Tales from another World: Uzi maalum wa kusimulia ndoto tunazoota (Just for fun)

Tales from another World: Uzi maalum wa kusimulia ndoto tunazoota (Just for fun)

Stephen Ngalya Chelu

JF-Expert Member
Joined
Oct 31, 2017
Posts
8,252
Reaction score
18,335
Ndoto ni kama movies ambazo zinatengenezwa akilini mwetu. Wakati tukiwa tumepumzika usiku, ubongo huwa upo kazini bado, hutuandalia ulimwengu mpya ambao huwa na mambo tofauti na haya tuyaonayo kwenye ulimwengu wetu huu wa kawaida. Mengine ya kufurahisha, kushangaza na hata kuogofya.

Hivyo basi, si vibaya kama tukashiriki pamoja maajabu ya ulimwengu wa ndoto. Uzi huu hauna lengo la kuuliza maana ya tafsiri za ndoto, it's just for fun and enjoying the experience from the other side...

Mimi naanza na hii ya leo hapo chini...​
 
MLIPUKO WA NYUKLIA ULIVYOONDOKA NA MARAFIKI ZANGU WENGI

Tulikuwa kwenye taasisi moja ya elimu, mimi pamoja na rafiki zangu kadhaa ninaowafahamu katika maisha ya kawaida tulikuwa kama wanafunzi katika taasisi hiyo. Na tulikuwa pale tukifanya utafiti wa kutengeneza kifaa cha kinyuklia. Kifaa hicho kilikuwa na mwonekano kama wa engine ya gari (nahisi hii inatokana na jana mchana niliangalia video huko youtube inayohusu injini ya gari inavyofanya kazi).

Basi bwana, wakati tukiwa katikati ya shughuli ile, mimi niliamua kutoka nje ya kile chumba kwenda nje japo sikumbuki nilikuwa naenda kufanya nini. Ile nakaribia mlangoni, kile kifaa kikalipuka. Cha kushangaza ni kuwa wakati kile kifaa kinalipuka muda ulianza kwenda taratibu, kama vile video ya slow motion. Nikawa nawaona washkaji waliokuwa jirani na kile kifaa wakimezwa na moto wa ule mlipuko. Pia nilikuwa nahisi jinsi joto linavyopanda kwa kasi kutoka joto la kawaida hadi kuwa kali sana.

Baada ya sekunde kama 2 au 3 za slow motion, speed ya muda ikarudi kama kawaida so nikajikuja nimetupwa nje mbali kabisa. Nilingua kwenye mkono wa kulia japokuwa majeraha yalikuwa siyo makubwa. Kukawa na taharuki, watu wakawa wanakimbia kimbia hovyo na vilio kila kona. Basi timu za uokoaji zikaja pale wakawa wanatusaidia. Watu wengi walikuwa wana majeraha ya kuungua na moto.

Sasa bwana katika ile timu ya uokoaji iliyokuja, kuna jamaa mmoja akawa anakuja anatushika mikono na kuangalia ule mstari iliopo kwenye ngozi unaotenganisha kiganja na mkono. Kwa mujibu wake, huo mstari alikuwa anauita 'Pulgatory line'. Anasema huo mstari unabeba taarifa za DNA ya ngozi ya mhusika. Mistari hii imegawangika kama makundi ya damu, ila yenyewe inatambuliwa kwa combination 5 za majina matatu ambayo nimeyasahau. Ila mfano wake ni kama kuwe na majina matatu kama alpha, beta na sigma; halafu hayo majina yatengeneze jina moja kwa combination tano. Mfano pulgatory line ya mtu mmoja inaweza kuwa alpha, alpha, beta, sigma alpha, na ya mwingine ikawa beta, sigma, alpha, alpha, sigma nk. Na hizi combination mnaweza kufanana na mtu mwingine kama ilivyo kwa makundi ya damu.

