TAMISEMI mnakosea sana mnapotaka kutoa ajira za walimu kwa upendeleo

TAMISEMI mnakosea sana mnapotaka kutoa ajira za walimu kwa upendeleo

Kweli mzazi huoni aibu kulipa 1,500/= kwa mwezi kwa ajili ya elimu ya mtoto wako? Hivi huwa mnategemeaga nini? Mi ningekuwa mwalimu mkuu wote mngelipa 10,000/= kwa mwezi
unapingana na elimu bure

1500 inatosha maana matoto yako mengi mno
 
“Inawezekana pia kufanikiwa mpaka kuwa millionaire bila kuajiria popote toka uzaliwe” By Regent.

Ningependa walimu kama moja ya taaluma yenye maslahi finyu kuishi katika msemo huu siku moja watanishukuru.
Mtu hana hata mtaji wa kufungua genge anawezaje kuwa millionaire?

Acha kutuzuga na conspiracy theories ambazo hazina maana katika maisha ya kawaida mkuu
 
Unaongea uongo kwa faida ya nani?

Mimi na wenzangu watatu, mmoja Mathematics, mmoja Physics na mmoja Chemistry rumejitolea shule moja hapa Dar toka mwaka jana na hatujawahi lipwa hata senti tano.

Mwisho wa siku ajira kapata mmoja wengine wote tumekosa wakaenda kupata waliokuwa private.

Kama kuna mtu anayejitolea na analipwa ni huko kwenu, huwezi sema kila anayejitolea analipwa.

By the way sijitolei tena sababu ajira zinatolewa kindugu.

MITANO TENA.
 
Wale hawajitolei bure kama wengi wanavyoamini isipokuwa wanalipwa na wazazi ndio wanachanga hizo pesa za kuwalipa
Tena ukute wanaojitolea wengi wao hawakwenda chuo cha ualimu ila kwakuwa wanajua kusolve math basi wanapewa chaki
 
Wanalipwa,kuna s/m huku wazazi/walezi tunalipa tsh 1500 kila mwezi kwa ajili ya mwalimu anayejitolea.
Na ukute hawajapita mafunzo ya ualimu yaani hawakwenda chuo cha ualimu ila kwakuwa wanajua kusolve math manawapa chaki wafundishe
 
Mtu hana hata mtaji wa kufungua genge anawezaje kuwa millionaire?

Acha kutuzuga na conspiracy theories ambazo hazina maana katika maisha ya kawaida mkuu
Nilikuwa najifunza Motisheni Skiping hongera kwa kunidukua.
 
Mkuu acha mtima nyongo
Sio mtima nyongo mkuu;keki ya taifa tugawane wote kidogo kidogo tuenee sio yote ipelekwe kwa kundi fulani la watu kwa kisingizio cha kujitolea...Sio fair
 
Then nadhani kila mtu asiye na ajira akajitolee basi
Shule hazina uwezo wa kubeba walimu wengi wa kujitolea kwa sababu hazina pesa za kuwalipa. Kama vipi serikali iweke utaratibu mzuri ili walimu wa kujitolea wawe wanalipwa na halmashauri uone kama shule hazitajaa walimu
 
Unaongea uongo kwa faida ya nani?

Mimi na wenzangu watatu, mmoja Mathematics, mmoja Physics na mmoja Chemistry rumejitolea shule moja hapa Dar toka mwaka jana na hatujawahi lipwa hata senti tano.

Mwisho wa siku ajira kapata mmoja wengine wote tumekosa wakaenda kupata waliokuwa private.

Kama kuna mtu anayejitolea na analipwa ni huko kwenu, huwezi sema kila anayejitolea analipwa.

By the way sijitolei tena sababu ajira zinatolewa kindugu.

MITANO TENA.
Michango ya walimu wa sayansi wanayo changishwa wazazi ni ya kazi gani?

Kuna shule kila mwanafunzi anayejiunga kidato cha kwanza kwenye joining instruction ameandikiwa mchango wa walimu wa sayansi 12,000/= kwa mwaka, nyingine 8,000/= nyingine 1,500/= kwa mwezi. Michango yote hiyo ni kwaajili ya malipo kwa walimu wanaojitolea na wanalipwa. Kama wewe hulipwi jaribu kufuatilia huenda michango inatolewa ila inaishia kwenye mifuko ya wanene.
 
Serikali iajiri watumishi ambao wengi walipunguzwa kwenye zoezi la vyeti feki badala ya kusisitiza kujitolea. Kwanza hao wanaojitolea huwa wanakula wapi kiapo cha utumishi wa umma ikiwa ni pamoja na kutunza siri, wengine hasa mabinti wanaojitolea badala ya kufanya kilichowapeleka wataanza kujilengesha kwa walioajiriwa ambao wengine ni maafisa waandamizi na hivyo kufanya mahusiano ya kikazi na ndoa kuingia mushkeli. Serikali acheni huo utaratibu wa kujitolea, ajirini watu kujaza nafasi zilizo wazi...
 
Usilalamike na wewe kajitolee, duniani kote first consideration huwa ni kwa volunteer maana mle wanakuwa washapata kauzoefu. So Mimi nakushauri ujitolee Mungu atafungua mlango wako
 
Na ukute hawajapita mafunzo ya ualimu yaani hawakwenda chuo cha ualimu ila kwakuwa wanajua kusolve math manawapa chaki wafundishe
Wapo wengi mkuu

Kuna mmoja kasomea uhandisi wa migodini(MINING ENGINEERING ) ajira imekuwa ngumu kwa upande huo yupo anafundisha physics kwenye shule ya kata
 
Kwa maana kinatoa mwanya kwa wakuu wa shule na maafisa elimu kata kuchomeka watu kwa hongo au ndugu zao kwa lengo la kuwasaidia kupata ajira serikalini kwa haraka.
Daftari la mahudhurio litatumika kuhakiki wanaostahili nasikia watakaobainika kuchomeka watu wao watakuwa na wakati mgumu
 
Daftari la mahudhurio litatumika kuhakiki wanaostahili nasikia watakaobainika kuchomeka watu wao watakuwa na wakati mgumu
This is too low, mkuu wa shule hawezi msainia kila siku kwenye hilo daftari la mahudhurio?
 
Back
Top Bottom