Hao walimu wapya itabidi wawe wavumilivu, vinginevyo miongoni mwao wataikimbia ajira hiyo mapema kwa njaa ukichukulia wengine tayari walikuwa wana miradi iliyokuwa inawapa kipato mpaka wakaanzisha familia.Sasa kama kuna suala la uhakiki wa NECTA lipo mpaka hilo zoezi likamilike litachukua muda mrefu,na huu utakuwa ni usumbufu,iweje wawapangie vituo bila kujiridhisha wakati TAMISEMI na NECTA ni taasisi za serikali? TAMISEMI ilitakiwa kwanza ipate taarifa za NECTA kama taarifa za hao waajiriwa ni sahihi ndiyo wapangiwe halmashauri za kwenda kuripoti na pia mafungu ya fedha za kujikimu yapo wakati wakisubiri majina yaingizwe kwenye payroll.Barua ya ajira hufuata na hatimaye barua ya kuthibitishwa kazini kazini huja.Hao walimu wavumilie kuna taratibu za ajira zitachukua muda kukamilika