Kukosea kujaza unapoomba kazi ni uzembe wa kupindukia issue nzito kama hiyo inabidi kutuliza kichwaYap mfumo unazengua lakini katika hyo changamoto ya kuedit taarifa ipo unachotakiwa kufanya ni kama unatumia simu inatakiwa uiseti kwenye mfumo wa desktop kwa kubonyeza vitufe vitatu vya kulia kwenye browser unayotumia na utaweza kufanya editing
Digrii ya bachelor of education administration sio degree ya kufundisha ni ya uongozi katika shule na taasisi za elimu sio ya kufundisha darasanimimi huwa siapply mapema huu mwaka wa saba natuma application maana ni mhanga wa ajira toka 2015.pia baadhi ya changamoto kawaida kujitokeza kama hizo za kozi ndio maana wametolea ufafanuzi kozi zinazoonekana ndizo walizopata kibali.vipi ulisoma bachelor of education administration from UDOM
Tunapolaumu mfumo tujipime wenyewe tunajua kuutumia huo mfumo? Mfumo was ajira ni mzuri na ni rafiki Kwa mtumiaji mwenye uelewa.Wanabodi salaam!
Serikali kupitia Tamisemi wametangaza ajira tar 20 mwezi huu kwa kada ya afya na elimu.Tunaishukuru serikali kwa hizi ajira kwani kimsingi hali ya ukosefu wa ajira imekuwa janga nchini.
Tatizo lililopo ni mfumo(system) kwenye uombaji hizi ajira unamatatizo yanayopelekea watu wengi kushindwa kuomba hizi ajira na hapa ndipo nimeona nimshuri Bashungwa kama wameshindwa kutengeneza mfumo mzuri wa watu kuomba ajira ni bora waturudishe posta ili kutoa fursa sawa kwenye uombaji hizi ajira.
Ukiingia kwenye a/c ya tamisemi instagram utaona watu wengi wenye malalamiko lakini wanakosa msaada,tamisemi wametoa namba ya simu kwa yeyote mwenye changamoto lakini namba haipatikani.
Kwenye huu mfumo wao,ukikosea kujaza na bahati mbaya ukasubmit hakuna namna yaku edit hata kama ni muda huohuo,ni mfumo wa hovyo sana.
Wapo watu wengi kozi zao hazipo kwenye mfumo na wanapo jaribu kuwataarifu tamisemi kwenye a/c yao instagram wanawajibu kwakuwapa namba ya simu ambayo haipatikani wakiwataka wawapigie ili wawakwamue.
Naomba sana serikali kwanza watatue hizi changamoto lakini pia waongeze muda watu wote wapate fursa yakuomba ajira kwani kwachangaoto za huu mfumo wiki mbili walizozitoa kwa watu kuomba hizi ajira hazitoshi.
Tatizo vinanunuliwa vifaa duni kwa pesa nyingi ndio tatizo watanzania wengi ni wezi.Haya mambo ya internet watz tumeyakimbilia mapema lakin serikal bado haijapata wataalam wazuri
Kutumia dakika 45 hiyo indicator mfumo unashidaTuwe wakweli mfumo hauna shida tatizo lipo kwa muombaji mfano mimi nimetumia dk 45 kukamilisha ila cafe niliofanyia kazi kuna waombaji hawana namba za nida,wengine wameshindwa kujibu maswali ya nida kama vile jina la mwisho au la kati la mama n.k. pia wengine yanatofautiana majina ya vyeti vya taaluma.nida na kuzaliwa na wengine hawana namba za nida kwa kifupi mfumo uko poa kwa sasa ila wazembe ndio wanalalamika ili kuukumbatia uzembe wao