Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 48,475
- 70,102
Utawala wa Taliban nchini Afghanistan umeendeleza mkandamizo mkali kwa wanawake wa nchi hiyo kwa kupitisha sheria kali za maadili zinazotaka wanawake kuficha kabisa gubigubi nyuso zao na miili yao wanapokuwa nje ya nyumba zao pamoja na kupiga marufuku wanawake kuongea mbele ya hadhira/umma.
Taliban wanasema sheria hizi ni kwa ajili ya kuzuia na kudhibiti vitendo vya tamaa na vishawishwi vibaya katika jamii ya nchi hiyo. Hata hivyo wanaharakati na viongozi sehemu mbalimbali duniani wamelaani vikali sheria hizo mpya za Taliban zitakazoanza kutumika mwezi huu.