TAMISEMI yafafanua taarifa ya kununua pikipiki 68 kwa Tsh milioni 789

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Wizara ya TAMISEMI imesahihisha taarifa yake iliyosomwa bungeni leo Aprili 14, 2022 na Waziri wa Wizara hiyo Innocent Bashungwa na kusema kwamba, Pikipiki za maafisa ustawi wa jamii zilizonunuliwa zilikuwa ni 268.

Kupitia taarifa iliyotolewa leo Aprili 14, 2022, na Mkuu wa kitengo cha mawasiliano Serikalini wa wizara hiyo imesema kwamba pikipiki hizo 268 zilinunuliwa kwa thamani ya shilingi milioni 789.9 na zilizosambazwa kwa awamu ya kwanza kwenye mamlaka za Serikali za Mitaa zilikuwa 68.

Thread 'Serikali yanunua Pikipiki 68 kwa milioni 789.8. Hizi ni aina gani za pikipiki?' Serikali yanunua Pikipiki 68 kwa milioni 789.8. Hizi ni aina gani za pikipiki?




Chanzo: TAMISEMI
 
Mahangaiko
Mitandao ya kijani inae kazi
 
Wanapika sana data..sio kwa hizo pikipiki tu kwa mengi..wakishitukiwa ndio wanakuja kutoa marekebisho..je kama watanzania wasinge hoji hicho kitu wangekuja kufanya marekebisho hayo.?

Usiniambie kuhusu uzalendo hii nchi ni shamba la bibi...watu wanakula kwa urefu hata mkulu karuhus hilo.

#MaendeleoHayanaChama
 
Basi ni za kichina
 
Pamoja na huo ujanja ujanja wa kujaribu kurekebisha takwimu ili kuficha huo wizi, bado upigaji unaonekana wazi, yaani piki piki ya boxer imenunuliwa kwa wastani wa milioni 3.
Ukienda leo dukani kununua reja reja pikipiki mpya ya Boxer inauzwa kwa wastani wa shilingi 2.5m, na kwa jumla pikipiki moja inauzwa kwa wastani wa shilingi 2m.

Sasa najiuliza kwa nini manunuzi ya serikali yanakuwa ya gharama kubwa?
 
Hiiii hajasema kama sio 11m kanunua kwa sh ngap!
kaona angesema bado yangemuwa madudu tuuu
 
Hata hiyo bado n uongo, kwa maana hiyo pikipiki moja wamenunua kwa mil 2.95???
 
Hii mijitu mijizi isiyo na aibu.
Yaani pikipiki 260 uuziwe kwa bei kubwa kwa kila moja kuliko anayenunua moja kwa rejareja huku ukinunua kuanzia 10 tu unauziwa kwa bei ya jumla
 
Anasema piki² 1 kununuliwa kwa tsh.11m sio sahihi.
.
Ila Hasemi kwamba hizo piki² 68 zilizosambazwa kwa awamu ya kwanza zilinunuliwa kwa kiasi Gani.
.
Acha wale asali bila mipaka ya urefu wa Kamba Yao.
 
Hii mijitu mijizi isiyo na aibu.
Yaani pikipiki 260 uuziwe kwa bei kubwa kwa kila moja kuliko anayenunua moja kwa rejareja huku ukinunua kuanzia 10 tu unauziwa kwa bei ya jumla
Haya mapikipiki yamenunuliwa awamu Hii. Ambayo alisemaga awamu Hii Hatutaona mambo ya hovyo² yakitendeka
 
Sheria ya manunuzi ni hovyo! unanunua kupitia taneps, mtu mwenye bei ya chini kabisa ana quote 3.2M, na unaambiwa uchukue the lowest price!

Manunuzi ya Umma, bado ni shida!
 
Tamisemi mnakuja kujibu hoja za mitandao not hoja na maswali ya wabunge.

Hakika kamba yako ikiwa ndefu kula, vuta kamba kale mpaka upande wa pili, wabunge kimyaaaa, wanaogopa kuhoji ahahaaaa...

Nchi imefunguliwa na unapigwa mwingi kweli kweli.
 
Uongo mtupu na hata kama ingekua ni kweli boxxer moja ni 2.4 means waziri kapiga cha juu 134,000,000.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…