fundi radio
Member
- Apr 2, 2023
- 52
- 95
UTANGULIZI.
Kipindi , Rais akiwa Hayati B.Mkapa alijitahidi sana kwenye kuboresha Taasisi, mashirika, wizara za Serikali zifanye kazi Kwa ufanisi Kwa kuwaweka watu makini na wenye ujuzi unao stahili kwenye vitengo mbalimbali vya Serikali.
Moja ya sera yake kubwa ilikuwa ni UKWELI NA UWAZI,
Kipindi hicho mpaka Sasa ukimwi na malaria ndio magonjwa Yanayoongoza Kwa wingi wa vifo nchini.
Kupitia wizara ya afya ya kipindi hicho ilijitahidi kushirikiana Taasisi na mashirika mbalimbali ya kiafya Katika kubadilishana taarifa za kiafya. Hii ilipelekea Serikali ya Tanzania kupata misaada mingi ya kiafya. Mfano Kwa kupata dawa za kufubaza virusi vya ukimwi Bure, kupewa chanjo za magonjwa mbalimbali Kwa watoto Bure. Serikali kupewa rasilimali mbalimbali za kupambana na ugonjwa wa Malaria.
2005 Alipokuja Mzee Jakaya aliendeleza diplomasia safi, ya kaka yake Hayati B.Mkapa , na akaenda mbali zaidi mpaka wafadhili kugawa vyandarua Bure Kwa wananchi mjini na vijijini nchini Tanzania.
Kigezo kikubwa Cha Hawa wafadhili kutoa michango na ufadhili wao ilikuwa ni siasa za "DEMOKRASIA SAFI", "UKWELI NA UWAZI" Kwa utendaji wa Serikali Kwa wananchi wake, ni kweli hawawezi kutoa pesa zao Kwa Serikali inayo pika kazidata,kwani hizo pesa zitatumika kinyume na makusudio yaliyowekwa.
Utakatishaji mkubwa wa taarifa za afya ulivoanza kumea.
2015, Wakajinadi kuwa wao ni nchi tajiri, kwamba wanajitosheleza kwenye matumizi, na kuita wadau wa maendeleo ya afya kuwa ni mbuzi dume "BEBERU" bila kusahau barakoa wanaagiza kutoka Kwa "BEBERU" hii ni baada kupuuzia utawala Bora na WA kidemokrasia.
Baadhi ya wadau wa maendeleo ya afya, kusikia wanavyozodolewa , hii Hali Ili washangaza sana na Iliwaudhi ukizingatia pesa wanazotoa ni za walipa Kodi wa wananchi wao na wanatoa Kwa nia njema TU kutusaidia sisi walalahoi, wakaanza kupunguza misaada na wengine kujitoa kabisaa.
Wazee baada kuona wamesusiwa kwenye masuala ya afya , wakaona njia pekee ya kuficha makosa, ni kutoa waraka wa Siri wa kuchakachua kanzidata za Malaria kuanzia wizarani mpaka ngazi za wilaya, aisee ilikuwa ni hatua mbaya sana waliyo amua kuichukua , sijui walijiamini Nini
Kanzidata za Malaria ndio zilikuwa zinachakachuliwa, na kazidata za ukimwi na VVU zilikuwa zikifichwa.
Yani Iko hivi, Kwa Vituo vya afya za kata ,wilaya mkoa ziwe za kibinafsi au za Serikali Kwa wagonjwa watakaopimwa na kukutwa na Malaria hawatakiwi kufikia 100 Kwa mwezi 1, wanataka 20,39 hivi, idadi ikizidi utawaeleza ni kwanini
Nakama kituo Cha binafsi kikakiuka hili agizo, wakaguzi wa wizarani,manisipaa,wakija kukagua na wakakuta umekiuka, wanawatishia kuwafutia leseni. na hii suala bado linaendelea mpaka hivi sasa.
Ukienda kupima malaria majibu yanakuja damu Yako chafu, mara una UTI , .
Ila wanafanya hivi Kwa watu wakubwa TU, na sio Kwa mama mjamzito, aliyejifungua mtoto na watoto wadogo.
Tanzania mpaka hivi sasa Ina Vituo vya utafiti wa ugonjwa wa Malaria visivyo pungua vitano, lakini Cha ajabu mwaka huu tumekosa chanjo za majaribio za Malaria,ambazo pia zinatokana na matokeo ya tafiti za Vituo vyetu, majirani zetu, Kenya, Uganda, Burundi wamepewa. Kwanini sisi tunakuwa tuko nyuma , Moja Kwa Moja shida ipo wizarani, hawatoi ushirikiano mzuri kwa madau wa afya wa kimataifa ikiwemo kuwapa taarifa sahihi na usheleweshaji wa vibali.
