 1999 ni europa cup,mbona UEFA hawahesabu arsenal ana europa moja,maana hilo kombe arsenal alishinda 1994
Al ahly alishinda caf winners cup 1993 baada ya kumfunga african sports, stella alishinda caf cup 1993 baada ya kumfunga simba,kwa hiyo al ahly na stella walishinda kombe la shirikisho 1993!?
 
Asante sana kwa Takwimu mkuu.
Jamaa hawatishi sana na hawana Timu nzuri kiasi hicho.

1. Simba nayo sio timu bora sana bado ina wachezaji wa kawaida mno Daraja C&D.

2. Wachezaji Muhimu sana wa Simba Daraja A ambao hawazidi wa 5 kwenye timu wana majeruhi wawili
Kamara na
Che Malone Fondoh..

3. Usisahau pia hatua za Mtoano hawaangalii sana Ubora wa Timu au matokeo ya Nyuma.
Hapo ni kuwa na wachezaji wanaoweza kuamua Mchezo mkubwa.
Yani namaanisha hapo uwe na quality ya Juu kama
Mayele.
Chama nk.

4. Ukweli mchungu sana lakini simba ina mchezo Mgumu mno ikitoboa hapo inachukua Ubingwa otherwise iuze kama 1993
Leo rasmi toka kuponda Mashabiki wa Simba na Yanga kuwa wapumbavu hadi wewe mwenyewe kuwa Mwandamizi kungwi wa Wapumbavu...🤭

Ubinadamu ni kazi/The humanity is work.

Ubinadamu ni kazi/The
 
Kawaida Simba huishia robo fainali mashindano ya CAF, na hata huko watabondwa tu na marudiano kupewa droo labda kama wameenda na wale wazee wafupi na mbuzi!
 
Simba ilishacheza final shirikisho mwaka 1993,Rais Samia aliwathibitishia mlipo mualika kwenye Tamasha lenu baada ya kufika final 2023
Mbumbumbu hamkujua kua Rais alikua ana balance story ilimsijione wanyonge? ukizingatia mlikua na mwaliko rasmi kuwapongeza kaka zenu kwa kuiheshimisha nchi.
 
Hebu acheni kujitoa ufahamu yani muwape simba mbinu kwa kukutana na vibonde kina rivers united na marumo gallants kwenye hatua za robo na nusu, mngekutana na wenye kombe lao kina zamalek na berkane kwenye hizo hatua nawahakikishia mngeishia robo, yani na kikosi chote kile bado mkashindwa kuchukua lile kombe mbele ya usm alger mnakuja kutupigia kelele na medali halafu eti mnataka muwape simba mbinu mtawapa mbinu gani sasa
Kwani Berkane hakushiriki hiyo michuano ya msimu huo? Si alishiriki lakini kashindwa kufurukuta mbele ya Monastir ambao ndiye akawa kundi moja na Yanga? tatizo hamtaki kukubali uwezo wa Yanga mnatafuta namna ya kuonekana timu zilikuwa ni vibonde kisa sio timu maarufu
 
Hoja ni kwamba mahali ambapo yanga wana uwezo wa kufika wakiwa na kikosi bora simba wana uwezo wa kufika wakiwa na kikosi kibovu, msimu jana simba walikuwa na kikosi kibovu ambacho karibu kila shabiki alikikatia tamaa lakini walifika na kuishia robo fainali cafcl sawa na yanga tu ambao walijinasibu kuwa na kikosi bora, ninyi mkiwa na kikosi mlichokiita bora huku mna striker kama mayele mlishindwa kubeba hilo kombe la cafcc matokeo yake mnakuja kuturingishia medali kana kwamba ninyi ni wanariadha kumbe ni timu ya soka
 
Hatakama hao almasiri takwimu zao hazi tishi ila Simba ni wa dhaifu sana kwa zile back pass zao na kawaida yao wataruhusu goli la mapema sana ndiyo waanze kujitafuta.
 
Hoja ni kwamba mahali ambapo yanga wana uwezo wa kufika wakiwa na kikosi bora simba wana uwezo wa kufika wakiwa na kikosi kibovu, msimu jana simba walikuwa na kikosi kibovu ambacho karibu kila shabiki alikikatia tamaa lakini walifika na kuishia robo fainali cafcl sawa na yanga tu ambao walijinasibu kuwa na kikosi bora, ninyi mkiwa na kikosi mlichokiita bora huku mna striker kama mayele mlishindwa kubeba hilo kombe la cafcc matokeo yake mnakuja kuturingishia medali kana kwamba ninyi ni wanariadha kumbe ni timu ya soka

Yanga aliishia robo fainali lakini mazingira ya Yanga kuishia robo fainali CAFCL hayafanani na Simba?
Yanga walicheza mechi ya robo fainali mkondo wa kwwanza bila uwepo wa wachezi muhumu wa kikisi cha kwanza ambao ni Aucho, Pacome na Yao Kwasi. Mechi ya marudiano pia hawakuwepo hao wachezaji muhimu na mbaya zaidi kule South Africa ilipatikana goli ila VAR iliyokuwa uwanjani haikutumika ipasavyo katia kuangalia uhalali wa hilo goli.

Mechi ya CAFCC hatua ya fainali, mazingira ni yale yale katika mechi ya kwanza ilichezwa pasipo mchezaji muhimu katika nafasi ya kiungo (Aucho) ikapelekea Yanga kuruhusu magoli mawili.

Simba iwe na kikosi bora ni hapo hapo robo fainali, ikiwa na kikosi kibovu ni hapo hapo robo fainali tokea msimu wa 2018/2019 ndio hatua hiyo hiyo tu mnayoishia na hamsongi mbele. Safari hii msonge mbele
 
Back
Top Bottom