Tamasha la Wasafi ''Wasafi Festival" jijini Dar es Salaam

Tamasha la Wasafi ''Wasafi Festival" jijini Dar es Salaam

Mondi...namkubali sana huyu jamaa ingawa nyimbo zake zmejaa upupu
Namkubali ni hustler

Ila kiba naskia show zake anazifanyia ghetto hapendi kujitangaza
Kiba anahusika na nini apa au ni genye tu kwake?
 
Nilikuwa na wasiwasi na mvua lkn nimegundua kila mtu na Starehe yake
,sasa hii ni saa 10 jioni hivi je baadaye.
 
Talent is not enough (kipaji pekee hakitoshi), hiki kitabu ni lazima kila msanii akisome...Diamond angekua anategemea tu kipaji asingekua hapa na hata yule hasimu wake anategemea kipaji kwa sana aliwika hapo nyuma kwa kutegemea bifu na Diamond ili nae azungumziwe (ukiwa karibu na waridi nawe utanukia), Kwa sasa Kiba hata hatoi ngoma kwasababu diamond hana time nae tena, kila kiki ya kipuuzi ya kukoleza bifu Diamond anaichomoa matokeo yake ni muda mrefu sasa kiba wanaogopa kutoa ngoma.

Diamond anaimba kawaida tu ila sasa ana brand kubwa mno, wenzake washamba washamba wamekomalia kujisifia hawapendi show off wanaishi maisha ya kawaida na huku ndio kunawafanya wasiendelee. Mohamed dewji hahitaji kupiga pamba Kali na ma bling bling kwasababu hayamuuongezei thamani kwenye biashara zake za mikonge ila msanii ni muhimu sana unyuke pamba za maana, uwe na dem mkali, uwe na gari Kali , uvae meno ya gold, kuanzisha vitu ambavyo watanzania hatujazoea kama kulindwa na mabodigadi wengi, n.k maana hivi ndivyo vinakomaza brand yako huchokwi kuzungumziwa na ndio maana makampuni kila kukicha yanagombania kufanyiwa matangazo na Diamond kwa mamilioni,

kiba na wenzake wanaoishi maisha ya kawaida hata mtu akitaka kufanya nao tangazo kwa haraka haraka anawaona ni watu wa kawaida tu hivyo wanaweza kuwapangia bajeti ya milioni 1 tu wafanyiwe tangazo na zaidi ya hapa wanajihisi wanapigwa.

Ila inapokuja swala la kufanyiwa tangazo na baba lao ukifikiria tu jamaa ana magari ya pesa ndefu kama V8 na BMW, nyumba Kali, Dem mkali anaehitaji matunzo ya kistaa, Nguo za gharama, sherehe za gharama, n.k kwa haraka haraka tu kama huna milioni 100 hata huwezi kufikiria kumpigia simu akufanyie tangazo.
ahahaha
 
Group la WhatsApp members 500?
Si huwa wanaishia 257?
 
Back
Top Bottom