Masanja,
Lakini hapa tunamuongelea Waziri Mkuu! Na kama Ogah alivyosema huwezi halalisha ujinga wa Bush kwa ku-compare madhambi ya Pinda..Ndo maana leo Obama anabadilisha kila kitu cha Bush..kwa sababu hata wanaomsupport Bush..wana-admit kwamba jamaa alichemka.
Mkuu Obama hakuja kupinga usemi wa Bush wala hakuwahi kusema ule ni Ujinga... hakuna kiongozi hata mmoja aliyempinga Bush katika usemi ule...na hakika record itaonyesha hata yeye Obama alisema akisikia Osama yuko mahala fulani ndani ya Pakistan ataruhusu majeshi yake akiwa kama C in C, kumuua bila idhini ya Pakistan ikiwa wao watashindwa...We will defeat Al Qaeda ndio usemi wake mkubwa na mwenye kuelewa maana anajua kinafuata kipi..
Hayo ni ya Marekani, lakini my point inapinga jinsi sisi wananchi tunavyochukua maamuzi yetu haraka bila kufikiria na binafsi hata tamko letu AJIUZURU linatangulia sheria hivyo naweza kusema tumekosea..
Nakumbuka Mwinyi kuna wakati aliwahi kusema kule Songea akiwahamasisha wananchi walime Korosho alisema hivi:- Wananchi kazaneni ktk Mikorosho na watu wakaichukulia out of context..Unajua tena yaliyofuata..
Mkuu nakubali Pinda kashemsha isipokuwa najaribu kuwafahamisha kwamba hii ni cheap shot kisiasa na hata ukitazama vibaka wanaokamatwa na kuuawa nchini hakuna kiongozxi hata mmoja aliyesimama na kusema wauliwe, sisi wananchi wenyewe tunachukua sheria mkononi na hii inaendelea hadi kesho.. Double standard ni pale tunapoweza kuua vibaka kwa kuwapiga mawe lakini tunapinga kauli tu ya Kiongozi ambaye mimi binafsi nimemsoma alikuwa akimaanisha kitu gani, besides kama sikosei kawaomba samahani ikiwa amewapotosha...
Tukirudi ktk issues nyinginezo tumezungumza humu kuhusu Lowassa, Mkapa na wengine wafilisiwe, waende jela na kadhalika haya yote ni maneno yanayotangulia sheria lakini haina maana tuna maanisha wafungwe na kufilisiwa bila sheria..Mkapa aliwahi kusema kuhusu Machafuko ya Zanzibar kutumia nguvu ya Dola na akatumia kweli lakini sikusikia Mtanzania (hasa Wabara) wakisimama kuom,ba ajiuzuru, Wauaji ya Mwembechai, Mrema na majambazi haya yote ni matendo machafu ambayo hayakufuata sheria tulishindwa kuyakemea badala yake tuliwasifia viongozi hawa, leo Pinda kasema tu wanaoua Zeruzeru wauawe imekuwa kosa kubwa ambalo halina hata msamaha kwetu..
Double standard ni sisi wananchi mkuu wangu, Pinda kasema alosema na hakuna mtu hata mmoja ambaye kisha chukua hatua ya kuua watu ovyo, ikiwa na maana wananchi wanaelewa kuwa Mh. Waziri mkuu hakuwa akizungumza na wananchi direct kuwaambia wachukue sheria mikononi mwao..lakini on the other hand sisi tunaendelea kuua vibaka bila hata kuuliza sheria inasema vipi na hakuna heading hata ktk gazeti moja likiwaomba wananchi kuacha vitendo hivyo!.. Kesho ukienda Kariakoo na ukaitiwa Mwizi watakuua...Hii law imepasishwa na wananchi na sisi tumeshindwa kuwakemea viongozi wetu kuhakikisha vitendo hivi havifanyiki..
Nazidi kusema ni kawaida ya binadamu kutanguliza hukumu inayotakiwa kulipa maovu ya mhusika hata kama wanafahamu ni lazima mhusika atinge Kisutu kwanza..Kuna maneno mengi yamesemwa na kina Mbowe kuhusiana na Utawala huu, kama vile kuingia msituni, afadhali ya Mkoloni na hata Dr.Slaa ambaye kama nakumbuka vizuri alisema kipigo alichopata Mtikila huko Tarime ni size yake..Haya ni maneno ambayo yanatangulia sheria haina maana kabisa kuwa kiongozi huku anasisitiza watu waendelee kufanya madhambi hayo...
Pinda alichemsha?.. Ohhh Yes, lakini kosa lake ni swala la kufahamu tu kuwa hakuwa na maana zaidi ya wito kwa sheria kutumika kutoa adhabu kali...