KERO TAMISEMI ajira za mkataba afya mlizotoa zimekuwa jipu

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Iko Hivi WB wametoa billion 600 kama Grants kusaidia afya ya mama na mtoto.

Tamisemi ikaajiri watumishi 300 kwa Mkataba was miaka mitatu majina walichukua kwenye database ya waliomba ajira mwezi was nne mwaka 2023 hivyo Kuitwa kazini ilikuwa mwaka huu January.

Tukalipoti kazini na kupanga vituo vya kazi .

Sasa changamoto iliyopo.

Mwezi was pili na wa tatu hakuna malipo tuliyopata kwenye mshahara.

Mwezi wa nne tukaambiwa na Halmashauri zetu kwamba hela imeingia tamisemi.

Sasa kinachotokea kwa sasa.

Walisema wanatulipa mishahara kuanzia wa pili ,tatu na nne hadi ninapoongea hii tunaambiwa hela iko kwa process tukiwauliza wakuu wa halmashauri zenu wanatupa majibu mepesi ya kuwa kuwa pesa imekuwama BOT.

Tukiuliza Tamisemi nao jibu ni hilo hilo.

Kinachotuuma tunashindwa kusaidiwa kama urgent ilhali tuna deal na afya za watanzania.
 
Na tuliaminishwa vibaya tangu tukiwa shule uhakika wa ajira ila mateso ni makubwa kuanzia diwani hadi mwananchi wa kawaida.
 
Kwanini msigome kwa siku kadhaa kuingia kazini ili kushinikiza mlipwe stahiki zenu.
Hamna platform yoyote inayowaunganisha nyote kwa pamoja au kwa wingi kama WhatsApp au telegram groups...??
 
Dah ni huzuni hela imekwama je?
 
Nitakuambia kitu nachojua kuhusu BOT
Kuanzia mwaka jana mwezi wa 8 walikuwa na uhaba mkubwa wa fedha zote za ndani na zakigeni hivyo walikuwa wagum kuprocess issue yyte ya Hela nakumbuka tulidai Hela BOT kuanzia mwezi wa 9 tukaja kulipwa mwezi wa 1 2024 kwhy ukiskia Hela zimepitia BOT ujue Kuna kazi ya ziada ya kufanya ili mpate Hela yenu na serikali haitosema chchte kwasababu walikuwa wanadaiwa kwnye miradi mikubwa kama SGR na bwawa la Morogoro so most of the money zilielekezwa huko nadhani kama Kuna mtumishi wa umma atakuwa na ushahidi juu ya hili OC zao wanaona wanavyozipata kwa shida
Kwhy walichowaambia ni sawa kabisa lakin kwa maslah mapan ya taifa siku zote Kuna kipaumbele taifa kwanza nd maan hamjalipwa. Kwhy komaeni make sure mnasurvive Hela yenu mtaipata tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…