Uchaguzi 2020 Tamko la Baraza la Vyama vya Siasa - Oktoba 25, 2020

Uchaguzi 2020 Tamko la Baraza la Vyama vya Siasa - Oktoba 25, 2020

John Paul Shibuda

New Member
Joined
Oct 25, 2020
Posts
2
Reaction score
14
25 Oktoba, 2020

NASAHA ZA MWENYEKITI WA BARAZA LA VYAMA VYA SIASA – TANZANIA ZA KUSHAURI KILA MGOMBEA NA ZA KUSHAURI KILA CHAMA CHA MGOMBEA WAWE KISAIKOLOJIA NA FIKRA TULIVU ZA UTAYARI WA KUPOKEA MATOKEO YA KUSHINDA AMA KUSHINDWA KUPATA USHINDI WA NAFASI ZINAZOSHINDANIWA KWA VITI VYA UDIWANI, VITI VYA UBUNGE NA KWA KITI CHA URAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA NA KWA RAIS WA TANZANIA VISIWANI, MWAKA HUU 2020.

Kwa kuwa Uchaguzi ni fumbo la Kiini macho la Siasa za Uzimuaji wa hamasa za Vuguvugu za kushindania hisia na kushindania Imani za Wapiga Kura.

Na kwa kuwa sasa, tupo katika kipindi cha Lala Salama na hiki ni kipindi cha mwisho wa kukaririsha wananchi nguvu za hoja za ukweli halisia ama kukaririsha wananchi hoja za nguvu ya Uongo mtamu na za ukweli bandia. Na kwa kuwa siku ya mwisho ni tarehe 27 Oktoba 2020.

Na kwa kuwa siku ya kuwekezwa aliyewekeza nguvu za Hoja za kugusa hisia na kukonga mioyo na kuwa na umiliki wa mtaji wa Umma wa kushindisha maombi ya kura - kura za maamuzi ya kuwekezwa na wapiga kura ni tarehe 28 Oktoba 2020.

Kwa hiyo sasa, nami nimeamua kuchangia Ushauri kwa Wagombea na kwa wapiga kura ili kila Mdau muomba kura za Wapiga kura sasa, wajiweke sawa kwa kuwa na Uimara kwa Maamuzi ya kupatikana Uongozi Bora wa kuendeleza Ustawi na Maendeleo ya Jamii, Uchumi na Taifa letu.

Baada ya utangulizi elezeka hapo juu na kwa hiyo sasa, napenda nianze kwa kuwakumbusha ya kuwa kwamba, kuhusu Wagombea wa Kiti cha Urais wa Tanzania, tuna Wagombea 15.

Tanzania ingekuwa wagombea wa Kiti cha Urais hawa ni wa Timu ya mpira na wanachaguana apatikane Kampteni wa Timu ya Mpira nina uhakika kura nyingi za kupatikana Kapteni wa Timu ya mpira angeshinda Ndugu Dr. John Paul Magufuli.

Nimeanza na mfano wa kiti cha Urais wa Tanzania lakini hali hii ni kwa viti vyote vya kuchagulika. Napenda kufafanua ya kuwa kwamba hali na sababu ya kuchangulika kuwa Kapteni wa Timu ya mpira kwa Uchaguzi ya mwaka 2020, Mhe. Dr. John P. Magufuli, hii ni kwa hali ya mfano wa Messi au Ronaldino ambavyo wangependekezwa na wachezaji wenzao wawe ni Kapteni wa kuongoza Morali na kuongoza Ari ya Timu zao ipate ushindi kwa manufaa ya sifa Bora kwa Klabu zao za mpira.

Kutokana na somo la kuchaguana wachezaji wa mpira wanapo tafuta Kapteni wa timu yao na kwa kuwa kila Timu ya mpira wa miguu huwa na Fursa ya Nyezo zake za kujipatia Ushindi; Na kwa hiyo sasa, natoa Wito kwa Wanasiasa wajikumbushe yafuatayo; Haya yafuatayo ni ya Ushauri katika Fursa za kutafuta kuchagulika na kupata Ushindi wa matokeo ya kutolewa na Tume ya Uchaguzi.


