Uchaguzi 2020 Tamko la Baraza la Vyama vya Siasa - Oktoba 25, 2020

Uchaguzi 2020 Tamko la Baraza la Vyama vya Siasa - Oktoba 25, 2020

Haya maneno aliyoongea Shibuda, juzi nimemsikia mgombea urais wa ADC naye kayasema hivyo hivyo. Inafikirisha mgombea wa urais anasema mshindi atakuwa wa chama kingine, kisha anasema hicho chama kingine kinachojaza kisidanganywe na nyomi. Hivyo vyama visivyo na nguvu, vyote vimepangwa na ccm ili kuwaandaa wapinzani wa kweli kuporwa ushindi wao.
Hayo maneno au tamko si la Shibuda. Ni tamko la umoja wa vyama vya upinzani. Ingekuwa ni ya Sjhibuda CHADEMA wanekanusha. Kumbuka CHADEMA ni sehemu ya hilo tamko, sioni kwa nini mashabiki wanashambulia.
 
Wewe unayetamka machafuko ndiyo utaingiza nchi kwenye machafuko. Yakianza utakimbilia Ubelgiji, utaacha wajinga wanapigana ili baadae uje ukatumbue. Watanzania wanajuwa zaidi. Hawawezi kuingia mtego wa kumsimika Mbelgiji Lissu akaweke madini yetu rehani.
Madini gani unayo ww, kama madini yangekuwa mali hivyo nchi hii ingekuwa masikini hivi.
 
Hayo maneno au tamko si la Shibuda. Ni tamko la umoja wa vyama vya upinzani. Ingekuwa ni ya Sjhibuda CHADEMA wanekanusha. Kumbuka CHADEMA ni sehemu ya hilo tamko, sioni kwa nini mashabiki wanashambulia.

Vyama vya upinzani vya kina Mrema, cdm Hawana muda na tamko la hilo kundi la wazee wahuni.
 
HAKI YAKO YA MSINGI KWENDA NA MTAKAE, KAMA LISU NI HAKI YAKO. ONDOA NENO SISI MAANA HILO NI NENO JUMUISHI. SEMA WEWE (MIMI) NA WENZAKO (WENZANGU). uNAPOSEMA SISI UNAMIJUMUISHA MIMI WAKATI MIMI SIKO UPANDE WAKO, NA NINA HAKIKA KUNA MAMILIONI HAWAKO UPANDE WAKO, INGAWAJE KUNA MAMILIONI PIA WAIYO UPANDE WAKO.
Uko sawa! Mara nyingi tunatumia lugha jumuishi!
 
MWISHO KABISA WAMESEMA

31. Watanzania tukumbukeni kuwa sumu haiwekwi jikoni, Nafasi ya Kiti cha Uraisi wa Tanzania Sio Asali ya kuchovya chovya na kila kidole

SIJUI WAMEMAANISHA NINI [emoji23]
hongera mkuu umesoma hadi point ya 31.,binafsi nimeishia ya pili haha
 
Mzee Shibuda umeeleza ukweli mtupu na sisi wananchi tumeapa kumpigia kura nyingi za KISHINDO JPM.

October 28th tutachagua MAENDELEO ya kweli na si mwingine wa kuyaleta ni JPM.

JPM ANATOSHA
CCM KWA MAENDELEO YA TANZANIA

Sema ww na familia yako, usitujumuishe
 
Hakika na wewe pia Mkuu maana kwa kukuona unaonekana MAENDELEO

JPM ANATOSHA
CCM KWA MAENDELEO YA TANZANIA

Kwetu hayo ndio maji yanatoka bombani, hayo maendeleo Sasa ni yapi kwangu kama hata maji tu lazima nichuje kwa dawa ya maji?
 
Attachments

  • 2020-10-25 09.17.05.png
    2020-10-25 09.17.05.png
    575.2 KB · Views: 1
Kwetu hayo ndio maji yanatoka bombani, hayo maendeleo Sasa ni yapi kwangu kama hata maji tu lazima nichuje kwa dawa ya maji?
JPM anakwenda kumaliza shida yote ya maji, mpaka sasa ipo miradi mikubwa ya maji katika utekelezwaji.

October 28th nenda kampe KURA MAGUFULI

JPM ANATOSHA
CCM KWA MAENDELEO YA TANZANIA
 
JPM anakwenda kumaliza shida yote ya maji, mpaka sasa ipo miradi mikubwa ya maji katika utekelezwaji.

October 28th nenda kampe KURA MAGUFULI

JPM ANATOSHA
CCM KWA MAENDELEO YA TANZANIA

Miaka mitano yote ameshindwa ataweza vipi hiyo mingine?

Ww kwenu Yanatoka maji kama haya? Hebu tuwe realistically kabisa
 
Miaka mitano yote ameshindwa ataweza vipi hiyo mingine?

Ww kwenu Yanatoka maji kama haya? Hebu tuwe realistically kabisa
Hata Lisuu hawawezi kufanya maajabu maana Development is the gradual process....JPM atatufikisha vizuri tunapopataka hebu tumpe kura za NDIO.

JPM ANATOSHA
CCM KWA MAENDELEO YA TANZANIA
 
Mzee wetu karibu sana jukwaani lakini usijekupotea kama viongozi na wanasiasa waliotangulia walivyolikimbia jukwaa.

Huku watu wanatumia akili kujadili na kuhoji, lazima utambue utakutana na hoja, maswali na changamoto utakazotakiwa kuzitolea maelezo na ufafanuzi. Kipimo cha ukomavu wako ni kuweza kuhimili na kupambana na hayo makundi ya watu, wengine wengi wameishia kutelekeza jukwaa.
 
Mzee wetu karibu sana jukwaani lakini usijekupotea kama viongozi na wanasiasa waliotangulia walivyolikimbia jukwaa.
Ha ha haaa! Walijifanya wanaomba maswali kutoka JF ili wafafanue sera na ilani zao, walipokutana na maswali nondo kutoka JF, hawajaonekana tena...Ha ha haaa! Ngudu Antipasu nadhani bado anatafakari namna ya kujibu maswali tuliyomuuliza hapa JF.
 
Hii imetokea kwa watu wa vyama vyote, si upinzani wala chama tawala, wengine naona wanajitahidi kuweka bandiko lakini hawawezi kujibu hoja na maswali kama ulivyoeleza, tulikua na wabunge, mawaziri na waheshimiwa wengi tu hapa jukwaani, wote wapo innactive.

Lakini JF ingekua ni uwaja mzuri sana wa wao kujijenga na kuongeza uwezo wao kwenye maeneo tofauti tofauti.
 
Lakini JF ingekua ni uwaja mzuri sana wa wao kujijenga na kuongeza uwezo wao kwenye maeneo tofauti tofauti.
JF ni pamoto sana....! Yaani unatwangwa maswali unaanza "kusikia miruzi masikioni"!!!

Hapa ni kweli ni sehemu nzuri ya kujifunza.
Nimefaidi elimu kubwa kupitia JF.
 
JF ni pamoto sana....! Yaani unatwangwa maswali unaanza "kusikia miruzi masikioni"!!!

Hapa ni kweli ni sehemu nzuri ya kujifunza.
Nimefaidi elimu kubwa kupitia JF.

Tunajifunza ustahimilivu na kuvumiliana pia, kuweza kukubali kukosolewa au kuwapokea watu wenye misimamo tofauti na wewe sio kitu kidogo.

Lakini ukifaulu ni dalili ya ukomavu.
 
Back
Top Bottom