TAMISEMI, suala la ustawi wa familia lichukulieni kwa uzito mkubwa

TAMISEMI, suala la ustawi wa familia lichukulieni kwa uzito mkubwa

N'yadikwa

JF-Expert Member
Joined
Aug 10, 2014
Posts
8,308
Reaction score
12,812
Tunafahamu kuwa utumishi wa umma unahusisha kufanya kazi popote pale kulingana na mahitaji ya Serikali.

Hata hivyo, ni muhimu pia kutambua kwamba familia ndiyo msingi wa jamii imara.

Kuna watumishi wengi, hususan wanawake walioolewa na wanaume waliooa, ambao hupangiwa vituo vya kazi katika mikoa tofauti na wenza wao.

Hali hii husababisha familia kuishi kwa kutengana kwa muda mrefu, jambo linaloweza kuathiri malezi ya watoto, ustawi wa ndoa na hata utendaji wa kazi kutokana na msongo wa mawazo.

Taifa imara hujengwa na familia imara. Suala hili ni sehemu ya kujenga maendeleo ya nchi, tukilitafakari katika picha ya Vision 2050.

Pale inapowezekana, TAMISEMI na mamlaka nyingine zinazohusika zingefikiria kuweka mifumo inayotoa kipaumbele cha kuwaunganisha wanandoa walio kwenye utumishi wa umma au angalau kuwapangia vituo vilivyo karibu ili kupunguza changamoto hizi.

Lengo si kupunguza mamlaka ya mwajiri kupanga watumishi kulingana na mahitaji ya huduma, bali ni kutafuta uwiano kati ya utoaji bora wa huduma za umma na kulinda taasisi ya familia.

Familia yenye utulivu hujenga mtumishi mwenye utulivu, mwenye ari ya kazi na anayetoa huduma bora zaidi kwa wananchi.

Hivyo, kuzingatia ustawi wa familia ni uwekezaji katika utendaji wa utumishi wa umma wenyewe.

Ndoa ni yuniti muhimu sana. Ipewe uzito katika kuilinda. Ndoa imara zitachangia kuwa na taifa imara.

N'yadikwa
 
Back
Top Bottom