Taliban yaja na sheria kali zaidi dhidi ya wanawake Afghanistan, jumuiya ya kimataifa yalaani vikali

Yoda

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2018
Posts
48,475
Reaction score
70,102
Utawala wa Taliban nchini Afghanistan umeendeleza mkandamizo mkali kwa wanawake wa nchi hiyo kwa kupitisha sheria kali za maadili zinazotaka wanawake kuficha kabisa gubigubi nyuso zao na miili yao wanapokuwa nje ya nyumba zao pamoja na kupiga marufuku wanawake kuongea mbele ya hadhira/umma.

Taliban wanasema sheria hizi ni kwa ajili ya kuzuia na kudhibiti vitendo vya tamaa na vishawishwi vibaya katika jamii ya nchi hiyo. Hata hivyo wanaharakati na viongozi sehemu mbalimbali duniani wamelaani vikali sheria hizo mpya za Taliban zitakazoanza kutumika mwezi huu.

 
Kuingia mbinguni itakuwa ni kwa neema tu na sheria za kipumbavu kama hizo hazimuingizi mtu mbinguni. Taliban ni takataka kabisa.

Wanawake wameumbwa watupendezeshe machoni wanaume halafu walevi wengine wanataka kutunyima huo uhondo wakati ni halali yetu. Bure kabisa.
 
Hao Taliban walivyo na sheria kali alafu atokee kenge eti amtamani mwanamke asie wake anaanzaje kwa mfano! mungu mwenyewe hajaweka hizo sheria wanazoweka wao alafu sijawahi sikia wanaume nao wamewekewa sheria
Wanachokifanya Taliban ni sahihi kabisa kulingana na mafunzo ya dini sahihi ya kiislamu na ndivyo ilivyokuwa wa wakati wa mtume na watawala wa mwanzo walioongoza Dola ya kiislamu baada ya kufa mtume.
 
 
Kwahiyo hawaruhusiwi kuongea mbele ya watu, wanafanyaje shughuli zao za kila siku kama kwenda sokoni. Wanaume wanapataje wake wa kuoa, sababu hawawaoni wanawake, hawaruhusiwi kuongea nao.

Mbwa, Ngombe , Kuku, Mbuzi wana haki huko zaidi ya wanawake.
 
Kwahiyo hawaruhusiwi kuongea mbele ya watu, wanafanyaje shughuli zao za kila siku kama kwenda sokoni. Wanaume wanapataje wake wa kuoa, sababu hawawaoni wanawake, hawaruhusiwi kuongea nao.

Mbwa, Ngombe , Kuku, Mbuzi wana haki huko zaidi ya wanawake.
Elewa mbele ya umma au public na sio one to one
 
Dini ya kiislamu haikuanzishwa ni wanaharakati wala vyombo vya habari wala nchi za magharibi, dini ya kiislamu imetoka kwa Mwenyezi Mungu mwenyewe aliyetuumba na miongozo yake ipo katika Quran na simulizi za Rasulu S.A.W, Taliban wanafuata miongozo ya Quran kumlinda mwanamke na vishawishi mbali mbali ambavyo mwenyewe mwanamke atakuwa na thamani zaidi kuliko wanawake wengi ambao huji-expose miili yao na kukaa uchi na kusababisha madhara mbali mbali duniani, kama kuenea kwa maradhi na magonjwa ya zinaa kama ukahaba na umalaya. Mwanamke mwili wake wote unatakiwa uwe kwenye stara. mila za wazungu waachiwe wenyewe wao hawana dini.

Haki za mwanamke zipo wazi katika uislamu tokea dini ya kiislam, Wale wasio na dini ndio hueka makongamano na kutunga haki za mwanamke upya kila wanapoona katika maslahi yao binafsi wanayotaka wao, Waislamu hawana haja kwenda Beijing kupata haki za Mwanamke Quran na khadithi za Rasulu S.A.W inatosha.

Sio kila uhuru utamnufaisha mwanadamu kwa maisha ya baadae. Uhuru una mipaka yake kwa kila mtu
 
Hizo sheria za kishetani, ni sawa na kusema wanawake hawakustahili kuwepo Duniani. Yaani badala ya kuwadhibiti wanaume wenye tamaa mbaya, wanaenda kuwatesa wanawake!! Halafu utawasikia eti ni maagizo ya dini!! Hiyo itakuwa dini ya wachawi?? Kwenye nchi za kishetani kama hizi, mtu akizaliwa mwanamke inakuea kama ni laana.

Siku ya saba, Mungu akasema, na tumwumbe mwanadamu. Kwa mfano wa Mungu, mwanaume na mwanamke akawaumba.

Enyi wana wa Mungu mnaomwabudu Mungu wa kweli zingatieni mafundisho ya Mungu yanayosema sote, wanaume na wanawake ni sawa mbele za Mungu.

Andiko jingine lasema:
Enyi wake watiini waume zenu, nanyi waume wapendeni wake zenu. Wanaume tumepewa jukumu zito sana kwa wanawake kwa maana upendo hukusanya mambo mengi sana. Ukimpenda mtu maana yake huwezi kumtesa, huwezi kumwekea sheria ngumu au za kumdhalilisha. Lakini pia kuwa tayari hata kufa kwaajili yake. Maana tunaambiwa tuwapende wake zetu kama Yesu alivyolipenda Kanisa.
 
Niwacheni nakuka darsa la wasiooneka kutoka kwa Arsis. Unamjuwa Arsis wewe? Njoo muulize kuhusu Taliban, huku:

 
Kwahiyo mwanamke kuvaa kwa stara ndio kumtesa,mbona makanisani hawaendi na chupi huko?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…