Tamko la Baraza la Maaskofu wa Kipentekoste (PCT) kumjibu Kaimu Katibu Mkuu Kiongozi

Tamko la Baraza la Maaskofu wa Kipentekoste (PCT) kumjibu Kaimu Katibu Mkuu Kiongozi

Mhabarishaji

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2010
Posts
1,007
Reaction score
600
attachment.php
 
Attachments

  • maaskofu.jpg
    maaskofu.jpg
    122.1 KB · Views: 6,969
Mungu awabaliki sana kwa kukubali kiaina.......
 
Mambo ya Walawi 18:7
Utupu wa baba yako, wala utupu wa mama yako, USIUFUNUE, maana ndiye mama yako; Usiufunue utupu wake.

Jamani ndo tumenyang'anywa haki yetu kirahisi hivi?? Mbona mimi sisikii kukubali kirahisi hivi? Maweeeeeeee!! Uwiiiii !! Huu ni ukandamizaji....
Askofu wangu Gwajima na Askofu Kakobe vipi jamani.... Haki zetuu.... PCT why are you backing down??
 
Baraza la maaskofu wa kipentecoste lilalamikia ubaguzi katika
1. Bunge la katiba

2. Kunyimwa nafasi radio na TV ya taifa

3. Kubaguliwa kwenye maombi ya kumsimika rais

Kama kwenye bunge hawakupeleka majina je hayo mengine walikaribishwa wakakataa?
 
Serikali yetu ..... Hii Katiba inaweza kwenda miaka mingine hamsini (50) tukiikosea nafasi tusije kujilaumu baadaye sisi Wapentekoste... Umoja wetu katika hili uko wapi?? Kweli tujikaze kisabuni katika jambo hili? Tusisubiri Maaskofu watusemee....
 
Wakiulizwa watasema wametumia hekima na wameongozwa na roho. Ukiniuliza mimi nitasema biblia haiwaagizi wao kuwa waoga kiasi cha kushindwa kusema kweli na kutetea maslahi ya wanyonge. Hivyo kwa msimamo huo waelewe wamekubaliana na upuuzi wote utakaofuatia ambao serikali imeshaanza kuufanya na itakaoendelea kuufanya.
 
Ningeshangaa sana kama kweli Maaskofu wa Kipentekoste wangeweza kuitisha Press Conference na kutoa manung'uniko yao kuhusu kutupwa kwa majina yote waliyoyapeleka, wakati hawakuwahi kupeleka hata jina moja Ikulu! Siasa za Tanzania bhana!
 
Sio rahisi PCT kuibuka tu... Nijuavyo Gwajima na Kakobe na Shemsanga ni watu makini sana... Wasingetokeza pua zao pale kama hiki kitu kingekuwa si kweli...
 
Kweli wewe ni "NAPITA", nakuona umepita tu hapa na kutoa comment, bila kusoma tamko lote.

Hebu lisome vizuri ulielewe Uungwana na Vitendo ndo walichofanya kuwa Great Thinker.
 
Nina wasiwasi na uongozi mzima wa Baraza la Maaskofu wa Kipentekoste Tanzania... kama mlioneana wivu katika kuchaguana nani awe na nani asiwe hiyo itakuwa imekula kwenu.....Kwa kukubali yaishe Maaskofu nyinyi mtakuwa hamjawatendea haki wafuasi.... hapa lazima kuna mkono wa uzembe mlioufanya katika uongozi wenu..la sivyo itabidi miongoni mwenu mjiuzuru maana hamkuwajibika na sasa mnaitumia biblia visivyo.... acheni kuwa waoga semeni kila kitu... kwa kuwa mkisema kweli kweli hiyo itawaweka huru nanyi mtakuwa huru kweli kweli.... waoga wote sehemu yao ni katika ziwa liwakalo moto na kibiriti.....
 
...kwa kuwa viongozi wa Kipentekoste hawakuwa na nalengo yanayofanana na magamba,ilikuwa sio raisi mwenyekiti wa chama chakavu kuwateuwa...
 
Hawa PCT wanahangaika sana. Wangekuwa waungwana kama wangetaja hayo majina. Maadam hawakupeleka, ndo maana wameshindwa kututajia humu
 
Waheshimiwa Watumishi wa Bwan, Nadhani kukaa kwenu kimya na kwa nukuu mliyotuonyesha haiwezi kuwa jibu sahii la kuiponya nchi yetu. Kwa vile Ikulu imeshawakana kwamba hamkuwasilisha majina kwa wakati ni bora maksema Ukweli.

Kumbukeni Mtumishi mwenzenu, Mzee Nathani aliposikia uovu uliotendwa na Mfalme Daudi hakukaa kimya kwa madai kama yenu kwamba hampaswi kuufunua uchi wa Baba mzazi. Ebu wasaidieni Watanzania na waumuni wote wajue ukweli wa nini kilichojiri. Siamini kabisa kwamba mnasema uongo, ni vema mngenyamza kabisa kuliko kulalamika halafu kisha mkatusomea mstari mmoja wa Biblia kwamba hataufunua uchi wa mzazi wenu. Ili kutibu majeraha yenu na sisi wafuasi wenu ni afya mkisema ukweli ili wahusika wafike mahali waombe radhi na kusameheana hadharani
 
Mkuu, sasa unafikiri watasema nini wakati hayo majina hawakupeleka? Kuendelea kujadili uzi huu ni kupoteza muda
 
Its over,

Pentecoste let it go,

Besides hata sisi answar sunnah tulipeleka yetu lakini hayajachaguliwa,tena bora hayachaguliwa,kwa maana naona hao waliochaguliwa washaanza kulalama posho haitoshi,na CCM keshaweka mkono wake hapo,hata mngekwenda mngejidhalilisha tuh

Nendeni mkaendelee na ibada zenu tuh,forget about it.
 
Ushauri mzuri japo sikubaliani na mambo uliyoeleza kuhusu ccm
 
Back
Top Bottom