Tamko la Baraza Kuu la Jumuiya za Ansaar Sunnah Tanzania (BASUTA) kuhusu mkataba baina ya Tanzania na DP World

Sawa Ibills bin Shetan. Mawazo yako yatazingatiwa pia
 
Haya makanisa ya hapa Tanzania yanaendeshwa na Mafarisayo na Masadukayo. ,wanaokula hela za watu eti sadaka ya bwana.
majirani zangu hapa wamelalamika na sasa hawatoi tena hela yao kuwapa mafarisayo na masadukayo waliozamia kwenye makanisa.
mbona kama unaandika upuuzi, kwani misikitini sadka hazitolewi masheikh wapokee? Unajua kutoa sadaka ni hiari na ni tendo la imani katika kufanya ibada? Panua wigo wa akili yako ufahamu mengi
 
Wamejibu kuhusu vipengele vyenye utata vya mkataba, au wanamtetea mwenzao katika imani hata kama hayupo sahihi?
Duh nanukuu..

"Hivyo basi, sisi BASUTA tusingependa kujikita kwenye mjadala wa vipengele mahususi wa Mkataba wenyewe wa bandari tukiamini mchakato unaenda vizuri na maslahi mapana ya taifa yatafikiwa"
 
TEC wanaogopa influence ya uislam hapa Tanzania, lakini huu upepo wa mabadiliko ya uchumi mzima wa dunia haukwepeki.

Naielewa hoja ya maaskofu ya kutotaka kupoteza ushawishi na heshima ya ukatoliki nchini, nauona ugumu wa matamanio ya kanisa kudumu kwa muda mrefu.

Waarabu wameshatuzunguka kila kona, muda huu Paul Kagame keshamalizana nao tayari Tshisekedi kule Congo keshamalizana nao tayari, wanasubiri sisi tumalize kujenga reli na biashara ianze.

Unapopinga uwekezaji wake ukumbuke kuwa michakato ilianza tangu 2015 na imeshakula matrilioni ya pesa, kusubiri eti wazawa wawe na uwezo wa kuendesha biashara zao wenyewe ikiwemo bandari ni suala la imani ya askofu yeye binafsi, halifanani kabisa na uhalisia wa uchumi mzima wa bandari.
 
Tatizo la TEC ni kutoamini kwenye mawazo mbadala,kujiona wao ndo kila kitu hapa wamegonga mwamba ,mwarabu ni kama maji kwa zama hizi haiwezekani kwa namna yeyote.
 
Mzee wenu kauza lolliondo ile sio yetu tena, leo mnampa na bandari na kuna tetesi za chini ya kapeti KIA Nayo bai bai ni suala la muda tu .yan kwenye nchi yenu evry where mtakuta waarabu na watawakagua identity zenu. Uhuru wenu uko wapiii??. Kuna sehemu yeyote wew mweusi unamiliki mali zao kule kwao??? Mnawapa Airports , Bandari,na mbuga za wanyama Nyie mna akili kweli?? Dah Tanganyika nchi yangu roho inauma sana
 
Hili nalo mkaliangalie
 
Ushauri: Mimi naomba Muslims , Christians na wasiokuwa na dini njoeni tukae meza moja sisi kwa pamoja ni watanzania na hii nchi ni yetu sote! Tuanze kuwauliza serikali where is our loliondo?, why did you chase the maasai our brothers and sisters from their natural land ngorongoro? We need them back!!! , stop ur nonses with our ports!! Na Kia yetu na mbuga za wanyama zibaki kwenye mikono ya watanzania. Hatuwezi kuwa wajinga kiasi hiko tushindwe kuthibit hadi fisi pale manyara. Umoja wetu ndio nguvu ila tukigawanyika hivi hatuna chetu!
 
Good points,ninakushukuru sana mtu wa Mungu.
 
Mimi najiuliza..
Ni lini TEC waliwaandikia waislam waraka mbona wanajipa kazi ya kuwajibu?
Kuna kipengele hata kimoja ndani ya waraka kimeongelea waislamu au uislamu?
Waraka wa TEC umeelekezwa kwa serikali ambayo ndiyo iliingia mkataba huu, wao ndio wanapaswa kujibu hoja za TEC.

Hili la baadhi ya waislamu kujipa jukumu la kuijibia serikali kwa kujificha kwenye dini bila kuchambua hoja yoyote, inaleta mashaka makubwa kwamba wanatumiwa na serikali baada ya serikali kushindwa kujibu hoja nzito zilizowekwa wazi na TEC na wamehongwa kufanya hivyo.

Nilitegemea taasisi nyingine zije na maoni yao, sio kujibu maoni ya wengine kwani
Kulazimisha watu tuamini kwamba kukosoa au kutounga mkono mkataba ni udini halafu kupongeza au kuunga mkono mkataba sio udini ni UPUMBAVU.

Halafu kuunga mkono mkataba mbovu eti kwasababu kuna mikataba mingine mibaya iliyopitishwa kupindi cha nyuma, huu ni ujuha uliokomaa.
 
hapo ni waislam ndo wanaleta udini maana wenzao wameweka hoja zao zisizogusa dini ya mtu ila wao wanashambulia watoa maoni baada ya kuleta hoja zao za kuunga mkono huu mkataba
 
kituko waarabu wanawaita hawa ni watumwa ila wao wanalazimisha uswaiba
 
Kwenye hili la bandari viongozi wa waislam wanajizalilisha sana Khaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…