Tambua: Matokeo yanaweza kuonyesha negative, lakini mtu akawa na HIV na kuambukiza zaidi kuliko mgonjwa wa zamani

Tambua: Matokeo yanaweza kuonyesha negative, lakini mtu akawa na HIV na kuambukiza zaidi kuliko mgonjwa wa zamani

TensorFlow

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2020
Posts
993
Reaction score
1,286
Nimeona mara kadhaa watu wakijiona wapo salama kufanya ngono bila kinga kwa sababu tu wamepima na matokeo kuonyesha negative. Hiyo sio sawa, kwa sababu vipimo vya juu kabisa kwa ujumla vita-detect HIV angalau week 4 baada ya maambukizi.

Vipimo vitaonyesha matokeo sahihi kwa watu walio wengi kuanzia wiki ya 4 mpaka ya 12, wengine itachukua mwaka mzima na hata miaka 2, Kipindi cha tangu mtu kufanya kitendo kinachomweka katika hatari ya kuambukizwa HIV mpaka pale atakapopata majibu sahihi ya afya yake huitwa window period.

Wakati huo wote, ikiwa mtu ana virusi naye huambukiza lakini vipimo haviwezi kuonyesha.

Mbaya zaidi, matokeo ya research ya hivi karibuni yanaonyesha kuwa mtu aliyeambukizwa karibuni ana uwezo wa kuambukiza zaidi kuliko mgonjwa wa siku nyingi.
 
Wacha kututisha bro, Tutaendelea Kuwagonga Kisawasawa Madada mpaka tufanane na Papuchi! Huo HIV sijui Ukimwi utajuana nao wewe na hao munaojiita Madaktari.
 
TensorFlow, Mkuu punguza uongo. Mtu mwenye virusi vya UKIMWI huchukua kati ya wiki 4 hadi sita kupata majibu sahihi ya uambukizo. Kuna baadhi wanakosa kipindi hicho na window period huweza kufika wiki 12 hadi 24 ambayo ni miezi sita na ni maximum. Hawa ni wachache sana, a micron of people. Kusema kuna watu huchukua window period ya miaka miwili ni a HELL NO.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu punguza uongo. Mtu mwenye virusi vya UKIMWI huchukua kati ya wiki 4 hadi sita kupata majibu sahihi ya uambukizo. Kuna baadhi wanakosa kipindi hicho na window period huweza kufika wiki 12 hadi 24 ambayo ni miezi sita na ni maximum. Hawa ni wachache sana, a micron of people. Kusema kuna watu huchukua window period ya miaka miwili ni a HELL NO.

Sent using Jamii Forums mobile app

Mimi sio mwongo, kuna cases ambazo huchukua muda mrefu kuliko kawaida, lakini sio nyingi. Niliweka link yenye scientific report inayotokana na research lakini naona imeondolewa na moderators, sitaki kujisumbua kuiweka tena. Ni sawa na cases za baadhi ya watu kutokuwa na uwezekano wa kuambukizwa ukimwi.
 
Back
Top Bottom