"Tamko la Pinda"

Pinda amekiri na naungana nae kabisa kuwa amekuwa Muungwana na kujenga imani kwa WaTanzania kuwa alichosema ni kweli kilisemwa nae.Pia nimefarijika kuona amerudi na kuifuta kauli yake ,kwa ufupi amezidisha mapenzi kwa WaTanzania,ila mapenzi yatazidi ikiwa atarudi kwa muangaza mwengine ambao utafuta kabisa mauaji ya Albino ,elimu anayo na uwezo pia anao.
Hayo ni ya Mh.Pinda.
Ila huyu Mkwere mpiga mirunzi nae ametenda kosa kama hilo kwa kusema ataenda kuwatesa watu wa Zanzibar 2010 ,nae vipi hebu angalieni maneno yake.

Mhishimiwa Rais anasema:
"Nasema mwaka 2010 tutatesa" "hatuna sababu ya kushindwa", maendeleo yaliofikiwa ni makubwa ninafurahi kuwa tulioyaahidi tumeyatimiza na mengine tutayatekeleza bado tunaendelea," alisema.

"Nasema mwaka 2010 tutatesa"

Si dhani kuwa neno "kutesa" ni lenye kwendana na kanuni (sharia). WanaJF mnaojua sheria mnaweza kutupa maelezo kisheria kuhusiana na utawala wa sheria.
 
Ahaaa! Sasa nimesikiliza hiyo sijui hotuba au maelezo yake bungeni. Kwa jinsi watu mnavyoiweka hapa ni kama vile Pinda alikuwa analia (bawling) uncontrollably. Hapana, Pinda alikuwa choked up. Kuna tofauti kubwa sana kati ya ku choke up na ku bawl.

Sasa watu wengine hapa mnafanya ionekane kama vile Pinda alibubujikwa na machozi. Hapana bana. Kwangu kulia sio hoja hata kidogo. Hoja na kilicho cha msingi hapa ni hatua gani za dharura zilizochukuliwa kukomesha unyama huu.

Mmekuwa so caught na huko so called kulia hadi mmesahau yaliyo ya muhimu. Kwa mfano, ni waziri yupi hasa anayehusika moja kwa moja na usalama wa wananchi? Yeye katoa tamko gani?

Kosa la Pinda sio kuzidiwa na hisia bungeni. Kosa lake ni kauli alizotoa. Na kama bado hajazikana (kuzifuta hawezi kwa sababu keshazitoa) na kuomba radhi, basi hapo mimi nalia naye mpaka kieleweke.
 

baada ya kumsikiliza unafikiri alijibu swali.. ukisikiliza vizuri ameomba radhi kwa kusema

"kama Watanzania wanaona uovu niliousema ni mkubwa kuliko uovu unaofanywa naomba samahani. Mungu anisamehe lakini nia yangu ilikuwa nzuri kabisa"!
 

Mkuu nimegundua unapenda sana kulia kama Pinda....
 

Uhuhuhuhuuuuu...ooohohohohooooo...ebana Steve naona jamaa ka-kumind ulivyotoa "thanks" kwa Icadon....ihihihihihiii...he (she) is very sensitive today so be careful not to hurt his (her) feelings again...
 

Watanzania hatuna.. now there is the hypebole. Sasa Pinda siyo Mtanzania. Uandishi mwingine crummy and cheezy.
 
Watanzania hatuna.. now there is the hypebole. Sasa Pinda siyo Mtanzania. Uandishi mwingine crummy and cheezy.

Nimesema toka jana, sijui juzi, kwamba Pinda ndio kaanzisha!!

Watanzania huwa hatuna hulka ya kujilizaliza kwenye podium tukikumbwa na public firestorm. Again, nimesema four hundred times, Pinda ndio ana set precedent!

He is erratic. Hana emotional steadiness or the judgment to hold office of Prime Minister.
 

Vilevile hili suala ni lazima tuliangalie kijamii. Hili tatizo sio limetambaa nchi nzima. Kuna Epicenter ya matatizo haya. Je jamii katika sehemu hizo zinafanya juhudi gani kutatua matatizo hayo ???
 

Ume scour Tanzania nzima na kuhitimisha kwamba Pinda ndio kaanzisha? Mijitu mingine bana...
 

Unajua kilichomfanya Pinda azidiwe na hisia ni nini? Ni alichokiona kuhusiana na ma albino au ni utata ulioanza kutokana na kauli zake? Kama hujui usiseme kama vile una mamlaka! Hivi wewe ukoje?
 
Nimesema toka jana, sijui juzi, kwamba Pinda ndio kaanzisha!!


kwamba katika utafiti wa Watanzania wote ni yeye wa kwanza kulia hadharani kati ya wanaume.

Watanzania huwa hatuna hulka ya kujilizaliza kwenye podium tukikumbwa na public firestorm.

Watanzania wangapi wamekumbwa na firestom na wakapata public podium? ili tulinganishe.

Again, nimesema four hundred times, Pinda ndio ana set precedent!

I don't think so. Hakuna precedent ya kulia duniani iwe hadharani au mafichoni. Mtu hulia anapolia.

