Tamko la jeshi la polisi na Madai ya Mange Kimambi yanashabihiana kwa kiasi kikubwa

Samiaagain2025

JF-Expert Member
Joined
Dec 2, 2020
Posts
4,834
Reaction score
5,310
Ukiyatafakari kwa kina matamko ya jeshi la polisi na madai ya Mange Kimambi utagundua kuwa;
Ni kweli polisi wamepanga kuwakamata wanasiasa baadhi wa chama cha upinzani na wengine wachache sana(au mmoja tu) wa chama tawala pamoja na baadhi ya viongozi wa dini.

Haya matamko ya leo ni maandalizi tu endapo watawakamata tufahamu ya kuwa walikuwa wanaratibu mambo ya vurugu au maandamano.
Hii si kweli.

Ifikie mahali Baraza la usalama la Taifa likae chini litafakari kama njia hii ya kukamata watu na kuwapa kesi nzito za uongo, kuteka na kuua inalinufaisha taifa letu au watu wachache ambao ipo siku watakufa na kuiacha Tanzania.

Sisi sote ni watanzania na hakuna mtanzania bora kuliko mwenzake.
CC: CDF
IGP
DGIS.
 
Polisi wanapiga ramli,hawana weledi wala intelijensia.
Wanatumia nguvu nyingi kuliko akili
 
Binafsi napendekeza yeyote atakayevuruga amani ya nchi hii, ashughulikiwe accordingly!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…