Uchaguzi 2020 Tamko la Baraza la Vyama vya Siasa - Oktoba 25, 2020

Uchaguzi 2020 Tamko la Baraza la Vyama vya Siasa - Oktoba 25, 2020

Kikwete aliwahi kusema vyama mkiparurana mnalipa jeshi nafasi kuchukua nchi.
 
Karibu Sana Jamiiforums.com
Home Of Greater Thinker Dare To Talk Open

Yanayoendelea Sasa Hivi Bila Shaka Iwapo Uchaguzi Mkuu 2020,Utasimamiwa Wazi Na Haki ,Uughwana
Basi Wale Waende Wakaanze Upya Hasa Hasa Chama Kile Cha Pole Pole
 
Wengine tuna vitecno vya mchina hatuwezi kuzisoma hilo tamko wametamkaje?
 
Shibuda usituchanganye. Ulishajulikana na Watanzania wanajielewa kwa sasa. Tulia. Toka Enzi ukiwa mtumishi wa Bunge ukagombea huko baadaye ukatoswa kwa malengo ukaingia upinzani kwa malengo uliyotumwa. Ukashtukiwa ukakimbilia kwingine. Sasa na Baraka fake. Miaka inavyosonga mbele watanzania wanabadilika maana kile kizazi cha kutojitambua ndiyo kinaishia. CCM wenyewe wameshajitambua na mwaka huu tujiandae.
 
Ndugu Wananchi, kwa msisitizo maalum nawaasa wapigakura wote watambue kwamba kiti cha Urais wa kila Taifa siyo chumvi ya kuonjwa kama chumvi imekolea katika Kitoweo na kila mtamani ladha ya mchuzi.

Ujumbe sahihi huu.. kwa muhusika.
Kweli makosa ya 2015 ndo Mda wa kuyasahihisha
 

Shibuda ww ni mmoja kati ya watu watakaoingiza nchi hii kwenye machafuko kwa kushurutisha nchi hii kuongozwa na ccm. KANU ilikuwa inatawala Kenya hapo na wapambe wenye jumbe kama ww walikuwepo. Leo hii KANU haipo madarakani, na Kenya ina uchumi bora kuliko sisi. Hiki sio kizazi cha kuburuzwa na ccm, kizazi chenu kilishapita, leo mnakuja na jumbe za kulazimisha mumtakae akae madarakani ili muendelee kula. Mmekula jana yenu, na sasa mko tayari kumwaga damu ili mle leo yetu. Chaguo letu ni Lisu fanyeni mtakalo ila mabadiliko tuyatakayo tutayapata kwa utashi wetu, na sio kwa utashi wenu nyie wazee wasaka mlo.
 
Tutafute namna ya kuvifubaza hivi vyama vyote vinavyoshirikiana na ccm kuwakandamiza wananchi wa Tz

Haya maneno aliyoongea Shibuda, juzi nimemsikia mgombea urais wa ADC naye kayasema hivyo hivyo. Inafikirisha mgombea wa urais anasema mshindi atakuwa wa chama kingine, kisha anasema hicho chama kingine kinachojaza kisidanganywe na nyomi. Hivyo vyama visivyo na nguvu, vyote vimepangwa na ccm ili kuwaandaa wapinzani wa kweli kuporwa ushindi wao.
 
Watu tunajiandaa na uchaguzi Shibuda analeta riwaya humu.

Mzee afupishe tu, kuwa ama

1. Anaumuunga mkono Magufuli

2. Anasisitiza wananchi wajitokeze na kuwa na haki na uhuru katika kumalizia sehemu muhimu. Atakayeshinda atangazwe.
 
Mkuu John Paul Shibuda , karibu sana jf.
P
Kuna tatizo gani Paschal Mayala kuwa kada wa CCM. Kama ni kweli huo si uchaguzi wake. Mbona wewe ni kada wa CHADEMA. Kuna mtu ana matatizo na ukada wako na CHADEMA. Sisi sote ni Watanzania huru, na tuna uhuru wa kuwa wanachama au kushabikia chama chochote tunachotaka CCM ikiwemo. Kwani ni dhambi kuwa mwanachama na kada wa CCM. CCM na upinzani ni sawa na Simba na Yanga, au vilabu vingine vya michezo, tuna uhuru wa kujiunga na kushabikia kilabu chochote. Kwa hiyo achana na hiyo dhana kuwa kila Mtanzania lazima ashabikie upinzani hasa CHADEMA.
 
It is a form of spinning politics.
Andiko refu, na mwandishi anazunguka kuandika alichotumwa kuandika na CCM, wakati ujumbe wake umelenga kusema kidumu chama cha mapinduzi.
Upuuzi mtupu.

..Good observation.

..ila sijui mlengwa wa makala hii ni nani.

..Watz wengi hawapendi kusoma makala ndefu kama hii ya Mzee Shibuda.

..Na " chambo " alichoweka kwenye "ndoana " / makala yake sidhani kama kuna msomaji atakayekimeza.

..Mzee Shibuda amepoteza muda wake.
 
Back
Top Bottom