Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
TAMKO LA CCM KWA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2024
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeandaa tamko maalum kwa ajili ya uchaguzi wa serikali za mitaa wa mwaka 2024. Uchaguzi huu ni muhimu kwa maendeleo ya nchi yetu, kwani utahusisha kuchagua wenyeviti wa mitaa, vijiji, vitongoji, wajumbe wa kamati za mitaa, na wajumbe wa halmashauri za vijiji. CCM imeweka wagombea katika nafasi zote, ikiwemo vijiji 12,280, mitaa 4,264, na vitongoji 63,886
Katika tamko hili, CCM imeeleza mafanikio yaliyopatikana chini ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2020-2025. Mafanikio haya ni pamoja na kuimarisha miundombinu, kuboresha huduma za afya na elimu, na kuongeza fursa za ajira kwa vijana. Aidha, tamko linaeleza mikakati ya chama katika kuhakikisha ushindi na kuendelea kuleta maendeleo kwa wananchi wote.
CCM imefanikiwa kuweka wagombea katika nafasi zote zilizogombewa, huku upinzani ukiweka wagombea katika 38% ya nafasi zote. Katika uchaguzi uliopita, CCM ilishinda katika vijiji 12,260 sawa na asilimia 99.9, mitaa 4,263 sawa na asilimia 100, na vitongoji 63,970 sawa na asilimia 99.4
Tamko hili pia linaelekeza wagombea wa CCM kuhusu mambo muhimu ya kuzingatia katika uchaguzi, ikiwa ni pamoja na ushirikiano na wananchi, uimarishaji wa miundombinu, na kutoa elimu kwa wananchi kuhusu umuhimu wa kushiriki katika uchaguzi.
CCM inawaomba Watanzania wote waendelee kuiamini na kuwachagua wagombea wake ili kuendelea kuleta maendeleo kwa wananchi katika maeneo yote ya nchi yetu.
Kwa kuhitimisha, Ikumbukwe, CCM ndio chama pekee kati ya vyama vyote vya siasa nchini Tanzania ambacho kimefanikiwa kutoa tamko kwa watanzania wote kuhusu chama chao kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa 2024. watanzania wengi wamevutiwa na hatua hii kwa kuwapongeza viongozi wake wakuu wakiongozwa na Mwenyekiti wao Dkt Samia Suluhu Hassan