(a) Kwanza kabisa kila mgombea wa kiti cha Urais wa Tanzania
na kila mgombea wa Kiti cha Ubunge na kwa Wagombea wote wa Viti vya Udiwani wa maeneo yote ya Tanzania.

(b) Na kwa hivyo sasa, Nachukua fursa hii kuwaasa kila Mgombea ajiandae kisaikolojia na kwa moyo mkunjufu kila Mgombea awe tayari kupokea matokeo ya Ushindi ama kupokea matokeo ya kushindwa kupata kura za Ushindi.

Kila Mgombea akubali somo la kwamba asiyekubali kushindwa siyo mshindani. Vile vile ikumbukwe kwamba mtu asiyekubali Subra za kuongozwa na mwenzake hana sifa za kuitwa Kiongozi wa Jamii.

Washindani wote wa nafasi za kushika mamlaka ya Dola, sasa kumbukeni kwamba Siasa siyo Imani za Kidini za kuenzi Nguzo kuu kwa Utukufu wa Mwenyezi Mungu. Kwa hiyo sasa, Wanasiasa tuache kufarakana kwa mambo yasiyo na thawabu kwa Mwenyezi Mungu.

(a) Kwa hiyo sasa, Wanasiasa wote na mashabiki wote wa
Vyama vya Siasa, hasa ambao hawatapata Ushindi kwa Wagombea wao, kumbukeni Usia usemao Kuvunjika kwa Jemba siyo mwisho wa Uhunzi.

(b) Kwa hiyo sasa, kama ambavyo Simba na Yanga hupeana
mikono baada ya kutifuana katika kushindania Ubingwa wa Taifa. Vivyo hivyo na Wanasiasa nawashauri tupongezane kwa kutakiana heri kwa matokeo ya kutokana na maamuzi matamu ama kwa kupatikana matokeo machungu ya Utashi wa Umma, yatakayotolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi.

Kwa Umuhimu wa pekee napenda kukumbusha Busara za Wanasiasa na Busara za Mashabiki wa Vyama vyote ya kuwa kwamba; kura za Ushindi kwa kila mshindi hazitotokana na kigezo cha Taswira ya hadhara zilivyokuwa katika vipindi vya mwitikio wa mahudhurio ya wasikilizaji wa mikutano ya kampeni.
Waafrika, Ikumbukwe kwamba ni mashabiki wa shangwe za Mikutano ya kampeni. Hii ni kwa sababu mikutano huwa na soga ama huwa na vimbwanga vya vijembe vya kukoleza Burudani za Mapiku ya Kisiasa.

Maajabu ya siku ya kupigwa kura hutoa somo ambalo lina jawabu la jibu lisemalo kwamba, kuwepo Umati wa watu wengi katika Mikutano ya Kampeni siyo Nyenzo ya matokeo ya Tarakimu halisia za namba za Takwimu za hesabu za Idadi ya Wapiga kura za NDIO na za kutoa Ushindi.

Kwa hiyo sasa, Ikumbukwe kwamba Wapiga kura wana vigezo vyao vya kutoa kura za ndio za kutoa Ushindi.

Na kwa hiyo sasa, Vigezo vya baadhi ya Wapiga kura, huwa zinajengwa na hoja za mitazamo ya kuoteshwa na dhana Mtambuka mfano hizi zifuatazo: -

Chema hujiuza, kibaya hujitembeza – kwa dhana za Uongo mtamu.

Siasa za Uongo hujenga kuundika dhuluma kwa Haki za Jamii kupata Ustawi na Maendeleo kwa kujengeka kwa maisha ya furaha ya leo na kesho. Naongelea Furaha ya kutokana na Umaana wa kwamba asiyefanya kazi na asile.

