Tambua sifa za mwanaume asiye na mvuto wa kimapenzi kwa mwanamke

Infinite_Kiumeni

JF-Expert Member
Joined
Jan 23, 2023
Posts
382
Reaction score
687
Wanaume wenye tabia/ aina hii hupata shida kwenye mapenzi. Wanaishia kuona wanawake ni wagumu/ hawaeleweki. Wanatumia muda mwingi kutaka kumridhisha mwanamke. Au atatumia mali kuficha udhaifu wake.

Wanaamini akipata kitu fulani basi hatopata shida tena na wanawake. Anaweza pata mahusiano lakini akakosa usingizi. Wanaume wa hivyo ni wadhaifu kwa wanawake. Angalia sifa hizi uzijue na uziepuke ili uwe jasiri mbele ya mwanamke.

Asiyejiamini
  • Asiyejiamini sio jasiri. Hathaminiki mbele ya wanaomzunguka. Anapelekeshwa na maoni ya kila mtu. Anaona yake hayafai. Na mwanamke anajua kumpelekesha kweli mtu asiyejiamini. Atamtumia kwa anachokitaka atamuacha na maumivu. Jijengee ujasiri kwenye maoni yako, kwenye mawazo yako. Kwenye matendo yako, bila kujali wengine watasemaje. Lakini kuwa makini usivunje mipaka ya wenzio, au haki zao.
Mwanaume anayetaka kulelewa
  • Mwanaume anayelelewa ni ngumu kumvutia mwanamke. Hana uthamani. Hana nguvu ya kujitegemea. Anamtegemea mwanamke ndo awe mstari wa mbele kwenye mahusiano. Mwanamke atajiuliza, mwanaume anayelelewa atawezaje kuilea familia? Na ataondoka kutafuta mtu anayejitegemea. Hivyo, tuhakikishe tunajiinua kiuchumi na kiakili pia.
Anayepelekeshwa na mwanamke
  • Mtu anaweza kuwa anajiamini akiwa na wanaume wenzake lakini akikaa tu mwanamke, anakua mnyonge. Anataka kumfurahisha mwanamke kila muda. Anaogopa kumkosea. Mwanamke atamjaribu sana kuhakikisha kweli anaweza kumpelekesha. Ndo apo unakuta watu wanasema amewekwa kiganjani na mwanamke. Lakini ni kwa sababu mwanaume anashindwa kusimamia misimamo yake. Pengine kapenda mpaka ubongo haufanyi kazi. Na anaogopa kumpoteza mwanamke. Mwanamke anayejua unaogopa kumpoteza atakutesa.
Sio mtu mwenye mtazamo wa kuweza
  • Yaani asiye na mtazamo chanya. Anapinga vitu, au anaona kila kitu ndo mwisho wa dunia. Maana yake ni dhaifu. Waachie wanawake wajisikie hivyo. Kama mwanaume ni muhimu kuamini na kuwa na mtazamo chanya. Kwamba inawezekana, mambo yatakua sawa au yatapita tu. Kuna muda wanawake wanahitaji sana kuwa na mtu atakaye waongoza kwenye wakati mgumu, kuliko kuwa na mtu atayefanya mambo yawe magumu zaidi. Kuliko kulalamikia kila kitu. Hata ukipata mwanamke, utapata mlalamishi mwenzio ambaye itakua ngumu kufanya maendeleo pamoja.
Asiye na maamuzi
  • Kutokana na kutojiamini
  • Kutokana na kutokuwa kiongozi
  • Kutokana na kukosa uzoefu
  • Kwa mwanamke mwanaume aliyefanya maamuzi alafu akakosea ni bora kuliko yule asiyefanya maamuzi kabisa
Kuwa na maamuzi, kuwa kiongozi wake. Hata kwenye jambo dogo kama la leo tupike nini, usiache mwanamke akabaki kujiuliza kama amekosea kuamua au la.

Asiyestahimili misukosuko
  • Kama muvi zinavoonesha, janga likitokea mwanamke ndio anamficha mwanamke ila kwenye maisha, ukitegemea mwanamke ndo akukinge kwenye misukosuko atakuacha. Yeye anategemea we ndo uwe muhimili wake. Anategemea uwe mpole hata kwenye majanga makubwa. Na sio umlilie.
Asiyemwelewa mwanamke
  • Mwanamke hataki kukufundisha jinsi ya kumvutia. Anategemea we uwe unajua hayo mambo. Anategemea utamwelewa ishara zake za chinichini na kumtimizia. Akiona humwelewi atajifanya hakukutaka na ataenda kwa mwingine.
Ni muhimu ujue kumsoma mwanamke na ishara zake. Hata maneno yake kuna muda yanaficha ujumbe, muhimu ujue kuchambua.

Cha msingi ujifunze kwa kasi yako, kama mtu umejifunza jinsi ya kufanya unachokifanya ili ukifaidi kwanini usijifunze jinsi ya kuishi na mwanamke bila shida kwenye mapenzi? Kuishi na mwanamke kiakili kunajumuisha kujifunza kwa namna yoyote ile. Hakuna mtu anazaliwa anajua kila kitu, sote tunajifunza.

Ukimshayajua hayo ni rahisi kuishi kwa ujasiri wa kiume na mwanamke. Na unafanya maisha yenu yanakua rahisi kimapenzi.
 
Cha ajabu mtoa mada nae hadumu katika mahusiano.....
 
Hayana utaratibu...we fanya unavyo ona ni sawa akizingua ajikatae tu
 
Kusoma ni kawaida, tatizo kuelewa na kutenda, hapo ndio penye shida.
 
Back
Top Bottom