KakaJambazi
JF-Expert Member
- Jun 5, 2009
- 18,804
- 12,227
Waheshimiwa Watumishi wa Bwan, Nadhani kukaa kwenu kimya na kwa nukuu mliyotuonyesha haiwezi kuwa jibu sahii la kuiponya nchi yetu. Kwa vile Ikulu imeshawakana kwamba hamkuwasilisha majina kwa wakati ni bora maksema Ukweli.
Kumbukeni Mtumishi mwenzenu, Mzee Nathani aliposikia uovu uliotendwa na Mfalme Daudi hakukaa kimya kwa madai kama yenu kwamba hampaswi kuufunua uchi wa Baba mzazi. Ebu wasaidieni Watanzania na waumuni wote wajue ukweli wa nini kilichojiri. Siamini kabisa kwamba mnasema uongo, ni vema mngenyamza kabisa kuliko kulalamika halafu kisha mkatusomea mstari mmoja wa Biblia kwamba hataufunua uchi wa mzazi wenu. Ili kutibu majeraha yenu na sisi wafuasi wenu ni afya mkisema ukweli ili wahusika wafike mahali waombe radhi na kusameheana hadharani
Wamehofia biashara zao haramu zitaanza kufuatiliwa.