Wanasiasa kumbukeni kwamba, Wapiga kura akili zao ni sawa na Darubini za kupambanua maelezo ya kila mgombea wa kiti chochote kile. Kuanzia Udiwani, Ubunge hadi Kiti cha Urais wa Tanzania

Kwa hiyo sasa, katika kila mkusanyiko, Umma hupima maelezo ya kila mgombea, Je yana Mwanga Angavu kwa kumulikia madhila ya Taifa – Madhila ya Giza la adui ujinga, Adui Umasikini na Giza la adui maradhi na mengineyo ya kero kwa ustawi wa maendeleo ya Taifa.
Wanasiasa fahamuni kwamba, na kwa kila mkusanyiko Umma hujadiliana baada ya mikutano ya kampeni – Je, katika hawa Washindani ni yupi simulizi zake zina Viashiria vya Wingu la Giza kwa mjengeko Bora wa kupatika Utawala Bora wa Siasa safi za mjengeko wa kutoa Uongozi Bora. Umma unataka Utawala Bora kwa Ustawi na Maendeleo ya kuendelezwa Siasa Bora, hasa Siasa za kilio cha Wahanga wa Damu za madai ya Uhuru na za vilio vya damu za wahanga wa madai ya Mapinduzi matukufu ya Zanzibar.

Kwa hiyo sasa, Ifahamike kwamba wapiga kura inapokuwa ni muda wao wa Lala salama na ni ni muda wao wa kuelekea siku ya kupiga kura, hawa wapiga kura huwa wanabadilisha Ushabiki wa kutokana na Uchambuzi makini wa kutafuta nani ndiye anayefaa kuwa mjenga Ustawi wao na mjenga Ustawi wa Taifa.

Wanasiasa tambueni kwamba, kura za ushindi ni matokeo ya kura za shukrani kwa Siasa za mwanga angavu dhidi ya Siasa za Wingu la Giza. Wapiga kura ni waoga wa Wingu la Giza la kupofusha mwelekeo wa Dira ya maendeleo ya Taifa.

(a) Umma huwa hawatoi kura kwa Siasa za mtu muongo
anayesema ana uwezo wa kuona Gizani Paka mweusi aliyefumba macho yake.

(b) Kwa hiyo sasa, Wanasiasa nawakumbusha kwamba kila Mgombea apataye kura nyingi za ushindi huwa ni yule anayegusa hisia za Umma na anayekonga mioyo ya Umma. Kwa vielelezo vya kauli za kutoa ujumbe wa kuwa kwamba ana matendo ya sifa za hisia za Uzalendo.

Kwa hiyo sasa, Wanasiasa tambueni kwamba Wapiga kura hupenda Mgombea wa sifa za mfano wa Uzalendo wa kuneemesha nchi kupitia mali asili na Rasilimali za Taifa. Aidha ifahamike kwamba Maliasili na Rasilimali za Taifa ni mtaji wa kuwezesha usalama kwa azma ya kutimizwa kilio cha Uhuru - kilio cha Uhuru ni kujitegemea siyo mgombea wa Sera za kutambulisha Utawala wa kuwa na utegemezi kwa nchi nyingine zile, huyu hukataliwa na Wapiga kura.

Wanasiasa kumbukeni kwamba, Wanachi wanaogopa wagombea wavaa Siasa Umiza madai ya Wahanga wapigania Uhuru wa jamii na Uhuru wa Taifa.

Na kwa hiyo sasa, wapiga kura za ushindi huchagua chama cha mgombea wa Siasa chapa maendeleo ya Taifa dhidi ya Siasa chapa sumu kwa Uhai wa Tunu za Taifa na dhidi ya sumu kwa Tuzo za Siasa Ukombozi – zilizoasisiwa na waasisi wa Taifa la Tanzania.