Maadhimisho ya siku ya ukimwi duniani 2022 yaliyo fanyika mkoani lindi, Balozi wa marekani wa kipindi hicho alisema Serikali ya marekani kupitia mfuko wa (PEPFAR) imeshatoa Dola za kimarekani bilioni 6 tokea mwaka 2003 Kwa ajili ya Tanzania pekee.ukiwa ni ufadhili mkubwa zaidi duniani uliowahi kutoa Kwa ajili ya kupambana na aina Moja ya ugonjwa.
Je Serikali ya Tanzania Ina Nia ya dhati ya ifikapo 2030 UKIMWI uwe umekwisha?.
Bajeti ya mwaka huu (2023-2024) ya kununua dawa za VVU ni bilioni 22 ivi, ya mwaka uliopita ilikuwa ni bilioni 12, unaweza jiuliza maswali mbona bajeti imeongezeka mara mbili ndani ya mwaka mmoja TU,
(I) je maambukizi yameeongezeka zaidi.
(ii) bajeti iliyopita haikutosha , kwa hiyo kuna wagonjwa wengi sana walikosa dawa.
(iii) je bajeti hii nayo itatosha kweli, maana data kamili zinafichwa sana.
Mwaka 2018,waliokuwa na maambukizi ya VVU idadi Yao ilikuwa ni 1.6milioni , maambukizi mapya Kwa mwaka huo ilikuwa ni 74,000, na vifo vya ukimwi ilikuwa ni watu 24,000. Data kutoka Serikalini.
Mwaka 2010 vifo vitokanavyo na malaria vilikuwa 15,915, mwaka 2021 vifo vilikuwa 1,920 , mabadiliko chanya yanaonekana kwa upande wa ugonjwa wa malaria, je ni kweli hii namba Ina akisi Hali husika?
Hali ilivyo Sasa kwenye Vituo vya afya.
Upungufu mkubwa wa wataalamu uchunguzi wa kitabibu wa maabara, Kwa ngazi za kata, wilaya, mkoa pia inaenda sambamba na upungufu wa vitendea kazi.
Nini kitakacho tokea, wananchi watakao patiwa matibabu ya uchunguzi wa maabara watakuwa Wachache kwasababu ya upungufu wa wataalamu, vifaa tiba na gharama za matibabu, Kwa hiyo Wananchi wengi Baadhi Yao wataishia kupewa dawa bila uchunguzi makini wa kimaabara.
Kwa hiyo wakija wakaguzi kuchukua repoti, watakuta waliopatikana na malaria, ukimwi ni waChache, na wataiyaindikia repoti hiyo kuwa ni chanya kumbe sio ukweli, wa mambo yanayo tokea kwenye Vituo vya afya kiutendaji wake.
Athari za kuchakachua ripoti za Malaria na kuficha data za maambukizi ya UKIMWI.
MTAMBUKA.
Serikali isione aibu kutangaza taarifa za afya. Ikiofia aibu, taharuki, kuonekana wazembe. Ni lazima Serikali iwajengee wananchi wake uwezo wa kujitambua . Itasaidia wananchi kuchukua hatua sahihi dhidi ya kupambana na haya magonjwa, kwani swala la afya linaitaji elimu.
Suluhisho
I) Serikali ishirikiane na wadau wa maendeleo ya afya bega Kwa bega mfano -USA, UK, EU, Hawa wadau Wana mchango mkubwa sana nchini .
II) Kuwe na tume huru itakayochukunguza kukagua takwimu za wizara ya afya.
Maono Yangu
Kutokana na maendeleo makubwa ya teknolojia na sayansi naamini kabisa , Kwa siku zijazo tutapata chanjo ya Malaria, na tutapata chanjo ya ukimwi.
KATIBA MPYA (ya warioba) iwekwe mezani Haraka sana, na ipitishwe. Nchi inaelekea kubaya hii.

- Misaada inayotolewa hasa kwa upande wa malaria kuwa pungufu, kwa sababu repoti wanazopewa wahisani haziakisi Hali halisi.
- Malengo ya umoja wa mataifa ifikapo 2030 UKIMWI duniani uwe umeisha kutowezekana, Kwa sababu hamasa ya uelimishaji imepungua.
- Vifo vitokanavyo na malaria, ukimwi kutorepotiwa kwa wakati sahihi.

Upvote
1