Kwa hiyo huyu jamaa akawa anakuja anatuuliza jina, anaandika kisha anaangalia huo mstari kwenye kiganja then utamsikia anataja na kuziandika combination za hiu mstari wako. Lengo la kufanya hivyo alisema ni kwa sababu mlipuko huo ni wa nyuklia hivyo mionzi inaweza kuathiri DNA zetu na kusababisha ngozi zetu ziharibike. Kwa hiyo watakachofanya ni kwenda mtaani kwa watu wengine na watawatafuta watu ambao wanafanana na sisi zile combination za hiyo mistari then kuna vitu watavichukua kwao na kuja kutuwekea sisi ili tusiathirike na hiyo mionzi ya nyuklia.

So wakati zoezi hilo linaendelea nikaamka toka usingizini. Niliipenda hii ndoto maana imekaa kama movie ya sci-fi from the future...​
 
Wiki ilopita niliota nipo China bila document wala mishe, naishi kama digidigi maana maafisa wa polisi wananisaka kila kona bila mafanikio. Nikawa najificha makanisani na shule zisizokuwa na wanafunzi, naishi kwa hofu sababu kila mahali wamebandika matangazo kuonesha nipo kwenye list ya wanted. Nilipoamka na kugundua ni ndoto nilifurahi sana.
 
Ndoto ni kama movies ambazo zinatengenezwa akilini mwetu. Wakati tukiwa tumepumzika usiku, ubongo huwa upo kazini bado, hutuandalia ulimwengu mpya ambao huwa na mambo tofauti na haya tuyaonayo kwenye ulimwengu wetu huu wa kawaida. Mengine ya kufurahisha, kushangaza na hata kuogofya.

Hivyo basi, si vibaya kama tukashiriki pamoja maajabu ya ulimwengu wa ndoto. Uzi huu hauna lengo la kuuliza maana ya tafsiri za ndoto, it's just for fun and enjoying the experience from the other side...

Mimi naanza na hii ya leo hapo chini...​
Kama ingekuwa uzi wa ku exprole ulimwengu wa ndoto zile ndoto zenye kuacha maana au kupush mtu atafute maana, Uzi ungekuwa MTAMU sanaaa.

Tungeyajua mengi sana ya ulimwenguni, mambo ya LUCID dreams , kuna wale wanaoweza kuongoza ndoto zao, kuna wale wanaota ndoto zenye muendelezo. Uzi ungekuwa fantastic sanaa, ila tunapenda sana burudani
 
Kama ingekuwa uzi wa ku exprole ulimwengu wa ndoto zile ndoto zenye kuacha maana au kupush mtu atafute maana, Uzi ungekuwa MTAMU sanaaa.

Tungeyajua mengi sana ya ulimwenguni, mambo ya LUCID dreams , kuna wale wanaoweza kuongoza ndoto zao, kuna wale wanaota ndoto zenye muendelezo. Uzi ungekuwa fantastic sanaa, ila tunapenda sana burudani
Hizo mada zipo kibao humu na tashazijadili sana. Nenda kule jukwaa la inteligence utazikuta...
 
UHALIFU WA KUTUMIA SILAHA

Usiku wa kuamkia leo niliota mimi na rafiki zangu kadhaa tukiwa na mtu mmoja maarufu ambaye sitopenda kumtaja ila anapatikana kwenye kiwanda cha muziki wa bongo fleva. Tulikuwa tunatembea miguu mtaani huku huyo mtu maarufu akitueleza mambo mbalimbali kuhusiana na kazi yake ya muziki.

Sasa ikafika mahali tukawa tunavuka barabara, wakati tunavuka almanusura tugongwe na gari. Tulipovuka, gari moja lilisimama na nikasikia sauti ya mtu mmoja kwenye gari inasema 'Nchi inahitaji watu watano wafe ili ikae sawa, kwa hiyo amebaki mmoja' Baada ya hapo niliona mtu mwingine aliyekuwepo kwenye hiyo gari akitoa bastola na kumfyatulia risasi mtu aliyekuwa anapita pembeni ya barabara.

