TAMISEMI kama mmeshindwa kuandaa mifumo mizuri ya watu kuomba ajira ni bora mkarudisha zama za posta. Mfumo umekuwa usumbufu

TAMISEMI kama mmeshindwa kuandaa mifumo mizuri ya watu kuomba ajira ni bora mkarudisha zama za posta. Mfumo umekuwa usumbufu

Yap mfumo unazengua lakini katika hyo changamoto ya kuedit taarifa ipo unachotakiwa kufanya ni kama unatumia simu inatakiwa uiseti kwenye mfumo wa desktop kwa kubonyeza vitufe vitatu vya kulia kwenye browser unayotumia na utaweza kufanya editing
Kukosea kujaza unapoomba kazi ni uzembe wa kupindukia issue nzito kama hiyo inabidi kutuliza kichwa

Tatizo unakuta kijana anawaza huku ana head phone masikioni akiburudika na mziki!!

Aende internet cafe kujaza mbona ziko kibao na komputa kibao
 
mimi huwa siapply mapema huu mwaka wa saba natuma application maana ni mhanga wa ajira toka 2015.pia baadhi ya changamoto kawaida kujitokeza kama hizo za kozi ndio maana wametolea ufafanuzi kozi zinazoonekana ndizo walizopata kibali.vipi ulisoma bachelor of education administration from UDOM
Digrii ya bachelor of education administration sio degree ya kufundisha ni ya uongozi katika shule na taasisi za elimu sio ya kufundisha darasani
 
Watuma maombi mjiandae tu kisaikolojia! Maana mtapigwa na kitu kizito kwa mara nyingine tena.

Haiwezekani watu 100 muombe nafasi ya kazi kwenye shule moja yenye uhitaji wa mwalimu mmoja tu wa somo husika! Hapa maana yake watu 99 hawana chenu!


Kama vipi vijana ingieni tu mtaani mpambane. Maana hakuna namna nyingine. Hii serikali yenu inawachezea tu shere. Mko zaidi ya laki 1! Halafu wanaajiriwa watu 9000 tu!

Hapo hapo kuna watu huko Tamisemi wana ndugu zao, wake zao, waume zao, watoto wao, vimada wao, wanaotaka kuajiriwa! Bado waliotoa rushwa, nk!
 
Kujaza kuomba kazi ni kama kufanya mtihani ukishakusanya hakuna kusema nipe ni edit!!

Uki send au move next basi ushakusanya hivyo no room for editing

Huko vyuoni mlikosoma hakufundishwa hayo?

Unakosea kosea kujaza application tu ukifika kazini kama daktari si utasahau kushona mgonjwa uliyemfanyia operation
 
Wanabodi salaam!
Serikali kupitia Tamisemi wametangaza ajira tar 20 mwezi huu kwa kada ya afya na elimu.Tunaishukuru serikali kwa hizi ajira kwani kimsingi hali ya ukosefu wa ajira imekuwa janga nchini.

Tatizo lililopo ni mfumo(system) kwenye uombaji hizi ajira unamatatizo yanayopelekea watu wengi kushindwa kuomba hizi ajira na hapa ndipo nimeona nimshuri Bashungwa kama wameshindwa kutengeneza mfumo mzuri wa watu kuomba ajira ni bora waturudishe posta ili kutoa fursa sawa kwenye uombaji hizi ajira.

Ukiingia kwenye a/c ya tamisemi instagram utaona watu wengi wenye malalamiko lakini wanakosa msaada,tamisemi wametoa namba ya simu kwa yeyote mwenye changamoto lakini namba haipatikani.

Kwenye huu mfumo wao,ukikosea kujaza na bahati mbaya ukasubmit hakuna namna yaku edit hata kama ni muda huohuo,ni mfumo wa hovyo sana.

Wapo watu wengi kozi zao hazipo kwenye mfumo na wanapo jaribu kuwataarifu tamisemi kwenye a/c yao instagram wanawajibu kwakuwapa namba ya simu ambayo haipatikani wakiwataka wawapigie ili wawakwamue.

Naomba sana serikali kwanza watatue hizi changamoto lakini pia waongeze muda watu wote wapate fursa yakuomba ajira kwani kwachangaoto za huu mfumo wiki mbili walizozitoa kwa watu kuomba hizi ajira hazitoshi.
Tunapolaumu mfumo tujipime wenyewe tunajua kuutumia huo mfumo? Mfumo was ajira ni mzuri na ni rafiki Kwa mtumiaji mwenye uelewa.
Changamoto kizazi Cha Facebook Kuna shida ya kuutumia mifumo.
Mfumo huu unaweza ku edit au kuondoa na kuweka upya taarifa zako changamoto Iko wapi?
 
Serikali isimamie mchakato wa kuwapangia mikoa/wilaya/vituo vya kazi waombaji wapya kwa weledi na bila upendeleo.Katika kikao Cha Bunge kinachoendelea,Kuna baadhi ya wabunge wamekiri kuwa, wapiga kura wao wanakwenda kuwalilia wawabebe vijana wao
Ushauri
1).Serikali Ni vema ikatoa vigezo vya kufanya uchaguzi wa waajiriwa wapi
2). Kamati ya upangaji wa watumishi wapya iongozwe na vigezo hivyo
 
Jinsi unavyoona ugumu wa mfumo kufunguka ndio ugumu huo huo utakao upata utakapofanikiwa kupchaguliwa kufanya kazi tamisemi
 
Tuwe wakweli mfumo hauna shida tatizo lipo kwa muombaji mfano mimi nimetumia dk 45 kukamilisha ila cafe niliofanyia kazi kuna waombaji hawana namba za nida,wengine wameshindwa kujibu maswali ya nida kama vile jina la mwisho au la kati la mama n.k. pia wengine yanatofautiana majina ya vyeti vya taaluma.nida na kuzaliwa na wengine hawana namba za nida kwa kifupi mfumo uko poa kwa sasa ila wazembe ndio wanalalamika ili kuukumbatia uzembe wao
Kutumia dakika 45 hiyo indicator mfumo unashida
 
Back
Top Bottom