TAMISEMI wametangaza ajira za afya leo kupitia Sekretarieti ya Ajira, sasa ni mwendo wa Interview

Sidhani kama wanawapigiwa lakin jitaidi umeweka mareferee watatu, kama wanavyotaka wao wasije wakakulima kichwa mapema, nasema hivi na ushahidi Kuna mwamba mmoja, aliliwa kichwa Kwa kutoweka refarees watatu yeye aliweka wawili tu ko jitahidi unaweka wote na details zao zote.
 
S
Sioni shida hapo!!!
 
Kuna dingi ana diploma sehemu ya academic qualification kajaza advanced diploma

mfumo unamtema huyu anatokaje hapa?
Awasiliane na PSRS ili waifute hiyo qualification aliyoijaza kimakosa, then atajaza kwa usahihi na ataweza kuomba kazi
 
Hao mareferee wako wana taarifa kuwa umewaweka kwenye CV yako au umewaweka tu bila wao kuwa na taarifa? Kama wanataarifa hamna shida. Isije ikatokea wametafutwa wakasema hawakujui.
 
Ukitaka kuepuka kigezo cha umri basi hakikisha umefaulu alama za juu kuwapita walio kuzidi umri msilingane!
 
Hao mareferee wako wana taarifa kuwa umewaweka kwenye CV yako au umewaweka tu bila wao kuwa na taarifa? Kama wanataarifa hamna shida. Isije ikatokea wametafutwa wakasema hawakujui.
Japokuwa referee Hua hawatafutwi Ila n muhimu sana kuwapa hy taarifa, mana huwez kujua
 
Habarini,hivi hizi ajira za tamisemi kupitia huu mfumo wa utumishi wa umma, kuna kuwa na interview? Kwamba ni mfumo mpya tumezoea miaka yote wanaombea uko tamisemi portal au wizara ya afya.je kuna uwezekano wa watu watakao chaguliwa kupelekwa moja kwa moja kazini bila interview?
 
Nami najiuliza. Hivi kama kutakuwa na interview ambayo ni online interview itakuwaje maana watu wanajaza permanent address na pia currently place of residence. Je siku ya interview itakuwa mkoa Kwa mkoa au mtu na kifaa chake? Eg simu au portable computer (PC) au watu watahitajika kukusanyika makao makuu ya mkoa husika? Na kama ni makao makuu ya mkoa husika ikitokea umesafiri nje ya mkoa uliojaza (address yako) itakuhitaji urudi mkoa husika Kwa ajili ya interview? Msaada wakuu maana hapo nyuma Sekretarieti ya utumishi wa umma walizindua online interview ima kupunguza ama kuepusha gharama Kwa wasailiwa
 
Ngoja waje
 
Hapo kwenye muhimu ongezea kuwa ni lazima.
Hapo wanaposema ku sign barua Kisha uambatanishe na vyeti vya taaluma sijaelewa naomba kufahamishwa.

Kwamba hivyo vyeti vya elimu pamoja na hiyo barua unaviambatanisha kwa kutuma kwenye anuani ya posta waliyoitaja ama vipi.
 
Hizi ajira ni mpya tujiandae kwa lolote.

Kama kitakuwa na interview sina uhakika hawatadeal na address nadhani tutafanya mkoa uliombea.

Tusubiri tuone
 
Sasa hicho kituo Cha usahili SI ndio kurundikana kwenyewe huko.

Hawa utumishi Wana mambo mengi sana mtu unaweza Kuta una sifa zote za kuomba ajira ukashindwa hata kufanya application.
Usaili unaweza usiwepo.
 
Usaili unaweza usiwepo.
Kwenye tangazo la ajira Kuna kipengele wanataka u sign barua ya maombi Kisha uiambatanishe na vyeti vya taaluma husika kupitia sanduku la posta walilotaja naomba ufafanuzi kidgo maana sijaelewa kwamba hivyo vyeti na barua vitumwe kwa njia ya posta badala ya online.
 
Hapo wanaposema ku sign barua Kisha uambatanishe na vyeti vya taaluma sijaelewa naomba kufahamishwa.

Kwamba hivyo vyeti vya elimu pamoja na hiyo barua unaviambatanisha kwa kutuma kwenye anuani ya posta waliyoitaja ama vipi.
Kutuma maombi n online kwenye huo mfumo wao ila n lazima uandike hy SLP yao.
Kuna kipengele cha academic qualifications hapo ndipo utaweka vyeti vyako kuanzia four, six mpaka chuo.
Barua n hatua ya mwisho kabisa baada ya kujaza taarifa zako zote, kwenye post ya kazi utaona sehemu pameandikwa apply ukigusa hapo utaletewa option ya kuweka pdf yako ya barua
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…