Baada ya kusikia tu milio ya risasi watu wote tukaanza kukimbia hovyo. Wale jamaa walishuka kwenye gari wakaanza kuua watu hovyo mtaani. Yaani ilikuwa ni mwendo wa milio ya risasi na vilio, hasa vya kina mama. Mimi binafsi nilishuhudia watu kama wanne wakipigwa risasi.

Basi, vurugu zikaendelea. Mimi na waskaji kadhaa tukaenda kujibanza kwenye ukuta wa nyumba moja hivi. Muda mchache baadae tukaona wale jamaa wanakuja. Mmoja akatuona, akawa anakuja tulipo. Alipofika nikamuwahi nikamyang'anya bastola ile nataka nimtwange risasi kumbe bastola imeisha risasi. Mwenzake alipoona hivyo akaninyooshea bastola, alipofyatua tu risasi nikaamka.​
 
URAFIKI WA KINAFKI, UTAFITI WA KISAYASI NA ONYESHO LA STAND-UP COMEDY (CHUKI NA UPENDO VINAPOONEKANA BILA KIFICHO)
Ndoto yangu ya leo ilikuwa ndefu sana na ina mambo mengi kweli, hivyo nitaikatisha kwa kuanzia mbele kidogo maana mwanzo wake nimeamka siukumbuki vizuri...

Urafiki wa kinafki
Ndoto yangu ilianzia somewhere ambapo nimesema sitosimulia kwa sababu sikumbuki vizuri, lakini baada ya kutoka huko, nilienda mitaa jirani na stand ya daladala ya makumbusho kwenda kupata chakula. Kuna chakula fulani nilikuwa nakitaka, nilipoulizia nikaambiwa ni sh 30000, na mimi kwenye wallet nilikuwa na hiyo hiyo 30000. Kwa hiyo nikamuambia mhudumu anipatie chakula chochote cha bei ya chini.

Basi akaniletea chakula flani hivi kama ubwabwa, kama biriani vile, yaani hakieleweki, nikala fresh. Baada ya kumaliza nikamuuliza bei akasema ni elfu kumi. Basi ile nazama nitoe wallet, kuna rafiki yangu mmoja akanilipia hiyo hela. Nilishangaa kwa sababu hakuwepo pale. Pia huyu rafiki yangu kwenye maisha ya kawaida urafiki ulishakufa sababu ya pesa. Sasa ule mtazamo nilikuwa nao hadi kwenye ndoto hivyo nilivyoona amenilipia chakula nikajiulza huyu si ndo yule aligoma kulipa pesa yangu mpaka urafiki wetu ukafa? sasa iweje anilipie chakula?

Sikutaka mambo yawe mengi, nikachukua buku ten kwenye wallet nikamrudishia hela yake huyo jamaa maana sikupenda unafki wake. Akaanza kama kujichekesha hivi , ni nikaondoka zangu nikamwacha hapo.

Utafiti wa kisayansi
Basi nikaenda mahali siyo mbali sana na pale, nikakuta kuna watu wanafanya utafiti wa kisayansi. Utafiki wenyewe ulikuwa ni kuhusu namna mpya ya kukamua mafuta ya nazi kwa ajili ya kupikia. Walichokuwa wanakifanya ni; walikuwa wamejenga kitu kama tanki kuwa la mduara ambalo lilikuwa linatumia kanuzi fulani za phyisics ambapo ukirusha nazi kwenye huo ukuta kwa hilo tanki, hiyo nazi itaanza kuzungukakwa kasi kubwa sana kuzunguka huo ukuta na kwa njia hiyo mafuta yalikuwa yanakamuliwa kutoka kwenye nazi.

Mkuu wa ule utafiti alisema kama mambo yatakuwa sawa kwenye utafiti huo yatatokea mapinduzi makubwa sana, kwa sababu kwanza; alisema kwa kukamua nazi kwa njia ya kawaida huwa tunapata mafuta aslimia 30 tu ya mafuta kutoka kwenye nazi, lakini njia hii itafanya tupate asilimia 100 ya mafuta kutoka kweye nazi. Pili, kitendo cha nazi kuzunguka kufuata ule ukuta wa tank kinazalisha umeme mwingi, hivyo mchakato wa ukamuaji mafuta utakuwa chanzo cha nishati pia.

