NAMBA MOJA AJAYE NCHINI
JF-Expert Member
- Oct 29, 2019
- 10,004
- 21,312
Za jioni!
Leo nitoe duku duku langu hili kuhusu mkoa wa Tabora, mkoa ambao ni duni sana kimaendeleo ukiwa na vichaa wengi na wakazi wake wengi wana kipato duni sana na miundombinu katika wilaya zake ni ya kuonea huruma!!
Nadhani TAMISEMI mnapaswa kuugawa mkoa huu mara mbili upatikane Mkoa wa Igunga na Mkoa wa Tabora ili wilaya kama Uyui zigawanywe vizuri ili kuzifikia kirahisi kimaendeleo!.
Haiwezekani Mkoa mkongwe wenye historia kubwa kama Tabora haukui kimaendeleo kwa kasi inayotakiwa! Eti hadi leo barabara ya lami kutokea Dodoma kupitia Itigi hadi Tabora bado haijakamilika!
Mkoa uliotoa Mawaziri wakubwa kama Kapuya na Sitta eti hauna maji ya kutosha, hospitali za kutosha yaani vurugu tupu! Eti pale mjini bado kunalimwa mahidi tena kati ya mji na nyumba za makuti hiyo ni fedheha na aibu kwa mkoa huu!
Wizara ya TAMISEMI inapaswa kuiboresha mikoa kama hii iliyojaa rushwa na ukabila ili kukuza uchumi wake kuliko kuiacha kuwa makazi ya vichaa wengi wanaongezeka kila mwaka! Hata watumishi wa umma hawakai kwa kukosa fursa! Watumishi wanahama sana Tabora kwasababu hapavutii kumejaa umimi na rushwa kibao. Bila hongo huwezi survive kwenye cheo cha uteuzi. Ni kawaida kuwaona wenye vyeo wakifungasha vyakula vya kusindika kuwapelekea wateuzi au maafisa kwenye halmashauri zao!
Ni aibu tupu!!
TABORA HAITAWALIKI BADO UMWINYI UMEJAA HUKU! NAAMINI PENDEKEZO HILI MTALIFANYIA KAZI!