Tamaduni Music tatizo lao ni nini?

hivi HIPHOP ni kuvuta Bangi...!!?? ni moja ya misingi??
 
Kama wanataka kuendana na soko la mziki wa sasa...inabidi wabadilike, wasiache uandishi wao ila waboreshe midundo(beats), videos na waache ujuaji wa kijinga.
Mimi Tamaduni huwa wananishangaza sana, wakiwa Facebook wanawaponda sana watangazaji hasa wa clouds na east Africa, halafu bila aibu wanawaomba intavyuu, juzi FNL nimemuona One akiuza nyago, kama wanataka wapate airtime ni lazima wawe karibu Na watangazaji/DJs, maana usitegemee kupata airtime wakati ukiwa fb unawaita 'machoko', mfano huyu nash mc anatabia hiyo sana, wakiendelea Na ujuaji wataendelea kusugua bench sana
 
Kwani mtu akikosea ukimchana ndo hutakiwi kuingea nae?...cha msingi umewaambia ukweli media ndo uti wa mgongo wa shughuli zao Mzee me nawapongeza kwa kuwa na uthubutu wa kuwasema haswa wanapozingua na hiyo ndo hip-hop...no beef wanawaelekeza wanapoteleza japo maneno wanayotumia ni makali.
 
Nash Mc, VitasaMoto, Mjahidina, Misimamo mikali, NashKazini.. Huyu huwa Hajipendekezi kwa MTU..

Anasonga Kivyake
 
Acha kunichekesha nduguyangu, hiphop tumeiga kwa wamarekani halafu unazungumzia identity Ndaxy EMI
 

Dawa ya kidonda lazma iwe dawa kali ili kidonda kiweze kupona mkuu.

Kisipopona basi ujue kimeshaoza hamna jinsi lazma mguu ukatwe.
 
kwa style hiyo wataendelea kusubiri sana, kama wanazingua njia sahihi ya kuwarekebisha ni kuwafata wenyewe kuwaeleza au hata kuwapigia simu, na sio kutafuta sifa FB
 
kwa style hiyo wataendelea kusubiri sana, kama wanazingua njia sahihi ya kuwarekebisha ni kuwafata wenyewe kuwaeleza au hata kuwapigia simu, na sio kutafuta sifa FB
Unafki/uoga siyo hip-hop... Hayo matatizo jamaa wanayowasema east africa na cloudz ni kweli yapo bt wasanii woooote walikosa Wa "KUMFUNGA PAKA KENGELE" kapatikana wa kumfunga paka kengele mna diss duuuuuh...me ni muumini wa ukweli na sipendi unafki nafurah namna jamaa wanavyowachana na bado kwenye intavyuu wanakwenda maisha yanaendelea thats hip-hop.
 
Tamaduni its about reality,wanaimba wanachoamini wanaweza na kupenda,kwani baadhi ya mcs wameacha asiki zao ili wahit,hawa madogo hilo wamekataa,uzuri ni kwamba wanaishi kama family na kushirikiana kwa karibu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…