Tamida yasema ni sawa BOT kuweka akiba ya madini

Tamida yasema ni sawa BOT kuweka akiba ya madini

bagamoyo

JF-Expert Member
Joined
Jan 14, 2010
Posts
24,941
Reaction score
28,869
Kahama, Tanzania

TANZANITE NI RASILIMALI INAYOPATIKANA TANZANIA PEKEE, HIVYO TUWEZE KUONGEZA THAMANI
YAKE

View: https://m.youtube.com/watch?v=TAir66Cw5X8

Sekta ya madini tupo nyuma katika kuongeza thamani, kwani tukikata madini kama tazanite, almasi, Vito hadi watalii wakija Tanzania wanunue madini yaliyoongezewa thamani katika umbo la pete, vidani, hereni, bangili, vikuku, mikufu n.k ingeongeza mapato nchini juu ya utalii.

Kwa mfumo wa kuongeza thamani pia ajira nyingi zitaongezwa kama masonara, madalali, maonesho n.k

Hayo yamesemwa na mweyekiti wa wauza madini Tanzania ndugu Osman Abdulsattar Tharia, kuwa eneo la kuongeza madini / Vito thamani na ajira nchini ni fursa kubwa

Sababu nchi zingine kama UAE, Belgium, India, Thailand zinafaidika na mikakati ya kuongeza thamani madini, ujuzi wa kukata, masonara na masoko pia maonesho ambayo yamefunganishwa na kuvutia utalii katika nchi hizo.

Osman Abdulsattar amesema kutegemea kodi ya kuuza madini ghafi ambayo hayajaongezwa thamani ni kuendelea kupata mapato madogo sana kutokana na madini tuliyo nayo. Hivyo mikakati ya kuongeza thamani madini yetu iharakishwe ili nchi ifaidi mapato makubwa kutokana na madini yetu.
 
Dubai Gold Souk Matket Walking Tour | Dubai's Real Gold


View: https://m.youtube.com/watch?v=MEG5sa9Nu8s

Je hivi nchini Tanzania tuna super malls ambapo watalii wa nje na wananchi wanaweza kuingia kukuta bidhaa za madini zilizoja na kusheheni katika mtaa mrefu au mall kubwa kiasi mgeni akija atapelekwa kununua kitu cha kama zawadi au urembo na kuondoka nacho kuitangaza Tanzania ? Au Tunaishia kuuza vinyago vya Kimakonde vya mbingo na picha za kuchora za TingaTinga huku haturuhusu vijana kujifunza usonara, udalali, uchongaji wa madini huku nchi yetu ikipata jina nchi ya Utalii wa Wanyama, Pwani za Mchanga Mweupe, Vito na Madini vikivyochongwa kwa ustadi kukupa ukumbusho wa nchi hii ya kipekee Afrika !
 
SLOVAKIA YATOA RAI KWA WAFANYABIASHARA TANZANIA KUCHANGAMKIA FURSA ZA KIBIASHARA NA NCHI HIO

View: https://m.youtube.com/watch?v=3Vtc3agZNCs
Balozi wa Heshima wa Jamhuri ya Slovakia nchini Tanzania Mhe. Moustafa Khataw ametoa wito kwa wafanyabiashara wa Tanzania kuchangamkia fursa kwa kushirikiana na wenzao wa nchi hiyo ambao wameonesha nia ya dhati ya kutaka kuwekeza Pamoja kufanya biashara na Tanzania.

Mhe. Khataw ameyasema hayo katika mahojiano maalumu wakati wa kongamano la uwekezaji na biashara la Umoja wa Nchi za Ulaya lililofanyika kwa siku mbili katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam.

Mhe. Moustafa Khataw amesema Slovakia, iliyojipatia uhuru wake Januari 1, 1993 baada ya kuvunjika kwa amani umoja wake na Czechoslovakia, ni nchi iliyoendelea na yenye uchumi wa hali ya juu wa kipato, ikishika nafasi ya 45 katika Kielelezo cha Maendeleo ya Kibinadamu.


Mhe. Khatawa amesema jumla ya makampuni 18 toka nchi hiyo yamehudhuria kongamano hilo la biashara la EU lililofunguliwa siku ya Alhamisi na Makamu wa Rais Dkt Philip Mpango na kufungwa siku ya Ijumaa na Rais wa Zanzibar Dkt. Hussein Ali Mwinyi.

Pamoja na mambo mengine, Mhe. Moustafa Khataw amesema makampuni kadhaa yamedhamiria kuwekeza nchini Tanzania katika nyanja mbalimbali, ikiwemo ujenzi wa nyumba bora za bei nafuu na uzalishaji wa mbolea halisi.

Mhe. Moustafa Khataw ameongeza kuwa nchi ya Slovakia pia ni wazalishaji wakuu wa magari kwa kila mtu duniani, ambapo ilitengeneza jumla ya magari milioni 1.1 mwaka wa 2019, ikiwa ni asilimia 43 ya jumla ya pato lake la kiviwanda. “Kuvurugika kwa uchumi katika maeneo yao kutokana na mgogoro wa Urusi na Ukraine wenzetu hawa wa Slovakia wameamua kugeukia Afrika kuendeleza shughuli zao za biashara na uzalishaji na wamevutiwa mno na Tanzania kwa kuwa nchi ya amani na vivutio vyema vya uwekezaji”, alisema Mhe. Khataw.

source : michuzi
 
TANZANIA KUWA SOKO LA MADINI

John Wambura Bina ambaye ni Rais wa FEMATA atilia mkazo Tanzania kuwa soko la madini Afrika

View: https://m.youtube.com/watch?v=N1M-uGBjVZM

mchakato waanza kupitia FEMATA kwa sababu nchi imefunguka, na sekta ya madini inataka Tanzania kuwa kama Dubai kwenye soko la madini..

Naye mweyekiti wa wauza madini Tanzania ndugu Osman Abdulsattar Tharia amesema wazo hili la FEMATA ni zuri ili kuwafanya waTanzania wawe matajiri..

John Wambura Bina rais wa Rais wa FEMATA anasema Tanzania ina kila sifa za kila mtu kuwa tajiri ..
 
Back
Top Bottom