He is erratic. Hana emotional steadiness or the judgment to hold office of Prime Minister.

wrong. Si kwa sababu ya kulia! Kulia hakuoneshi character ya mtu au emotional steadiness. Inaonekana hujasumbuliwa na kile anachodaiwa kusema unasumbuliwa na yeye kulia.
 
Vilevile hili suala ni lazima tuliangalie kijamii. Hili tatizo sio limetambaa nchi nzima. Kuna Epicenter ya matatizo haya. Je jamii katika sehemu hizo zinafanya juhudi gani kutatua matatizo hayo ???

tatizo hili lina impact nchi nzima, siyo tu kuwa lina epicenter.. chora ramani ya mauaji ya albino utashangaa.. lakini hilo dogo. Implication ya kuendelea kwake ni dire kwa taifa zima. So, hatuwezi kulireduce to local areas. Hili ni suala la kitaifa.
 

Hahahahaha...now I see why you graduated Summa Cum Laude at the you know who Institute of Advanced you know what because you have talent on loan from God only...ahahahahahaaaa
 
Hahahahaha...now I see why you graduated Summa Cum Laude at the you know who Institute of Advanced you know what because you have talent on loan from God only...ahahahahahaaaa

and "I'm doing this with half of my brain tied behind my back just to make it fair!" Our institute is doing very so far my fellow student.
 
...Nampongeza waziri Mkuu kwa ujasiri aliouonyesha. Huhitaji kuishi na mtoto/mtu mwenye Albinism kutambua machungu na kadhia ya mauaji ya hao Albino...

 
Sidhani kama Pinda alilia kwa bahati mbaya...Inawezekana ni ka usanii flani hivi...Wapinzani wawe makini otherwise inaweza ku backfire kwasababu issue ya Albino imewagusa watanzania sana na kama kulia wamelia wengi na kama maneno kama aliyosema Pinda ambayo ni ya ku wish kuwa wauwaji hao nao wakikutwa wanafanya mauwaji hayo nao wauwawe ni maneno ambayo nadhani yemeshasemwa na watanzania sehemu mbali mbali either majumbani ama vijiweni nk.

Kwa hiyo kuna uwezekano mkubwa sana wa Pinda ku connect na wananchi licha ya kwamba sisi tunaona kachemsha kisheria ama ki ethic....Kwani si wananchi hao hao wanao wauwa vibaka wezi wa kuku? Muullize mwananchi huyo machungu atakayokuwa nayo kwani kuku huyo pengine alikuwa ni wa sherehe ether krismasi ama idi ama graduation ya mtoto ama mjukuu kumaliza darasa la saba ama form four nk. Ni kwamba kuku huyo kwa wengine ni big deal kiasi cha kutoa maisha ya mtu mwingine? Tujiulize...Nani anaye connect na wananchi hapa? Vipi kuhusu wanao commite murder? Sina hata haja ya kusema albino kwa sababu albino or no si bado ni wanadamu?

Hii ni 09,Kwanza alianza kwa kuwafungia leseni waganga wa kienyeji, Kwa upande mwingine hapo wananchi walio wengi ambao ni wapiga kura lazima wanasupport,issue ishakuwa kubwa kwa serikali na hata kulia kwa Mh Pinda ni tabia ya hao wazungu kama wengine wanavyosema...Then tujiulize unafikiri wazungu hao nao hawafuatilii? Hao mnaowaita wafadhili ambao Mh Rais kasema ni lazima asafiri kuwaomba misaada,unadhani hataulizwa? Si atasema mnaona hata waziri mkuu kalia na waganga wamefungiwa? Jiwe moja ndege wawili...Wafadhili na wananchi.

Kwa ujumla ni issue ambayo wapinzani inabidi wawatch their steps kwani serikali ya ccm ni maaruu sana kwa kuplay na emotions za wananchi wa Tanzania.
 

Hujui kwa uhakika ni nini kilichomfanya Pinda kuonyesha hisia.
 
kwamba katika utafiti wa Watanzania wote ni yeye wa kwanza kulia hadharani kati ya wanaume.

Mfumo dume!!

Wewe nitajie basi, mwanamke au mwanamme, toka the founding of the nation, mtu aliyekumbwa na public repudiation akaenda kulia kwenye stage.
Watanzania wangapi wamekumbwa na firestom na wakapata public podium? ili tulinganishe.

Ulimbukeni!

Ulinganishe na nani? Sio lazima utupime na wengine. Sisi Watanzania, bila kuangalia through the prism ya tamaduni nyinginge, sisi wenyewe hatulilii hadharani tukikumbwa na kashfa!!

I don't think so. Hakuna precedent ya kulia...

Pinda kafungua dimba la kitabia cha kutumia pulpit kujilizaliza amidst a public debacle. Kama kuna mwingine nitajie basi!!!

Kulia hakuoneshi character ya mtu au emotional steadiness...Inaonekana hujasumbuliwa na kile anachodaiwa kusema unasumbuliwa na yeye kulia.

"Character"? Nani kasema Pinda ana luck character? Nimesema Pinda is erratic.

Sisumbuliwi na kile alichosema? Sasa kwa nini ningesema Pinda hana judgment to hold the office of Prime Minister?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…