I am Groot
JF-Expert Member
- Jul 20, 2018
- 3,929
- 10,747
IBARA YA 16:
(1)Wanaume na wanawake waliotimiza umri wa utu uzima, bila kujali uasili, uraia au dini wana haki ya kuoa na kuolewa na kuanzisha familia, wanapaswa kuwa na haki sawa katik ndoa.wakati ndoa inaendele au ikivunjika.
(2)Ndoa itafungwa tu pale wanandoa watakapokuwa wamekubali kwa hiari yao wenyewe.
(3) Familua ni kundi la msingi na la asili la jamii na inapaswa kulindwa na jamii pamoja na taifa.
IBARA YA 17:
(1) Kila mtu ana haki ya kumiliki mali yake binafsi au kuwa pamoja na watu wengine.
(2) Hakuna mtu atakaenyang'anywa mali yake bila sababu.
IBARA YA 18:
Kila mtu ana haki ya uhuru wa kufikiri, hisia na dini, hii haki inajumuisha uhuru wa kuielezea dini yake au imani kwa kufundisha , kutenda au kuabudu na kukiri iwapo ni kibinafsi au katika jumuiya na watu wengine.
IBARA YA 19:
Kila mtu ana uhuru wa kutoa maoni yake na kujieleza. Haki hii inajumuisha uhuru wa kusimamia maoni yake bila kuingiliwa na kutafuta, kupokea na kutoa habari na mawazo kupitia vyombo vya habari vya aina yoyote bila kujali mipaka.
IBARA YA 20:
(1) Kila mtu ana haki ya uhuru wa kukutana na watu wengine na kujumuika kwa amani.
(2) Hakuna mtu atakaelazimishwa kujiunga na umoja wowote.
IBARA YA 21:
(1)Kila mtu ana haki ya kushiriki katika serikali ya nchi yake moja kwa moja au kupitia wawakilishi waliochaguliwa kwa uhuru.
(2)Kila mtu ana haki ya kupata kwa usawa huduma za umma katika nchi yake.
(3) Matakwa ya watu nduo yatakuwa msingi wa mamlaka ya serikali, hii itajieleza katika chaguzi za vipindi na za kweli ambazo zitakuwa kwa wote na kwa haki na zitafanyika kwa kura za siri au kwa njia huru za kura zinazofanana na hiyo.
IBARA YA 22:
Kila mwanajamii ana haki ya kupata hifadhi ya jamii na anapaswa kupokea kupitia juhudi za taifa na ushirikiano wa kimataifa nakulingana na shirika au rasilimali za kila taifa kwenye haki za kiuchumi, jamii na utamaduni ambazo ni lazima kwa hadhi yake na maendeleo dhahiri ya utu wake.
IBARA YA 23:
(1) Kila mtu ana haki ya kufanya kazi, uhuru wa kuchagua kazi, mazingira ya kazi yenye haki na ya mafao na kulindwa dhidi ya kutokuwa na kazi.
(2) Kila mtu ana bila ubaguzi ana haki ya kulipwa sawa kwa sawa na kazi anayoifanya.
(3) Kila mtu aliyeajiriwa ana haki ya kupata malipo ya kazi yatakayo mhakikishia yeye na familia yake kuishi kama binadamu na kuongezewa ikibidi aina nyingine za hifadhi ya kijamii.
(4) Kila mtu ana haki ya kuanzisha na kujiunga katika vyama vya wafanyakazi kulinda maslahi yake.
IBARA YA 24:
Kila mtu ana haki ya kupumzika na starehe pamoja na muda maalum wa saa za kazi na vipindi vya likizo zenye malipo.
IBARA YA 25:
(1) Kila mtu ana haki ya kuwa na hali nzuri ys maisha inayofaa kiafya na maisha yake kwa ujumla ikijumuishwa na chakula , mavazi, malazi na haki ya kupata tiba na hifadhi za jamii zilizo na lazima. Pia haki ya kuhifadhiwa anapokosa ajira ,akiwa mgonjwa , mlemavu, mjane, mzee au hali nyingine yeyote itakayoyatishia maisha yake kwa kiasi asichoweza kujisaidia.
(2) Hadhi ya kuwa mama na utoto vinapaswa kupewa uangalizi maalum na kusaidiwa. Watoto wote hata kama wamezaliwa ndani au nje ya ndoa wafaidi sawa na ulinzi wa kijamii.
IBARA YA 26:
(1) Kila mtu ana haki ya kupata elimu.Elimu itatolewa bure, angalau elimu ya msingi. Elimu ya msingi ni lazima kwa kila mtu. Elimu ya ufundi na elimu ya juu itakuwepo kwa ujumla na iwe inapatikana kwa wote kulingana na uwezo.
(2) Elimu ielekezwe katika kumkuza mtu kufikia hadhi kamili kama binadamu na kuimarisha heshima ya haki za binadamu na misingi ya ya uhuru wa mtu. Ikuze mawasiliano, uvumilivu na urafiki kati ya mataifa , asili, na vikundi vya dini na iendeleze hatua za umoja wa mataifa wa kulinda amani.
(3) Wazazi wana haki ya mwanzo ya kuchagua ni aina gani ya elimu itakayotolewa kwa watoto wao.
IBARA YA 27:
(1)Kila mtu ana haki iwapo atapenda kushiriki katika masuala a utamaduni katika jumuiya yake kufurahia sanaa na kushiriki katika maendeleo ya kisayansi na mafao yake.
(2) Kila mtu ana haki ya ulinzi wa utu wake na vitu vyake anavyopendelea vinavyotokana na sayansi, fasihi, vitu vya sanaa ambavyo yeye ndio mwandishi wake.
IBARA YA 28:
Kila mtu anastahili utulivu katika jamii yake na kimataifa ambapo haki na uhuru wake utatolewa kwa tamko hili utapatikana.
IBARA YA 29:
(1) Kila mtu ana wajibu katika jumuiya ambayo uhuru na maendeleo kamili ya utu wake yanaweza kupatikana.
(2) Katika kufaidi haki na uhuru kila mtu atakuwa chini ya mipaka ya sheria kwa ajili ya kupata uwezo wa kuheshimiwa kwa haki hizo na uhuru wa watu wengine na pia kulingana na utu, taratibu za jamii nzima katika jamii ya kidemokrasia.
(3) Hizi haki na uhuru hutolewa zisitumiwe kinyume na misingi na malengo ya umoja wa mataifa.
IBARA YA 30:
Hakuna chochote katika tamko hili kinachopaswa kutafsiriwa na nchi yoyote, kundi la watu au mtu yeyote ili kumaanisha kuharibu haki na uhuru uliotolewa.
****** ****** ******
Tazama pia:https://www.jamiiforums.com/threads...la-haki-za-binadamu-lhrc-sehemu-ya-1.1809658/