Hapana! Ninachomaanisha ni kwamba kama wewe ni mtoto wa masikini kitu pekee kitakachofungua Dunia yako ni ufaulu wako wa Shule/Chuo hayo mengine yote ya vipaji yapo lkn ni wachache sana wanaofanikiwa kwa njia hiyo hasa wale masikini kwa maana wewe kama masikini ina maana hauna refa au mtu wa kukushika mkono na kukupa kazi au kukutambulisha kwa watu wakubwa hivyo njia pekee ya wewe kupenya ni kupitia Ufaulu wako tu hakuna njia nyingine kwa mtoto wa masikini!
Hivyo mimi nikija kubahatika kupata mtoto nitamwambia hakuna kulala ni kusoma tu kwani hiyo ndiyo njia pekee ya mtoto wa masikini kwenye nchi ya kimaskini ya kutoka na kufika mbali hapa Duniani!