"IF YOUR LEGS CAN'T TAKE YOU TO PRAYER,THEN HOW DO YOU EXPECT THEM TO CARRY YOU TO PARADISE??"
nimeipenda hiyo hapo juu.
Lakini ukweli wa MUNGU kabisa kama kweli maaskofu wametumia mstari huo ku-justify tatizo hili naomba niwe wazi kabisa kuwa wamekosea saaaana na waombe radhi waumini wote wa kanisa la Tanzania kwa mhusika aliyetumwa kufanya kazi hiyo na asifanye!!!
1. Inapaswa maaskofu wajue kuwa waumini wana akili zao na wanamjua MUNGU sana na wanayajua maandiko vizuri sana. wao kuwa hapo walipo si kwa akili zao hata kidogo! kwanini wanataka kutumia akili zao wakati wanajua hawana za kutosha pasipo MUNGU??? Hata mimi naamini serikali haikusema uongo kuna kosa tu limefanywa na maaskofu.
2. Mtu anaetaka kujibu hoja zozote kihekima lazima apime mambo makuu ya hoja hiyo! Hoja hapa ni kupata katiba ya Nchi itakayotumiwa na watu wote wa imani zote, mtu mwenye kujibu kwa kumtumia Roho Mtakatifu katika hoja kama hii hawezi kabisa kutumia mstari huo!! huko ni kuchoka kiroho kabisa wala haihitaji kuuliza mtu!!!
3. Je Nabii nathan angesema nini mbele ya mfalme Daudi kama ukweli wa kuzini na mke wa Uria ulikuwa kumkosea MUNGU?
4. jE, Musa alipoamriwa kuwatoa wana wa Israel katika utumwa kule Misri angesemaje mbele ya Mfalme Farao? tena alimlazimisha mfalme awatoe watu wake!
5. Je, Shedrack, Meshak na Abednego tungewajuaje kama wangetoa majibu kama haya wakati wa utumishi wao kwa Bwana? maana wao walimwambia ukweli mfalme kama kufa na wafe lakini Mungu akawasimamia kwa kuwa walijua wajibu wao kwa Mungu wao na watu wao! mbona ninyi maaskofu mmshindwa kabisa kusimamia ukweli mbele ya Taifa hili lote? mimi nalia na mstari mlioutumia kujustify TAMKO lenu, it is not right at all!!!
6. Kama Daniel (mkuu wa wilaya wakati huo) huku akiwa Nabii na mtumishi wa MUNGU aliyetukuka alitupa chini heshima yake yote ya ukuu wa wilaya akadharauliwa ili Mungu atukuzwe ndani ya tundu la simba, vipi leo ninyi watumishi wa MUNGU mnasita kusema ukweli? kutetea wanyonge wa nchi hii? kutetea imani? kutetea haki za msingi za watu!, Je hamjui kuwa mwoga na mchawi na mzinzi wamewekwa kundi moja??? maandiko hayo mliyoyatumia hata kama mmekuwa waoga hamwoni kuwa sii sawa kabisa? tena mkatumia andiko moja tuuu! Hamkusoma YESU alisema ushahidi wa watu wawili wakubalika?
7. Je Stephano hakuuwawa kwa kutetea imani dhidi ya watawala? je aliwavua nguo wazazi wake?
8. Je Petro hakufungwa gerezani kwa kuwaambia ukweli watawala? YESU hakuwajibu mafarisayo juu ya hukumu zao na sheria zao juu ya watu? Soma Math. 23: 1 - 29 uone alivyowapa haki yao.
9. Je Paulo hakupigwa viboko 40 kasoro kimoja kwa kuwaambia ukweli watawala? kwanini ninyi mmeshindwa ilhali ni viongozi wa IMANI?
10. JE Yohana hakukatwa kichwa sababu ya kumwambia Mfalme ukweli?
11. Je kwanini mmetia mashauri giza?? enyi wana wa kizazi cha upotevu!!!
12. Mumewatwika watu wa Mungu mzigo mzito ambao ninyi wenyewe hamkuweza kuuchukua!! NENO hili lawafaa ninyi hasa katika wakati huu , Yer. 23:1 - 9!!! mmekumbuka mafungu ya 10 tu na kuwaita watu mbele ili muwaabishe wala si sheria ya MUNGU, lakini serikali mmeistahi! mumetubisha watu hadharani lakini serikali mumeiogopa!!
Kwasababu hiyo ya unafiki na kutenda haya yote mbele za watu, BWANA WA MAJESHI, MUNGU MWENYE NGUVU MFALME WA AMANI, amewaondolea kilicho chenu mahali pake!!! wala hamtafikia upeo wa mafanikio yake aliyowakusudia tena! ama sivyo mtubu na kuliambia kweli KANISA LA MUNGU hapa Tanzania! Nayo yamekuwa.
huu ni ujumbe wa BWANA anaetaka aweza kunipigia 0765 118 221