TAMISEMI wametangaza ajira za afya leo kupitia Sekretarieti ya Ajira, sasa ni mwendo wa Interview

TAMISEMI wametangaza ajira za afya leo kupitia Sekretarieti ya Ajira, sasa ni mwendo wa Interview

Na huu mfumo wa maombi utumishi ukoje? Mfano Dar Kuna nafasi 5 Ina maana wakiomba watu wa5 ndio inakulazimu uombe kwingine kwenye nafas ama ndio mnaomba tu ila wao ndio watachagua wanaowahitaji kwa mkoa husika?
Mkuu huu mfumo sio kama TAMISEMI kwamba ukiomba tu unasubiri upangiwe hapana,hapa ukifanikiwa kuwa shortlisted unaitwa kwenye usaili wa kuandika (written) then oral washindi wa nafasi huwa wanapatikana baada ya usaili kuogea yaani oral,hivyo nafasi ata ikowa 1 au 5 kama ulivosema mtaomba ata elf 5 na mnaweza kuitwa kwenye usaili wote kama sifa mnazo ili mkashindane

Ni mitihani ni zile UE maambo uliyosoma darasani lakini itategemea na job desrcription ya kada uliyoomba
 
Ahsante sana mkuu umeandika vyema sana
 
Muda si mrefu chawa wakiamka utasikia
Serikali ya mama yamwaga ajira kwa mamilioni ya watanzania
Wananchi walia vilio vya furaha na kububujikwa machozi
Mama ameaandika tena historia nyingine ya kipekee haijawahi kutokea tangu tupate uhuru.
😂😂😂😂😂😂😂😂😂Umetisha mkuu aiseeee
 
Nikitaka kuappply niambiwa hivi
IMG-20240706-WA0022.jpg
 
Upigaji tu. Kwani Kuna umuhimu gani na ulazima upi wa ku certify vyeti? Technology na mambo ya kizamani Sana. Upo Karne ya 21 lakn unaishi kama upo Karne ya 19 huko. Ondoeni hicho kigezo Cha ku certify vyeti.
Hamna namna, kama uko interested na hizo nafasi, certify vyeti omba.

Kama hauko interested, acha wengine wafanye na usiwahadae kwa mtazamo wako.

Pia acha mawakili/wanasheria nao wapate za kumwagilia moyo.

Kingine, kama taalauma yako haiwezi kukuingizia hela moja kwa moja au siyo moja kwa moja lazima uone nongwa kwa wale ambao wanaweza kupata za kubrashia kupitia taaluma zao kwa urahisi.

Binafsi naheshimu taaluma za watu na huwa sioni shida kulipia huduma inayotokana na taaluma ya mtu
 
Sijapinga. Nataka umuhimu na ulazima wa kufanya hivyo ukiondoa kutengenezea mawakili na wanasheria upigaji wa nje nje.
 
Na huu mfumo wa maombi utumishi ukoje? Mfano Dar Kuna nafasi 5 Ina maana wakiomba watu wa5 ndio inakulazimu uombe kwingine kwenye nafas ama ndio mnaomba tu ila wao ndio watachagua wanaowahitaji kwa mkoa husika?
Nimemfanyia rafiki yangu Application leo.

Tulijadili na jamaa yangu achague mikoa 5 then aombe hiyo mikoa.

Ila nilipoanza kuomba mkoa wa kwanza, nilipomaliza, zikaandika kwa pamoja kwenye nafasi zote mikoa yote kuwa ALREADY APPLIED then jina la Mwajiri likajitokeza ni MDAs and LGAs kule kwenye MY APPLICATIONS.

Kwa hiyo utakapoomba mara moja ndio imeisha hiyo, itabaki sasa utakapoitwa kwenye Interview na ukatusua, utaweza kupangiwa mkoa wowote au mkoa ulioomba wakati wa Application
IMG-20240708-WA0001 (1).jpg
 
Nimemfanyia rafiki yangu Application leo.

Tulijadili na jamaa yangu achague mikoa 5 then aombe hiyo mikoa.

Ila nilipoanza kuomba mkoa wa kwanza, nilipomaliza, zikaandika kwa pamoja kwenye nafasi zote mikoa yote kuwa ALREADY APPLIED then jina la Mwajiri likajitokeza ni MDAs and LGAs kule kwenye MY APPLICATIONS.

Kwa hiyo utakapoomba mara moja ndio imeisha hiyo, itabaki sasa utakapoitwa kwenye Interview na ukatusua, utaweza kupangiwa mkoa wowote au mkoa ulioomba wakati. wa ApplicationView attachment 3036746
Ahsante sana mkuu.
 
Kama Kuna ulazima na umuhimu na si mazingira ya upigaji na kuwatengenezea ma deal wanasheria na mawakili, basi waelekeze Kila wilaya/halmashauri awepo wakili/mwanasheria wa serikali atakae kuwa special Kwa ajili ya kutoa huduma ya ku certify hivyo vyeti. Ikibidi awepo Kila kata maana majobless wapo wengine mno na kama itashindikana kuwepo Kila kata basi katika kata tatu au nne awepo mmoja Kwa ajili ya kufanya zoezi Hilo yaani free of charge. Tofauti na hapo ni mradi tu wa kuwapiga ma jobless. Sipingi ku certify vyeti nachopinga ni mazingira ya upigaji na usumbufu Kwa wanaoomba nafasi hizi za kazi. Maana bila pesa huombi isitoshe hatufanani kiuchumi na pia si Kila sehemu kuna wakili wala mwanasheria hivyo itabidi tu watumie gharama kuwafuata na pia ukifika huko waliko watahitaji pesa na si chini ya elfu 5000 per certificate.
Ukisema hiyo service charge haifai ndio kupinga kwenyewe
 
Hii awamu kwa muda wa miaka hii mitatu na nusu imetoa ajira kuliko miaka yote ya kukwete mitano ya mwisho na magufuli.
Hapana, kwa Kikwete sikubaliani na wewe.

Kikwete alitoa kila baada ya watu kuhitimu chuo ualimu na Afya kuanzia ngazi ya cheti hadi Degree.

Watu waliohitimu mwaka 2014, walipata bila kikwazo ila waliohitimu mwaka 2015 ambapo muda mfupi Mwendazake akashika Dola ndio walianza kukiona cha mtema kuni.
 
Back
Top Bottom