Asante Mh. Dr. W. P. Slaa, ubarikiwe. Kwangu mimi binafsi, familia yangu, ndugu zangu, wafanya kazi wenzangu, watanzania wenzangu na rafiki zangu popote walipo nchini Tanzania na nje ya Tanzania, wewe ni shujaa wetu. Wananchi wametimiza wajibu wao wa kikatiba wa kumchagua kiongozi wanayeamini ana uwezo wa kuwaongoza katika kipindi cha miaka mitano kutoka 2010 mpaka 2015 lakini uamuzi wao unataka kuchakachakuliwa na waovu wasioitakia mema Tanzania. Badala yake waovu hawa wanatafuta kila njia ya kujikwamua kwa kung'ang'ania madaraka bila kujali matakwa ya wananchi kwa njia za giza, ulaghai, wizi wa kura na nguvu za dola. Hata hivyo tuna imani kuwa moto uliouwasha hautazimwa hivi hivi wala taa ulioiwasha mwanga wake hautatoa nafasi kwa giza hili zito lililo mbele yetu. Kwa hili hatukati tamaa, a luta continua !