Tuashumu wewe ungekuwa mwalimu, ungeenda huko kijijini ilhali nafasi ya kufundisha mjini ipo?
Kila mmoja anakula kwa urefu wa kamba yake.
Dada yangu alipangiwa Uyui Tabora , shule ipo kilometer 173 toka mjini, usafiri ni bus moja tu, ukichelewa unasubiri siku inayofuata. Ukishuka kwenye bus unatembea masaa matano kwa miguu.
Hakuna mwamko wa elimu, shule ina walimu watatu tu, hakuna madawati, madarasa yanavuja, nyumba za shule hakuna unalazimika kupanga nyumba kijijini umbali wa lisaa hadi shule.
Msimu wa kiangazi watoto wanaenda kuchunga ng'ombe hawahudhurii shuleni. Maji ya shida, umeme hakuna, barabara ni mbovu hakuna gari isipokuwa wakati wa mitihani ya drs la sana. Ukitaka kusafiri unalazimika kuamka saa Saba za usiku ili ukavizie bus njia panda.
Kwa mazingira kama hayo wewe au mwanao au ndugu yako ungeacha kutafuta vimemo?
Nilimhangaikia dada yangu akapata nafasi penye nafuu