Basi nikavutiwa na hiyo idea, nikatania nikisema kuwa kama utafiti utafanikiwa bei ya nazi itakuwa juu sana. Nikaendeelea kwa kusema kuwa, msanii anaweza kwenda studio kurekodi, producer akimuuliza unanipa sh. ngapi ili tufanye huu wimbo, msanii angeweza kusema 'nitakupa nazi tatu', watu wakacheka sana...

Onyesho la stand-up comedy
Tukiwa tunaendelea na shunghuli za utafiti pale, alikuja msanii moja wa stand-up comedy ambaye sitopenda kumtaja jina. Alikuja kasema kuwa alikuwa na onyesho ya stand up comedy kwa wanafunzi wa chuo cha CBE lakini mtu aliyekuwa afanye naye onyesho amepata dharula hivyo alikuwa anamuomba jamaa ambaye ndo alikuwa mkuu wa ule utafiti wa kisayansi akamsaidie. Yule jamaa akasema yuko busy, ila akasema naweza kwenda mimi maana anaona kama ninaweza kwa ku-refer ule utani wangu kuhusu nazi. Basi yule msanii akakubali, tukaondoka kwenye huko ukumbini ambapo pangefanyika hilo nyesho.

Tulipofika ukumbini kulikuwa hakuna watu, kwa hiyo akasema ngoja aende akawaambie watu waanze kuingia ukumbini. Sasa nikiwa pale ndani nikapata changamoto mbili; Kwanza, koo kuuma sana kiasi kwamba nikawa naongea kwa tabu. hali hii huwa ikinipata kwenye maisha ya kawaida huwa naamua kujizuia kuongea sana, maana nikiongea sana sauti huwa inapotea kabisa. Pili; nilisahau material ya jokes zote ambayo ningeweza kuperfom. Jamaa aliporudi, nikamwambia kuwa mi nimepata changamoto ya koo kuuma sana, ila nitaperfom hivyo hivyo sema tu sitotumia nguvu kubwa katika kuongea, akasema haina shida.

Watu wanaanza kuingia ukumbini mimi sikumbuki kitu, najaribu kuvuta kumbukumbu lakini wapi. Ikabidi nitoke nje nikae sehemu mwenyewe sehemu yenye utulivu labda niweze kukumbuka. Sasa nikiwa nimekaa sehemu ya peke yangu najaribu kuvuta kumbukumbu hata jokes kadhaa, kuna mama ana mtoto mdogo akaja nilipokaa, yule mtoto akaanza kunisumbua kiasi akanipotezea concetration kabisa.

Muda wa pefomance ukafika, yule msanii akaja kuniita kuwa niwe tayari maana show ni karibu inaanza. Lakini this time alikuja na watu wengine ambao hawa watu katika maisha ya kawaida nilisoma nao chuo. sasa kuna mmoja wao aliponiona na kujua kuwa jamaa alikuwa amenikaribisha niperfom pale, akaanza kummaindi yule msanii na kumwambia anitoe haraka sana kwenye ratiba. Wenzake wakawa wanamwambia avunge lakini jamaa akazidi kuwa mkali akidai kuwa huyo msanii amefanya jambo la kijinga sana kuniweka mimi niperfom hapo.

Hili jambo lilishanganza maana huyo jamaa chuoni alikuwa ni mshkaji na nilimsaidia kwenye mambo mengi sana ila nikasema fresh tu, haina noma. Tukaingia ukumbini nikaenda nikakaa sehemu, pembeni yangu alikaa mwanamke wa kizungu. Akaanza kuniongelesha kwa lugha ya kabila letu. Nikawa nashangaa huyu mtu amejuaje kuwa mimi ni mtu wa kabila hilo, ila nikawa namjibu. MC akaanza kusherehesha, muda huo mimi sikumuki joke hata moja, najiuliza nikiitwa kwenda jukwaani nitafanya nini. wakati nikiendelea na tafakari, nikaamka...​
 
Back
Top Bottom