Ushirombo
hili tatizo la wabongo ni kubwa sana? How many PMs should resign for you to know its not worth it?? Kujiuzulu maana yake nini haswa? Acheni ushabiki wa kimichezo!! Kama PM kaongea bungeni tayari what else do you want him to explain?
Nadhani hapa tunajipotosha tu... watanzania tunapenda kujadili mambo ambayo suluhu yake ishapatikana kuliko yale yanayohitaji tuyatatue... Lets please discuss some other things lakini sio hili!!
Kama ni kujiuzulu how will it help the Albinos??
Hii inahusu uhai wa binadamu wenzetu sio FA Premiership wala UEFA cup! Lets talk sense and think wise!!
I admit hata mi ningekuwa katika position yake i would have just said the same on the people who kill albinos! Things that are happening out there are not any better, they are evil..very evil and inhuman!!
Mungu Ibariki Tanzania... Mungu Ibariki Afrika!
Ndugu hapa watu wanazungumzia sheria,hivyo inatakiwa akili yako iweze kupambanua juu ya alichokitamka Mheshimiwa Pinda ,kwani hata huko Bungeni aliambiwa ni sawa lakini si sehemu yake ,na ndio maana ameomba msamaha,ile kuomba msamaha peke yake inatakiwa mimi na wewe tusio waelewa wa sheria tujue kwamba jamaa amevunja sheria,na ndipo hapo utawala wa sheria unapojengeka na kukubalika kwenye jamii na ndio hapo wengine wanapoanza kuchukuliwa sheria,kwa maana zinatakiwa zifuatwe na sio kuburugwa.
Mheshimiwa amekiri ,hivyo baada ya kukiri ni lazima taratibu zifuatwe ili aonekane kama amefanya kosa na iwe somo kwa wengine pia,kujiuzulu hilo lisikupe shida sana,kwani ni lazima litumike neno hilo ili kumuweka sawa muheshimiwa asione hii nchi ni yake na yeye anaweza kusema atakavyo ,hapo ndio litakuwa fundisho kwa wenye kutumia kauli zinazoashiria vitendo viovu,na wengine nao wataelewa kuwa sasa mambo yamebadilika,
kiongozi wa Serikali ajue anazungumza kama kiongozi wa Serikali na sio raia wa kawaida au kiongozi wa Chama chake,Pinda ameenda mbali baada ya kuamuru vijana wa CCM japo amejitetea,lakini kanda sivyo ilivyo.
Viongozi wanatakiwa wawe wanaongozwa na sheria na wawe wenye kuzifuata kimaadili na sio jazba kwani mwisho wa jazba ni kuliweka Taifa kwenye mgawanyiko.Na kama unavyoona kuwa sasa tumegawanyika kuhusu kauli ya Pinda.
Kwa upande wangu naona kitendo kilichofanyika kwa Mizengo Pinda kinastahili sifa kwa wabunge wetu,kwani ile peleka peleka ya mapolisi kwenda kupiga raia nayo itaweza kukoma kwa viongozi wa mikoa au vyama kuamrisha polisi wafanye watakavyo katika kupambana na waandamanaji.
Ni kauli za namna hii ndizo zinazowapa polisi kufanya kiburi,maana watakwambia sisi tumetumwa na ndio tupo kazini nani anaewatuma ni viongozi wenye kauli kama za Pinda...Mkiwaona wapigeni na hata risasi wapigeni ndio hayo yaliyotokea Pemba na hata Tanganyika siku hizi yameanza kuonekana kwa polisi kutumia nguvu za ziada kwa kuwa tayari wameshapewa maelekezo.