URAFIKI WA KINAFKI, UTAFITI WA KISAYASI NA ONYESHO LA STAND-UP COMEDY (CHUKI NA UPENDO VINAPOONEKANA BILA KIFICHO)
Ndoto yangu ya leo ilikuwa ndefu sana na ina mambo mengi kweli, hivyo nitaikatisha kwa kuanzia mbele kidogo maana mwanzo wake nimeamka siukumbuki vizuri...
Urafiki wa kinafki
Ndoto yangu ilianzia somewhere ambapo nimesema sitosimulia kwa sababu sikumbuki vizuri, lakini baada ya kutoka huko, nilienda mitaa jirani na stand ya daladala ya makumbusho kwenda kupata chakula. Kuna chakula fulani nilikuwa nakitaka, nilipoulizia nikaambiwa ni sh 30000, na mimi kwenye wallet nilikuwa na hiyo hiyo 30000. Kwa hiyo nikamuambia mhudumu anipatie chakula chochote cha bei ya chini.
Basi akaniletea chakula flani hivi kama ubwabwa, kama biriani vile, yaani hakieleweki, nikala fresh. Baada ya kumaliza nikamuuliza bei akasema ni elfu kumi. Basi ile nazama nitoe wallet, kuna rafiki yangu mmoja akanilipia hiyo hela. Nilishangaa kwa sababu hakuwepo pale. Pia huyu rafiki yangu kwenye maisha ya kawaida urafiki ulishakufa sababu ya pesa. Sasa ule mtazamo nilikuwa nao hadi kwenye ndoto hivyo nilivyoona amenilipia chakula nikajiulza huyu si ndo yule aligoma kulipa pesa yangu mpaka urafiki wetu ukafa? sasa iweje anilipie chakula?
Sikutaka mambo yawe mengi, nikachukua buku ten kwenye wallet nikamrudishia hela yake huyo jamaa maana sikupenda unafki wake. Akaanza kama kujichekesha hivi , ni nikaondoka zangu nikamwacha hapo.
Utafiti wa kisayansi
Basi nikaenda mahali siyo mbali sana na pale, nikakuta kuna watu wanafanya utafiti wa kisayansi. Utafiki wenyewe ulikuwa ni kuhusu namna mpya ya kukamua mafuta ya nazi kwa ajili ya kupikia. Walichokuwa wanakifanya ni; walikuwa wamejenga kitu kama tanki kuwa la mduara ambalo lilikuwa linatumia kanuzi fulani za phyisics ambapo ukirusha nazi kwenye huo ukuta kwa hilo tanki, hiyo nazi itaanza kuzungukakwa kasi kubwa sana kuzunguka huo ukuta na kwa njia hiyo mafuta yalikuwa yanakamuliwa kutoka kwenye nazi.
Mkuu wa ule utafiti alisema kama mambo yatakuwa sawa kwenye utafiti huo yatatokea mapinduzi makubwa sana, kwa sababu kwanza; alisema kwa kukamua nazi kwa njia ya kawaida huwa tunapata mafuta aslimia 30 tu ya mafuta kutoka kwenye nazi, lakini njia hii itafanya tupate asilimia 100 ya mafuta kutoka kweye nazi. Pili, kitendo cha nazi kuzunguka kufuata ule ukuta wa tank kinazalisha umeme mwingi, hivyo mchakato wa ukamuaji mafuta utakuwa chanzo cha nishati pia.
Basi nikavutiwa na hiyo idea, nikatania nikisema kuwa kama utafiti utafanikiwa bei ya nazi itakuwa juu sana. Nikaendeelea kwa kusema kuwa, msanii anaweza kwenda studio kurekodi, producer akimuuliza unanipa sh. ngapi ili tufanye huu wimbo, msanii angeweza kusema 'nitakupa nazi tatu', watu wakacheka sana...
Onyesho la stand-up comedy
Tukiwa tunaendelea na shunghuli za utafiti pale, alikuja msanii moja wa stand-up comedy ambaye sitopenda kumtaja jina. Alikuja kasema kuwa alikuwa na onyesho ya stand up comedy kwa wanafunzi wa chuo cha CBE lakini mtu aliyekuwa afanye naye onyesho amepata dharula hivyo alikuwa anamuomba jamaa ambaye ndo alikuwa mkuu wa ule utafiti wa kisayansi akamsaidie. Yule jamaa akasema yuko busy, ila akasema naweza kwenda mimi maana anaona kama ninaweza kwa ku-refer ule utani wangu kuhusu nazi. Basi yule msanii akakubali, tukaondoka kwenye huko ukumbini ambapo pangefanyika hilo nyesho.
Tulipofika ukumbini kulikuwa hakuna watu, kwa hiyo akasema ngoja aende akawaambie watu waanze kuingia ukumbini. Sasa nikiwa pale ndani nikapata changamoto mbili; Kwanza, koo kuuma sana kiasi kwamba nikawa naongea kwa tabu. hali hii huwa ikinipata kwenye maisha ya kawaida huwa naamua kujizuia kuongea sana, maana nikiongea sana sauti huwa inapotea kabisa. Pili; nilisahau material ya jokes zote ambayo ningeweza kuperfom. Jamaa aliporudi, nikamwambia kuwa mi nimepata changamoto ya koo kuuma sana, ila nitaperfom hivyo hivyo sema tu sitotumia nguvu kubwa katika kuongea, akasema haina shida.
Watu wanaanza kuingia ukumbini mimi sikumbuki kitu, najaribu kuvuta kumbukumbu lakini wapi. Ikabidi nitoke nje nikae sehemu mwenyewe sehemu yenye utulivu labda niweze kukumbuka. Sasa nikiwa nimekaa sehemu ya peke yangu najaribu kuvuta kumbukumbu hata jokes kadhaa, kuna mama ana mtoto mdogo akaja nilipokaa, yule mtoto akaanza kunisumbua kiasi akanipotezea concetration kabisa.
Muda wa pefomance ukafika, yule msanii akaja kuniita kuwa niwe tayari maana show ni karibu inaanza. Lakini this time alikuja na watu wengine ambao hawa watu katika maisha ya kawaida nilisoma nao chuo. sasa kuna mmoja wao aliponiona na kujua kuwa jamaa alikuwa amenikaribisha niperfom pale, akaanza kummaindi yule msanii na kumwambia anitoe haraka sana kwenye ratiba. Wenzake wakawa wanamwambia avunge lakini jamaa akazidi kuwa mkali akidai kuwa huyo msanii amefanya jambo la kijinga sana kuniweka mimi niperfom hapo.
Hili jambo lilishanganza maana huyo jamaa chuoni alikuwa ni mshkaji na nilimsaidia kwenye mambo mengi sana ila nikasema fresh tu, haina noma. Tukaingia ukumbini nikaenda nikakaa sehemu, pembeni yangu alikaa mwanamke wa kizungu. Akaanza kuniongelesha kwa lugha ya kabila letu. Nikawa nashangaa huyu mtu amejuaje kuwa mimi ni mtu wa kabila hilo, ila nikawa namjibu. MC akaanza kusherehesha, muda huo mimi sikumuki joke hata moja, najiuliza nikiitwa kwenda jukwaani nitafanya nini. wakati nikiendelea na tafakari, nikaamka...