Kwahiyo una mshitakia au unamaanisha nini maana Adam alikua ni binadam kama wewe hayupo kwenye kundi la akina Musa, Elia n.k?
Lipo andiko la biblia pia linazungumzia jinsi Mungu alivyo mletea wanyama Adam ili aishi nao.
Mwanzo 2:18–23
18. Bwana Mungu alisema kwamba si vizuri mtu awe peke yake; angemfanyia msaidizi anayemfaa.
19. Mungu akawaumba wanyama wa nchi na ndege, akawaleta kwa Adamu aone atawaitaje; jina alilotoa Adamu likawa jina lao.
20. Adamu akawapa majina wanyama wote, ndege na wanyama wa mwituni; lakini hakupatikana msaidizi aliyemfaa.
21. Mungu akamletea Adamu usingizi mzito, akatwaa sehemu ya ubavu wake na kuifunga mahali pake.
22. Kutokana na sehemu hiyo, Mungu akamfanya mwanamke na kumleta kwa Adamu.
23. Adamu akasema: “Huyu sasa ni mfupa katika mifupa yangu, na nyama katika nyama yangu.”