Kuanzia tarehe 15 hadi 17 mwezi Juni, tamasha la 18 la utamaduni na utalii wa Qici ambalo pia ni tamasha la kwanza la utamaduni na sanaa za Qiuci mjini Kuqa, China lilifunguliwa. Shughuli mbalimbali za kitamaduni kama vile maonyesho ya fataki, maonyesho ya urithi wa utamaduni usio wa mali duniani, na uimbaji wa opera ziliwavutia watalii wengi.