TAMISEMI yawataka watumishi kuripoti kazini saa 1:30 asubuhi

TAMISEMI yawataka watumishi kuripoti kazini saa 1:30 asubuhi

Watumishi wa kada kama za ualimu, uuguzi, udaktari, uaskari, nk. Zinatakiwa zijengewe makazi bora karibu na maeneo yao ya kazi ili kuboresha utendaji wao wa kazi.

Na siyo kutoa tu matamko ya kukurupuka ya kuwataka wafike saa 1:30 asubuhi, huku ukiwa hujui hao watumishi wanaishi umbali gani kutoka maeneo yao ya kazi.
 
Kingine Hawa viongozi Huwa wanahisi walimu kma ndo chuo au uwanja wao wa mazoezi ya kujifunzia uongozi na mikwaraaaa

Badala aanze na uozo uliopo pale ofisini kwao TAMISEMI,
watu wavivu,wapiga deal za uhamisho na watoaji Vibali fake

Lkn anahisi uongozi Bora ni kuwatisha Walimu tu
 
Kawahi na cruiser yake anaenda kupiga mikwara walimu wako kwenye foleni ya daladala huko.
Kibongo usafiri majaliwa tu,
shukuru mradi mtu kafika hata kazini.
 
Watumishi wa TAMISEMI mmefikiwa huku

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI), Reuben Kwagilwa amewataka watumishi wote waliopo chini ya Tamisemi nchi nzima kuzingatia muda wa kuripoti na kudumu kazini kulingana na kanuni za kudumu za utumishi wa umma.

Amesema watumishi wanapaswa kufika kazini saa 1:30 asubuhi, kuanza kazi mara moja na kudumu hadi saa 9:30 alasiri, ili kuhakikisha wananchi wanahudumiwa ipasavyo na kwa ufanisi.

View attachment 3506714

Akiwa katika ziara yake katika Shule ya Msingi Kisasa jijini Dodoma leo Novemba 24, 2025, Naibu Waziri Reuben amesema alipowasili shuleni hapo na kusaini kitabu cha mahudhurio saa 1:30 asubuhi, alikuta akiwa mtumishi wa 16 kusaini licha ya shule kuwa na takribani walimu 55, jambo alilolieleza kuwa ni ishara ya kutokutiliwa mkazo kwa taratibu za kazi.

Amesema maelekezo hayo anayatoa kwa niaba ya Waziri wa Tamisemi, Prof. Riziki Shemdoe, na kwamba serikali inalenga kuhakikisha Watanzania wanahudumiwa kwa wakati, wanasikilizwa na changamoto zao zinashughulikiwa ipasavyo.

“Hatuwezi kupeleka tabasamu kwa Watanzania kama hatuwahi kazini na hatudumu kwa muda tuliopangiwa. Watumishi wote hakikisheni mnazingatia hili,” amesema.

Aidha, amewataka wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya nchini kusimamia kikamilifu utekelezaji wa maelekezo hayo katika maeneo yao.
Hivi anajua kuwa saa moja kwa mkoa kama Kigoma bado ni giza?
 
Punguzeni kodi za magari hao watumishi wachukue Honda Fit wawahi kazini ikiwezekana wakopesheni maisha yaendelee sio wanajibana kwenye boda boda..
 
Back
Top Bottom