Doubleg Malafyale
JF-Expert Member
- Feb 17, 2017
- 2,733
- 3,561
Swali zuri sana mkuu.Nami najiuliza. Hivi kama kutakuwa na interview ambayo ni online interview itakuwaje maana watu wanajaza permanent address na pia currently place of residence. Je siku ya interview itakuwa mkoa Kwa mkoa au mtu na kifaa chake? Eg simu au portable computer (PC) au watu watahitajika kukusanyika makao makuu ya mkoa husika? Na kama ni makao makuu ya mkoa husika ikitokea umesafiri nje ya mkoa uliojaza (address yako) itakuhitaji urudi mkoa husika Kwa ajili ya interview? Msaada wakuu maana hapo nyuma Sekretarieti ya utumishi wa umma walizindua online interview ima kupunguza ama kuepusha gharama Kwa wasailiwa
Mkuu iko hivi usaili unafanyika mkoani kwa maana wana vituo maalumu vya kufanyia mirihani katika kila mkoa hivi vituo ni computer lab za vyuo mfano VETA,OUT, n.k utaratibu wa usimamizi ni ule ule kama ule wa paper based examination utakaguliwa vyeti na kusimamiwa na wasimamaizi zaidi ya mmoja ndani ya chumba cha mtihani
Computer ziko connected na mtandao na utakuta wamefungua mfumo wa mtihani yaani (Online aptitute test system ),kisha utaambiiwa u log in kwa kutumia password na username unayotumia kwenye akautn yako ya ajiraportal kwa hiyo hakikisha muda wote unaikumbuka username yako na password
Kisha muda ukifika mtaruhusiwa kuanza mtihani maana muda wa kuanza ni mmoja kwa nchi nzima kama ilivyo mitihani ya NECTA
Mfumo una display muda unaobaki mfano mtihani ni dk 50 kwa hiyo zitakuw zinaonekana kwa kupungua mfano,utakua unaona pale kwenye screen dk zilizobaki 49.48 ......mpka 0 ikitokea hujamaliza kujibu maswali yote na muda umeisha basi mtihnai una jisubmit automatically ila kama umemaliza unaweza kusubmit ata kabla ya muda kuisha kuna option ya kusubmit itakuja baada ya kumaliza swali la mwisho
Mtihani unafunguka wote na unaweza kuanza swali lolote kwenye mitihani kwa maana swali la kwanza au mwisho au la katikati,au vinginevyo kama ilivyo kwenye paper based exams
Unakuwa jna screw kupanda na kushuka kama unavofanya ukiwa unasoma document yenye pdf n.k pale kazi yako unacheza na mouse tu basi keybord unatumia kwenyebkulog in tu basi kazi yake inakuwa imeisha
Kujibu maswali unacheza na mouse tu maana una tick au kuselect jibu unaloona ni sahihi na linabadilika rangi kuwa kijani au blue kama sijakosea,na unaweza rudia ukabadilisha jibu kamw umejiridhisha umejaza pumba,mfumo unakubali kubadili jibu
Kama una saili zaidi ya moja mfumo unakuruhusu ufanye zote kwa siku hiyo ila utafanya wa kwanza baada ya kumaliza utasubiri mruhusiwe kuingia sesion ya pili maana muda wa kuanza ni mmoja kwa nchi nzima,kwa hiyo kama uko na interview nyingi siku hiyo unaweza kaa mpaka jioni kwa chumba cha mtihani maana hutoruhusiwa kutoka, pia mabegi na vitu vyote munavikusanya mbele kwenye meza unqbaki wewe na kompyuta yako
Kingine ukiwa kwenye mfumo wa online aptitude test hauruhusiwa kufungua tab nyingine pale kwenye browser ,ukifanya hivyo mfumo unakutema kwenye mtihani automaticaly kwa hiyo unakuwa umeaga mashindano
Kabla ya mtihani mnapewa dk 10 za kusoma maelekezo umo umo online then mtaambiwa muanze mtihani
Kawaida ni saa 1 yaani dk 60 ila wamegawa dk 10 za kusoma instruction na dk 50 za mtihani
Maswali hayapungue 40 kwa kada husika ,na yanaweza kuzidi inategemea na kada walivoona inafaa ila muda ni dk 60 (dk 10 kusoma instruction na dk 50 kufanya mtihani)
Matokeo unayapata siku hiy0 hiyo unawekewa kwenye akaunti yako ya ajiraportal kwamba selected for oral interview au not selected for oral interview
Online aptitude test ni mchujo tu ukifanikiwa kupita oral (usaili wa mahojiano) itafanyika dodoma ofisi za psrs au kwingineko watakako panga kutokana na kada husika
Kama bado una swali karibu