Tamasha la Sikukuu ya Mwaka mpya wa jadi wa China ni tafrija kubwa kwa wachina nyumbani na nje ya nchi. Ni alama muhimu kabisa ya kujumuika kwa familia na marafiki.
Tamasha hili huleta kumbukumbu nyingi kwa wachina wote, nyumbani na nje ya nchi. Likiwa na maonyesho kama ngonjera, mchoro mfupi, kungfu, kuimba na kucheza, na kuwafanya watu kukumbuka furaha na wakati muhimu zaidi katika mwaka unaopita, na kutarajia bahati na kila la heri kwa mwaka unaofuata. Tamasha hili limekuwa ni sehemu ya lazima ya sikukuu ya jadi ya mwaka mpya, na kuwafanya ndugu na marafiki kukaa pamoja kulifuatilia kwenye televisheni, mitandao ya kijamii na simu za mkononi.
Mwaka wa 2021 ni Mwaka wa Ng'ombe kwa mujibu nyota za kichina. Katika utamaduni wa Wachina, ng'ombe huwakilisha wachapakazi, wenye akili na watu wanaoaminika.
Fuatilia kikamilifu kwenye mtandao wa internet Tamasha la Sikukuu ya Mwaka mpya wa jadi wa Ng’ombe la CGTN kwa njia ya mtandao, na ujifunze juu ya maazimio ya mwaka mpya na matarajio waliyonayo wachina kwa mwaka mpya.