TAMISEMI yawasilisha Bungeni makadirio ya bajeti yake ya mwaka 2025/26 Aprili 16, 2025

TAMISEMI yawasilisha Bungeni makadirio ya bajeti yake ya mwaka 2025/26 Aprili 16, 2025

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
5,352
Reaction score
15,876
Mkutano wa 19 wa Bunge la 12 unaendelea leo Aprili 16, 2025 bungeni Jijini Dodoma ambapo hotuba ya bajeti ya Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kwa mwaka wa fedha 2025/2026 itasomwa na kuanza kujadiliwa.

Shughuli nyingine ni Waziri wa Fedha Dkt. Mwigulu Nchemba kuwasilisha hati mbalimbali mezani ikiwemo ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kuhusu Ukaguzi wa Taarifa za Fedha za Serikali Kuu kwa mwaka wa fedha ulioishia Juni 30, 2024.

Kama kawaida kutakuwa na Kipindi cha Maswali na Majibu kwa wabunge kuiuliza maswali Serikali.


Waziri wa TAMISEMI, Mohamed Mchengerwa, amesema kuwa katika mwaka wa fedha 2024/2025, Wizara hiyo iliidhinishiwa jumla ya Shilingi bilioni 254.82 kwa ajili ya kuratibu na kusimamia uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa mwaka 2024.

Akizungumza leo Aprili 16, 2025, Bungeni jijini Dodoma wakati wa kuwasilisha hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya wizara yake kwa mwaka 2025/2026, Mchengerwa alisema:

“Kuhusu Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa mwaka 2024, Ofisi ya Rais – TAMISEMI iliidhinishiwa Tsh. bilioni 254.82 kwa ajili ya kuratibu na kusimamia uchaguzi huo. Kati ya fedha hizo, Tsh. bilioni 247.03 zilitoka Serikali Kuu na Tsh. bilioni 7.78 zilikuwa ni mapato ya ndani ya halmashauri kwa ajili ya uchaguzi.”
Alifafanua kuwa uchaguzi huo ulihusisha ngazi za msingi za uongozi, zikiwemo nafasi za wenyeviti wa vijiji, mitaa, vitongoji, pamoja na wajumbe wa halmashauri za vijiji na kamati za mitaa.

“Shughuli zilizotekelezwa ni pamoja na uhakiki wa maeneo ya utawala yaliyojumuisha kata 3,956, vijiji 12,333, mitaa 4,269 na vitongoji 64,274, uandaaji wa nyaraka, uhamasishaji na utoaji wa elimu ya mpiga kura, ununuzi na usambazaji wa vifaa pamoja na uratibu wa usimamizi, ufuatiliaji na upigaji kura wa kuchagua viongozi hao katika Mamlaka za Serikali za Mitaa,” alieleza Mchengerwa.
Katika hatua nyingine, Mchengerwa amesema Ofisi ya Rais – TAMISEMI imewasilisha bungeni makadirio ya mapato kwa mwaka 2025/2026 yenye thamani ya takribani Shilingi trilioni 11.783 kwa ajili ya wizara na taasisi zilizo chini yake. Bajeti hiyo imeongezeka kutoka Shilingi trilioni 10.125 za mwaka 2024/2025 hadi trilioni 11.783, ikiwa na ongezeko la zaidi ya trilioni 1.66.

“Shilingi trilioni 3.95 zinaombwa kwa ajili ya miradi ya maendeleo, ambapo kati ya hizo, Shilingi trilioni 2.5 ni fedha za ndani, ikijumuisha Shilingi bilioni 613.44 za mapato ya ndani ya halmashauri na Shilingi trilioni 1.45 ni fedha za nje. Aidha, Shilingi trilioni 7.84 ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida yanayojumuisha mishahara Shilingi trilioni 6.3 na matumizi mengineyo Shilingi trilioni 1.53, ikiwemo Shilingi trilioni 1.067 za mapato ya ndani ya halmashauri,” alisema.

“Tumewasilisha si tu makadirio ya mapato na matumizi, bali tumeweka mbele yetu dira ya matumaini, ramani ya maendeleo na ahadi ya uongozi unaowajibika. TAMISEMI haitafuti sifa ya kisiasa, tunatafuta suluhisho sahihi kwa maisha ya Mtanzania wa kawaida,” alisisitiza Mchengerwa.

Alihitimisha kwa kutoa wito kwa mikoa, mamlaka za serikali za mitaa na wananchi wote kushirikiana kwa mshikamano:

“Kwa dhamira hii, na kwa imani kubwa katika maono ya Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, tunawasilisha bajeti hii kama zana ya kazi, dira ya matumaini na silaha ya mapinduzi ya kiutawala, kiuchumi na kijamii. Kwa hiyo, tunasema kwa ujasiri mkubwa, TAMISEMI ndiyo msingi wa maendeleo endelevu. Kila Shilingi ina jukumu, kila kiongozi ana wajibu na kila mwananchi ana nafasi!”
 

Attachments

Hili Bunge ni la one man army.

"Strongest man is the one who stand alone" - reference Alvl
 
Back
Top Bottom