TAMISEMI fuatilieni Wakurugenzi wa Halmashauri zote kuhusu ajira mpya za Waalimu kuna urasimu mkubwa

Nimekumbuka mbali sanaa jinsi nilivyofanyiwa kwenye ajira yangu na serikali, barua ya kazi na kupangiwa kituo nimepewa, nimeacha kazi yangu nimeripoti kituoni nimekaa mwezi kwenye kituo cha kazi baadae naambiwa ajira zetu zimefutwa hili sitalisahau na Mungu ni Mwema kila wakati
Pole sana mkuu
 
Bila kukomaa hiyo hela ya kujikimu hamtaipata na mbaya zaidi mmeingia shule zimefungwa mitihani mmeshasahihisha na kupanga matokeo sasa hakuna effect kwa idara ya elimu hata mkigoma.
Mimi nakumbuka tulipata post wakati masomo yanaendelea na kukuta hali ni mbaya hakuna waalim wa sayansi. Yaaan tukakinukusha tulipewa hela fasta za kujikimu halmashauri yetu ila mshahara ulichelewa mwezi mmoja.
Ila tulisain 716,000 mshahara wa degree ila awamu hiibwa degree wamesaini 756,000.
Sijaelewa hapo inakuwaje mbona magepu hayaaa
756,000?Au labda posho ya kujikimu mkuu

Nijuavyo basic ni ile ile haijabadilika
 
Hao walimu wapya itabidi wawe wavumilivu, vinginevyo miongoni mwao wataikimbia ajira hiyo mapema kwa njaa ukichukulia wengine tayari walikuwa wana miradi iliyokuwa inawapa kipato mpaka wakaanzisha familia.Sasa kama kuna suala la uhakiki wa NECTA lipo mpaka hilo zoezi likamilike litachukua muda mrefu,na huu utakuwa ni usumbufu,iweje wawapangie vituo bila kujiridhisha wakati TAMISEMI na NECTA ni taasisi za serikali? TAMISEMI ilitakiwa kwanza ipate taarifa za NECTA kama taarifa za hao waajiriwa ni sahihi ndiyo wapangiwe halmashauri za kwenda kuripoti na pia mafungu ya fedha za kujikimu yapo wakati wakisubiri majina yaingizwe kwenye payroll.Barua ya ajira hufuata na hatimaye barua ya kuthibitishwa kazini kazini huja.Hao walimu wavumilie kuna taratibu za ajira zitachukua muda kukamilika
Sidhani kama kuna uhakiki wa NECTA kama upo mbona wengine wameshalipwa posho yao ya kujikimu?
 
Nimekumbuka mbali sanaa jinsi nilivyofanyiwa kwenye ajira yangu na serikali, barua ya kazi na kupangiwa kituo nimepewa, nimeacha kazi yangu nimeripoti kituoni nimekaa mwezi kwenye kituo cha kazi baadae naambiwa ajira zetu zimefutwa hili sitalisahau na Mungu ni Mwema kila wakati
Ongezea nyama kidogo mkuu.
Ilikuwaje ukaachishwa kazi kizembe hivo
 
Ongezea nyama kidogo mkuu.
Ilikuwaje ukaachishwa kazi kizembe hivo
Kuna dhuluma kubwa inafanyika hasa hichi kipindi cha awamu ya tano, nilipigwa danadana nikaamua nising'ang'anie labda haikua kher kwangu. vijana tusikate tamaa! !
 
pola sana aysee!
 
Nimekumbuka mbali sanaa jinsi nilivyofanyiwa kwenye ajira yangu na serikali, barua ya kazi na kupangiwa kituo nimepewa, nimeacha kazi yangu nimeripoti kituoni nimekaa mwezi kwenye kituo cha kazi baadae naambiwa ajira zetu zimefutwa hili sitalisahau na Mungu ni Mwema kila wakati
Pole sana mkuu. Huwa yanatokea haya. Ni jambo la kawaida tu katika maisha ya jamii
 
Kuna ajira mpya wamesain 756k. Nakawaza na sisi wa zaman itaingia 756k nashangaaa leo kitu 716k iko pale pale
 
Kwa manispaa per diem ni 80,000 kwa TGTS D siku 7 itakuwa 560,000/=
Wewe ni kilaza..unapojibu swali uwe makini.

Nimekuuliza posho ya kujikim ni shngap wametoa?

Kwenye mshahara kuna sintofaham..wengine wamesain 750k wengn 756k
 
Kwanini viwango vitofautiane wakati wote ni intake moja
 
Hata mimi nimeshangaaa. Ajira mpya wengi wamesaini 756k wachache niliowauliza wamesainib716k. Ila amini usiamini mahali TANZAGIZA ilipofikia chochote kinaweza kutokea maana ni nani anaweza kuhoji. Sio vyama vya wafanyakazi sio mimi sio ww yaaan awamu hiii ukisema suuuuuuuu ndo umewekwa pembeni jumlaaaa na figisuuu juuu
 
Binafsi niliripoti tangu 3rd December lakini hakuna linaloendelea. Wanadai wametuma Vyeti vyetu Necta ili vihakikiwe kwanza. Yaani kila kitu Afisa utumishi anadai kuwa hadi Uhakiki ujibiwe na Necta
Ndo utaratibu ndugu sio kwako tu wenzako wamepita humo lazima NECTA wahakiki kwanza

Sent from my TECNO CF7 using JamiiForums mobile app
 
Hata mimi nimeshangaaa. Ajira mpya wengi wamesaini 756k wachache niliowauliza wamesainib716k. Ila amini usiamini mahali TANZAGIZA ilipofikia chochote kinaweza kutokea maana ni nani anaweza kuhoji. Sio vyama vya wafanyakazi sio mimi sio ww yaaan awamu hiii ukisema suuuuuuuu ndo umewekwa pembeni jumlaaaa na figisuuu juuu
Pia kuna uzi humu mdau alitupia salary slip basic inasoma 736k yani ni mkanganyiko juu ya mkanganyiko
 
Mkuu punguza panic, wenzenu waliwahi kukaa miezi4 bila salary, pesa ya kujikimu walipata baada ya miezi7.
 
Hata mimi nimeshangaaa. Ajira mpya wengi wamesaini 756k wachache niliowauliza wamesainib716k. Ila amini usiamini mahali TANZAGIZA ilipofikia chochote kinaweza kutokea maana ni nani anaweza kuhoji. Sio vyama vya wafanyakazi sio mimi sio ww yaaan awamu hiii ukisema suuuuuuuu ndo umewekwa pembeni jumlaaaa na figisuuu juuu
mkuu inaonekana watu wa sayansi ni 756k na wa arts ni 716k
 
Back
Top Bottom