Na kwa hiyo sasa kila Mgombea atakayepoteza Ushindi wake Atafakari na Ajiongeze, hivyo ajifahamu kwa kujiuliza Je, maelezo yake mbele ya Umma yalikuwa na Ombwe la Umaana wa Elimu ya Uraia, hivyo Siasa zake mbele ya Umma siyo Siasa za kuitwa ni Siasa Ongovu kwa Usalama wa Tunu za Taifa na kwa Usalama wa Tuzo za Siasa Ukombozi - Siasa zilizo asilishwa na Waasisi wa Taifa la Tanzania?

Wakati natafakari na Wanasiasa wenzangu kupitia vyombo vya habari kwa kifupi sana, nawaasa Wapiga kura wakubali kwamba, Taifa lenye kupona kutoka hadhi ya maisha Duni na maisha Dumavu ya kutoitwa Taifa endelevu, Tiba yake ni Umma kufunga mikanda. Na pale Pakunywa Tabibu za Siasa za Ladha chungu, Watanzania tuwe tayari kumeza ladha chungu inayoitwa ni ladha Tiba. Tukumbuke kwamba, maumivu ya mkulima ya leo ndio shangwe kwa furaha yake ya kesho. Hii ndio maana ya Mchumia juani hulia kivulini.

Ndugu Wananchi, kwa msisitizo maalum nawaasa wapiga kura wote watambue kwamba kiti cha Urais wa kila Taifa siyo chumvi ya kuonjwa kama chumvi imekolea katika Kitoweo na kila mtamani ladha ya mchuzi.
Kwa hiyo sasa, kila mpiga kura atambue kwamba, kila kura moja ya Uamuzi wa Hekima ni Ngao Kinga ya Lindo Bora kwa Usalama wa mafanikio yaliyopo ndani ya Jamii na ndani ya Taifa letu.

Kosa la kura yako mpiga kura ni majuto ya sawa na mfu abiria aliyepanda Gari la Gea kurudi kinyume – Nyume katika mwinuko wa mlima.

Athari ya kura ya sifa Potofu za kuitana mwenzetu na si mwenzetu ni kujenga matokeo ya mporomoko wa kuunda Janga la kusambaratika Kidira kwa safari yetu ya Uhuru ni kujitegemea.

Watanzania kumbukeni kwamba sumu haiwekwi jikoni. Kiti cha Urais wa Tanzania siyo asali ya kuchovya – chovya na kila kidole.

Mwisho Tulinde Amani yetu. Amani Tukiitunza - Itatutunza.

Ahsanteni.

Ndimi,



John P. Shibuda
Mwenyekiti
Baraza la Vyama vya Siasa – Tanzania.


Imetolewa Tarehe: …………………………


4917C525-39E6-4AD4-A39D-783E6DEF734C.jpeg
C193E8A4-BD14-4B41-AC6C-DEBB6637735F.jpeg
019D7F72-8E11-4B39-AF0E-30623FC8C8C7.jpeg

BF0AC2AD-E433-4A53-B0F3-1B7FAB5AE9E5.jpeg

6EE9101F-D1F1-4C4C-BA64-55B4FF699ACA.jpeg
9F9FBF57-12DA-4DF2-BAB7-599E269366EA.jpeg
2772526C-3BC9-4747-A2D6-2B59AB2F5097.jpeg
BF0AC2AD-E433-4A53-B0F3-1B7FAB5AE9E5.jpeg
 
Kuna watu wanafikiri hii nchi imejaa wajinga! Hivi hili unaweza kuliita Tamko? Baraza la Vyama linawesa kuwa na Tamko la kipuuzi hivi?

Hizi njaa zinauma kwa kiwango gani mpaka tunakuwa na watu wa hivi? Hata kama tumbo linauma alikuwa na nafasi ya kutafuta shibe kwa suala hili hili lakini angalau wanaosoma wakaona shibe ilitafutwa kwa akili!
 
