Sam Gidori
Senior Member
- Sep 7, 2020
- 165
- 417
Wanagambo wa Taliban wametishia kuyachukulia hatua mataifa ya Marekani na Uingereza ikiwa watashindwa kuondoa wanajeshi wao kufikia Agosti 31 mwaka huu.
Kauli ya Taliban inakuja siku moja baada ya Rais Joe Biden kusema kuwa kuna uwezekano wa kuongeza muda wa wanajeshi wao kuendelea kukaa nchini Afghanistan, wakati Waziri wa Ulinzi wa Uingereza, Ben Wallace akisema shughuli ya kuwaondoa wanajeshi wa Uingereza inaweza kukamilika ndani ya saa, sio wiki.
Msemaji wa Taliban, Dkt. Suhail Shaheen amesema kundi hilo halitakubaliana na hatua ya mataifa hayo kuongeza muda wa wanajeshi wao kukaa nchini humo, na kuahidi kuchukua hatua kali ikiwa wanajeshi wataendelea kubaki nchini humo.
Awali, Rais Biden alionya kuwa shughuli ya kuwatoa Wamarekani wote nchini Afghanistan inaweza kuwa ndefu na ya kuumiza.
“Haitawezekana kuwatoa maelfu ya watu nchini Afghanistan bila kushuhudia maumivu na kuwapoteza watu na picha tunazoziona kwenye televisheni,” Rais Biden alisema, akiongeza kuwa zaidi ya watu 11,000 wameondolewa nchini Afghanistan ndani ya saa 36, na kufanya jumla ya watu walioondolewa nchini humo kufikia 33,000 siku ya Jumapili.
Zaidi ya watu 20,000 wanasubiri kutolewa kutoka uwanja wa ndege wa Kabul. Uingereza inataka kuongeza idadi ya watu wanaotolewa nchini Afghanistan kufikia 12,000, lakini Waziri Mkuu wa Uingereza, Borris Johnson amesema kufanikiwa kwa hatua hiyo kunategemea wanajeshi wa Marekani kuendelea kudhibiti Uwanja wa Ndege.
Zaidi ya watu 20 wameripotiwa kufariki nje ya Uwanja wa Ndege wa Kabul, wengine wakitajwa kufariki kwa kukanyagana, kwa mujibu wa Shirika la Habari la Reuters. Waziri Mkuu wa Uingereza anatarajiwa kufanya mkutano na Rais Biden hapo kesho kumshawishi kuendelea kuwabakisha wanajeshi wa Marekani nchini humo. Onyo la Taliban ni pigo kubwa kwa mataifa hayo ambayo yanajitahidi kupata muda zaidi kufanikisha kuwaondoa wananchi wao nchini humo.
Taliban, kwa upande wao, wamesema wananchi wa Afghanistan hawakimbii nchi yao kutokana na wasiwasi, bali kutokana na sababu za kiuchumi.
Msemaji wa Taliban, Dkt. Shaheen ameongeza kuwa taarifa zinazosambaa za kufungwa kwa shule za wasichana si za kweli, akisisitiza kuwa wanawake nchini humo wana haki sawa kama hali ilivyo kwenye nchi za Magharibi, “lakini tu wakiwa na hijabu.”
Chanzo: Daily Mail
Wanajeshi wa Uturuki wakitoa maji kwa Waafghanistan wanaosubiri kuondolewa kutoka Uwanja wa Ndege wa Hamid Karzai mjini Kabul [Picha: AA]