Kuna watu wanafikiri hii nchi imejaa wajinga! Hivi hili unaweza kuliita Tamko? Baraza la Vyama linawesa kuwa na Tamko la kipuuzi hivi? Hizi njaa zinauma kwa kiwango gani mpaka tunakuwa na watu wa hivi? Hata kama tumbo linauma alikuwa na nafasi ya kutafuta shibe kwa suala hili hili lakini angalau wanaosoma wakaona shibe ilitafutwa kwa akili!
Sasa utafanyaje Ndugu yangu ndio washatamka Sasa dah [emoji23][emoji23]
 
Ndugu Wananchi, kwa msisitizo maalum nawaasa wapigakura wote watambue kwamba kiti cha Urais wa kila Taifa siyo chumvi ya kuonjwa kama chumvi imekolea katika Kitoweo na kila mtamani ladha ya mchuzi.

Ujumbe sahihi huu.. kwa muhusika.
 
Kuna watu wanafikiri hii nchi imejaa wajinga! Hivi hili unaweza kuliita Tamko? Baraza la Vyama linawesa kuwa na Tamko la kipuuzi hivi? Hizi njaa zinauma kwa kiwango gani mpaka tunakuwa na watu wa hivi? Hata kama tumbo linauma alikuwa na nafasi ya kutafuta shibe kwa suala hili hili lakini angalau wanaosoma wakaona shibe ilitafutwa kwa akili!
Hili jukwaa ni shule nzuri sana, na kuna watu wanaona mambo kwa marefu na mapana. Ubovu wa katiba inayompa mtu mmoja mamlaka yasiyo na mipaka katika kila jambo athari zake ndio hizi. Maprofesa na watu tuliodhani ni werevu wanajikomba ili tu wapate teuzi za mfalme aliyechaguliwa kwa kura za wananchi. Wachumia tumbo wanahama vyama wanatukana jukwaa lililowafanya wajulikane baadaye wanajikomba kwa mfalme ili wapate teuzi. Natamani sana kusema sasa basi kwa UJINGA huu kupitia boksi la kura. Tukipata kiongozi bora na siyo bora kiongozi tutafika, lakini kwa mazoea haya ya kuwa na mfalme katika nchi isiyo ya kifalme ni UCHURO
 
Mzee Shibuda umeeleza ukweli mtupu na sisi wananchi tumeapa kumpigia kura nyingi za KISHINDO JPM.

October 28th tutachagua MAENDELEO ya kweli na si mwingine wa kuyaleta ni JPM.

JPM ANATOSHA
CCM KWA MAENDELEO YA TANZANIA
 
Wewe Shibuda jifunze kuandika kwa kifupi ili watu wasome ujumbe wako kikamilifu na kuelewa. Usiandike kama shairi au tungo ndefu za kujaza kitabu ili kiwe na kurasa nyingi. Pili, usiwafanye wala usitake watanzania wawe kama kondoo, sisi ni watu wenye akili. Tatu amani haipatikani bila haki. Haki isipotendeka usitegemee watu watakubaliana na matokeo. Tukifanya kama unavyodhani CCM itatawa milele, na hili sio takwa la watanzania wengi.
 
MWISHO KABISA WAMESEMA

31. Watanzania tukumbukeni kuwa sumu haiwekwi jikoni, Nafasi ya Kiti cha Uraisi wa Tanzania Sio Asali ya kuchovya chovya na kila kidole


SIJUI WAMEMAANISHA NINI [emoji23]
Wanamaanisha kuwa yalikuwa makosa makubwa kumpa mamlaka Magufuli, chamoto tumekiona hivyo tusifanye makosa na kumrudisha.
 
Huyu Shobida yuko kazini. Sijui ni nani alimpa hiyo nafasi. Ni wale walio wengi kwenye mfumo ambao wanajifanya mpinzani. Vyema bus upinzani muwe makini sana sana katika kuongoza baadhi ya mambo yenu. Ninafahamu huyu Shibuda in and out. Sisemi mengi ila ni vyema upinzani mjitambue.

Ila mwambieni watanzania wa leo ni tofauti sana na wale waliowazoea.
 
Back
Top Bottom